mr pipa
JF-Expert Member
- Jul 26, 2021
- 2,332
- 4,858
Kuna jirani yangu mmoja amewawekea msimamo na katazo kwa watoto wake kutoangalia television, na mwanzoni popote anapowakuta wanaangalia huwatandika sana viboko.
Katika sababu zake moja wapo anasema zinaharibu uwezo wa kufikiri, na kumharibu mtoto kisaikolojia katika ukuaji wake.
Zaidi huyu jirani amewapa base kwenye kusoma vitabu yaani watoto wake muda wao mwingi wanasoma vitabu ambavyo vipo nje ya uwezo wao mfano mtoto wake wa darasa la tatu humletea vitabu vya chemistry na bioloji yaani anamuandaa mtoto kwa miaka ijayo na sio ampe masomo ambayo anasomea darasani kwake hapana na zaidi atampa vitabu vya kiuchumi nk, na nikiri kwamba wale watoto wa jirani yangu ukikaa nao unaweza sema umekaa na mtu mwenye degree wa Cuba maana anavyokuchambulia mambo kujua ni wadogo utajiona mjinga mbele ya hutu tutoto.
Narudi kwenu wakuu ni sahihi mzazi kumpa katazo la kutoangalia tv aina yoyote hasa kwenye kizazi hiki cha taarifa, na maarifa.