Ni sahihi Mh. Rais kuzungumza lugha ya kabila lake katika mkutano wa hadhara?

Hata akizungumza au aache aina matokeo hasi kwa taifa letu. Hata wewe ukiumia sana andika kwa kutumia lugha yako katika hii slide yako
 
Yupo sahihi kwani katika msimbo wa Isimu Jamii niliyojifunza katika chuo cha Kikatoriki Mwenge ni halali kabisa lengo ni kutaka kuwateka anaowahutubia.
 
Hakuna tatizo lolote kuongea kisukuma kwa sababu huende mkutano huo walengwa walikuwa Wasukuma na akaona kuna haja ya kukazia kwa Kisukuma.
 
Huo uzi hauna mashiko, ingekua labda uteuzi wa wasaidizi wake asilimia zaidi ya hamsini ni wa kabila lake, hapo tungeanza kufikiria hivyo
Tatizo kwa wazaliwa wa intermarriage. Hawajui wapi wapi
 
Kikwere ni kama kiswahili? Sijawahi kusikia Kikwete akiongea hicho Kikwere kwenye media au mkutano wa hadhara lakini huyu ndugu yangu duuu. Aseee! washauri wake wafanye kazi. Anafufua ukabila taratibu mpaka miaka 5 inaisha basi wasukuma wataonekana watu wa ovyo kabisa na hawafai kupewa uongozi wowote maana official language hawazitaki wanataka lugha yao tu. Jamani urais ni taasisi kubwa muno...!!
 
Nimeona leo kule shinyanga, anachomekea kuzungumza kwa kisukuma.

je haiwezi kuwa ni kuonesha kuwa "mimi ni wenu?" kuna ulazima gani wa kuzungumza kisukuma ktk mkutano unaotazamwa na watanzania wa makabila 120 nchi nzima?

nawasilisha!
Kweni aliekwambia yeye ni msukuma nani?
The way amekua akitumia lugha nyingi kulingana na mahala alipo,hyo ni sifa ya mtumishi mkongwe aliepita maeneo mengi ndani ya nchi yake.
 
Unajua yule bwana huwa anafikiria kwa hiyo lugha halafu anatafsiri ndipo aongee.sasa sometimes muda hautoshi.anaongea hivyo hivyo. Sasa shughuli ni pale anapotakiwa kuongea lugha ya tatu!fikiri huo mlolongo!
 


Kweli wapinzani wa JPM mmeishiwa hoja.Akizungumza kisukuma tunahoji ila tunalamika hajui kiingereza wala hatumii kiingereza?Kwenu Kiingereza ni muhimu kuliko Kiingereza.Fuatilia hotuba za Rais wetu marehemu (mtaalam wa lugha) JK Nyerere,aliweza kuchanganya lugha tatu hadi nne kwa wakati mmoja Kiswahili,Kiingereza,Kizanaki hadi Kihaya.
 
Nimeona leo kule Shinyanga, anachomekea kuzungumza kwa kisukuma.

Je, haiwezi kuwa ni kuonesha kuwa "mimi ni wenu?" kuna ulazima gani wa kuzungumza kisukuma ktk mkutano unaotazamwa na watanzania wa makabila 120 nchi nzima?

Nawasilisha!
Tafuteni Vitu vizuri vya kumkosoa sio kila kitu tu. Lwakatare huko bukoba alisema maneno kibao mbona sikuona utumbo kama huu... Mnachosha sana aro
 
Teh..teheeeeeh..mh anadumisha mila ndg zanguni.
Au amefanya vibaya ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom