Ni rekodi gani iliyompandisha chati Kikwete kiasi kile mwaka 2005?

1. Baby face
2. Alisema atavunja mikataba ya madini na kuipitia upya.
3. Alisema ata deal na rushwa nene nene.
4. Reli mpya ya kati
5. Jina lake Jk lilidhaniwa angefanana kiutendaji na Jk wa butiama
6. Chama kikuu cha upinzani enzi hizo (CUF) kilikuwa kimepoteza dira
7. Alitudanganya eti ni kijana.
8. Alionekana mtu wa watu (simple) mengne mtaongezea.

...sisi alitudanganya kuwa atatujengea barabara yetu, iwe ya lami ndani ya siku 100' tukimchagua! lakini mpaka sasa amebakiza miezi michache kuondoka ikulu' bado barabara hiyo iko vilevile! "najutia kura yangu kumpigia JK"
 
MKuu umesahahu huyu ndiye aliyeileta IPTL, kuilea na kuipa Mkataba.
pia umesahau huyu ndiiye aliyeuza VIBALI/LESENI zote za MADINI kanda ya ZIWa kwa yule mzungu amabaye na yeye akawuzia wakanada ?
 
Alikuwa na mvuto kwa wananchi,mvuto ambao haujulikani aliko upata,kama alikwenda kuchukua kwa waganga wa kienyeji ana jijua mwenyewe,mvuto ambao upo hata kwa rafiki yake ambaye hawakukutana naye barabarani labda walikutana kwa muganga hukohuko wakati wanachukua mvuto na hata ikitokea rafiki yake akawa rais hakuna cha zaidi atakachokifanya zaidi ya kile kinachofanywa na rafiki yake.
Mkuu Tukundane mimi ni miongoni mwa vijana wakati ule niliyekuwa na mshabikia sana kwa matumaini kuwa angeleta mageuzi makubwa ya kiuchumi baada ya Mkapa kuzidiwa nguvu na mabeberu na kuuza mashirika hata ambayo yalikuwa ni nembo za taifa kama ATC na TRC, lakini kilichotokea hadi sasa nimeduwaa na sina imani tena na yeyote ndani ya kampuni hii, namuomba radhi sana rafiki yangu bwana Jacob Ndekele popote alipo, kuwa sikumwelewa mwaka 2005 alivyoniambia chaguo lile halikuwa sahihi kwa maendeleo na uchumi wa nchi na kweli, wote tunaona mambo yanavyokwenda. MWAKA WA UKOMBOZI NI HUU 2015.
 
1. Baby face
2. Alisema atavunja mikataba ya madini na kuipitia upya.
3. Alisema ata deal na rushwa nene nene.
4. Reli mpya ya kati
5. Jina lake Jk lilidhaniwa angefanana kiutendaji na Jk wa butiama
6. Chama kikuu cha upinzani enzi hizo (CUF) kilikuwa kimepoteza dira
7. Alitudanganya eti ni kijana.
8. Alionekana mtu wa watu (simple) mengne mtaongezea.
Hizi zote ni hisia tu! eleza vitu alivyofanya kabla akiwa katika nafasi nyingine serikalini. Acha kuongelea hadithi alizotoa wakati wa kampeni ambazo ni za sayari ya nne. Eleza kwa uwazi alifanya nini na sio alisema nini!
 
wewe umefanya nini kwa familia yako

Hata kama wewe ni nyumba ndogo yake nijibu tu dadaangu. Kujua alichofanya sio kwa nia mbaya. Kama kuna zuri alilofanya sema tu. Mie sijapewa dhamana ya kusimamia mali za umma hata familia yangu ife njaa.
 
Hizi zote ni hisia tu! eleza vitu alivyofanya kabla akiwa katika nafasi nyingine serikalini. Acha kuongelea hadithi alizotoa wakati wa kampeni ambazo ni za sayari ya nne. Eleza kwa uwazi alifanya nini na sio alisema nini!

Kiongozi asante sana kwa kunielewa. Kuna watu wanajazba balaa.
 
Wadau nisaidieni. Katika harakati hizi za kupata kiongozi mpya kuna maneno mengi na analysis nyingi zinaendelea. Ili niweze kupima chanzo cha mtu kukubalika ningeomba nisaidiwe kujua ni Jambo au mambo gani ya maana aliyokuwa kafanya

J Kikwete kabla ya kuwa rais hadi tukachanganyikiwa kiasi kile 2005 na kumfanya awe Rais kwa kishindo. Jambo hili pia nitataka kujua kilichofanywa na Mh. Pinda hadi sasa. Hii itatusaidia baadhi yetu kujenga hoja zenye mashiko katika ushawishi wa nani anatufaa.

Naomba tuweke siasa pembeni kidogo tuwe objective. Asanteni wadau.

Kimsingi tulifanya kosa kubwa sana kumchagua J.K kwa sababu akiwa katika nyadhifa za chini hakuwahi fanya lolote la msingi ambalo lingempa credit ya kuwa rais wa nchi. Tukubali tulifanya kosa hivyo yatupasa tubadilike tusirudie kosa eti kwa sababu J.K alichaguliwa basi hata sasa akitokea mwingine kama Pinda, makamba, Mwigulu ambao kati ya hawa wameshindwa kabisa kumudu nafasi zao eti tuwachague tu mbona JK nae alichaguliwa kama wao. Tujiulize JK amefanikiwa???

Binafsi mwaka 2005 wakati J.K anafanya kampeni alikuja Mkoani Moro, wakati ule nilikuwa nafundisha katika shule 1 ya sekondari ya binafsi; tulikuwa walimu 23 na wanafunzi 600. Wakati anapita hapo shuleni kwetu wote walikwenda kumsubiri barabarani kumlaki isipokuwa mimi, hata alipofika msafara wake ulisimama na aliongea kwa dakika tano hivi kisha wanafunzi wakaanza kusukuma gari lake. Kati ya walimu wote na wanafunzi hata waliokuwa wagonjwa walikwenda kumwona lakini mimi nilibaki ofisini peke yangu kwa kuwa sikuona, sikusikia, sikuhisi kama kuna jambo lolote la maana alilokuwa amewafanyi watanzania kwa muda wake wote aliokaa serikalini akishikiria nafasi mbalimbali. Nilihisi hata kusikiliza hotuba zake ni ku-toxicate brain yake. Sikuhisi hata kama katika ubaya kuna kujifunza, nilihisi ubaya ni ubaya tu! Mpaka leo Uamuzi huo naufurahia kwani sioni cha maana alichofanya kwa miaka yote hii 10. Sumu haijaribiwi kwa kulabwa. "Chondichondi watanzania wezangu tusirudie kosa" .
 
1. Baby face
2. Alisema atavunja mikataba ya madini na kuipitia upya.
3. Alisema ata deal na rushwa nene nene.
4. Reli mpya ya kati
5. Jina lake Jk lilidhaniwa angefanana kiutendaji na Jk wa butiama
6. Chama kikuu cha upinzani enzi hizo (CUF) kilikuwa kimepoteza dira
7. Alitudanganya eti ni kijana.
8. Alionekana mtu wa watu (simple) mengne mtaongezea.
Mambo matatu: 1) kama walivyosema wengine, sura iliuzwa kwa wanawake na wote walimpa kura. 2) wanamichezo, hasa wanaocheza na wanapenda mpira wa miguu na mashabiki wao wote. Waliona huyu ni mwenzao sana. 3) alikuwa na EPA money alizokuwa amewaibia walipa kodi maskini wa TZ. alitubia hela zetu na akatuomba kura, tukampa. haya yanatokea TZ tu, kwenye nchi ya watu wa ajabu
 
kagoda agriculter co.ilikwapua mabilioni toka BOT,zikatumiwa kutuhonga t-shirt,kanga,nk.tukamchagua
 
Back
Top Bottom