Ni nini hasa kilichokuwa kinakukera kwenye Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Mimi kilichokuwa kinanikera ni kumuona Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Lewis Makame alivyokuwa akitangaza matokeo ya kura za Urais Jakaya Kikwete anaendelea kuongoza....Endeleza na wewe yaliyokukera
 
kutokuwepo kwa kura ya kutokubaliana na mgombea yeyote kati ya wanaogombea, ili kura zikiwa nyingi za kukataa! vyama vijipange upya vituletee mgombea anayeuzika
 
Mimi kilikuwa nachukia sana kumuona mrema akifanya kampeni manzese ndio ulikuwa uwanja wake wa nyumbani
 
Mi kilichonikera ni wasanii wa bongo fleva kuwa upande wa ccm huku wakikisifia kuwa n chama cha bora.
 
mimi kilichokuwa kinanikera na polisi walivyokuwa wanasitisha mikutano ya vyama vya upinzani hata kabla ya muda halali kutimia na kuwaruhusu wagombea wa chama cha ccm hata kama muda umeshatimia
 
Nilichukia kampeni ya chuki dhidi ya Kikwete kwa kutumia udini iliyoendeshwa tar 24 oct kwenye Kanisa Kuu la Njombe.
 
Nilichukia kupoteza kura yangu kutokana na wizi wa kura yangu uliofanyika jimbo la segerea.
 
me nilichukia kuona majina ya watu yanakosekana kwenye vituo sahihi walivyojiandikishia, hali iliyopelekea wengine kukata tamaa ya kufuatilia hivyo kukosa haki yao ya msingi
 
Kitendo cha Batilda kukataa kushindwa hadi kumuita Lowasa ili wampe chapa Mh. Lema, hicho kitendo kilinikera sana
 
mi kilichonikera ni baa niliyozoea kupata supu na bia asubuhi ilifungwa eti kisa meneja na wahudumu wapo kwenye foleni za kupiga kura.
 
Mi nilikerwa na mtindo mzima wa upigaji kura, nafuu ingekuwa ya kwamba mtu anatangazwa kwanza kuwa mshindi halafu ndio upigaji kura unafuata baadae.
 
Back
Top Bottom