Ni sahihi mke na mme au wapenzi kutaniana kwa kutukanana matusi?

Kuna baadhi ya wanandoa na wapenzi kutaniana kwa kutukanana matusi tena matusi mengine ni ya ajabu sana

Na wanawake wanapenda sana kutumia matusi kwa wenza wao Kama matani
Mifano ni mingi,mfano ikiwa mwanamke anataka kufahamu mumewe alipo atampigia simu au sms "Weee bwege uko wapi?
Wewe kenge njoo ule

Halafu wewe nyoko acha ubishi basi!
Wewe mwanaume wa michepuko Sasa hivi upo kwa nani coz sikuoni home "

Wanaume nao hukubali kujibizana kwa njia hiyo hiyo ya matusi mpaka ya nguoni
Je ni sahihi kutaniana kwa njia ya matusi?
Binafsi ni big nooooooo!!!!
Sio sahihi kabisa kwasababu mwisho wake unakuaga mbaya sana mmoja wao akizidisha kwa mfano kuna mwanamke aliwai kuachana na mumewe sasa kwenye kujibizana aliwai kumtukana mumewe ambaye ni mlinzi kwamba ww huna lolote bwege tu nenda kalale getin uko aisee io kauli ilimuuma sana uyo jamaa kwaio sishauri kabisa ayo maiya utani na matusi
 
Mithali 14:12 Iko njia ionekanayo kuwa sawa Kwa mtu bali mwisho wake huelekeza mautini.

Mithali 3:5_6 Mtumaini Bwana Kwa moyo wako wote Wala usitegemee ufahamu wako mwenyewe;Katika Kila njia zako mtambue,naye atazielekeza njia zako.

Nipende kusema watu wanaofanya mambo kama hayo wanafungua mlango Kwa Shetani kwenye ndoa Yao.Na wote mnajua kazi ya Shetani “Kuiba kuua na kuharibu” (Yohana 10:10)
 
Back
Top Bottom