Ni nini chanzo cha mapato cha wana CCM kwani kila nikikutana nao ni kuomba fedha kila wakati!

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,829
21,461
Kuna kitu kinanishangaza sana bora leo nikiseme wengine wakupatie majibu.

Kila nikikutana na viongozi na wanachama wa CCM hawasiti kuomba omba fedha na hawajishughulishi kutafuta fedha au kufanya kazi.

Ni nini vyanzo vya mapato vya watu hao!!

Je familia zao wanazihudumia vipi?
 
Moja wapo wa kigezo yawezekana kisiwe rasmi, ili huwe kiongozi lazima uwe na kipato rasmi. Kwa hiyo, nadhani hao uliokutana nao yawezekana wamekutapeli. Sidhani kama Kuna kiongozi wa CCM Nafanya hayo uyasemayo.
 
Katibu wa ccm tawi analipwa Tsh 5,000 Kwa mwezi!!
Una Habari hiyo mkuu!
 
Kuna kitu kinanishangaza sana bora leo nikiseme wengine wakupatie majibu.

Kila nikikutana na viongozi na wanachama wa CCM hawasiti kuomba omba fedha na hawajishughulishi kutafuta fedha au kufanya kazi.

Ni nini vyanzo vya mapato vya watu hao!!

Je familia zao wanazihudumia vipi?
Hiki Chama wanachama wake wameshagundua Viongozi wao wako pale kimaslahi. CCM wametengeneza mfumo wa kipuuzi Kweli kweli.

Muda wote wanachama wanawaza kupewa vya bure tu. Nikiwa mjini Sumbawanga wiki mbili zilizopita nimekutana na ugomvi wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wao Dan Chongolo.

Wanachama waliosombwa kutoka wilaya za mbali kama Nkasi, Kalambo na Sumbawanga vijijini (Laela) waliahidiwa 5000 Kila mmoja lakini wajanja wakazizima na kuwapa baadhi 3000 na wengine wakapitishwa kushoto.

Moto uliowaka si wa kitoto maana nilishuhudia pale nje ya uwanja wa Mandela watu waliovaa mashati ya kijani wanakunjana.

Utaratibu wa Wabunge au wagombea kulazimishwa na Chama kuwahonga (wao wanaita kuwagharimia) wanachama ndipo wafanye kazi Fulani ya Chama umekizika kabisa Chama hiki na Kwa Sasa kama hutoi hela husikilizwi na mwanaCCM yeyote.
 
Kuna kitu kinanishangaza sana bora leo nikiseme wengine wakupatie majibu.

Kila nikikutana na viongozi na wanachama wa CCM hawasiti kuomba omba fedha na hawajishughulishi kutafuta fedha au kufanya kazi.

Ni nini vyanzo vya mapato vya watu hao!!

Je familia zao wanazihudumia vipi?
Kushikilia madaraka ya nchi ndo chanzo cha mapato ya CCM.

Unapoona ripoti ya CAG haishughulikiwi maana yake ni kuwa CCM imechota hela na hakuna wa kuwahoji....

Tuendelee kula wali mtori upo njiani
 
Back
Top Bottom