Nawashauri wahitimu wa vyuo na wasiopatiwa ajira kuishitaki serikali ili iwalipe fidia kwa kupoteza muda wao

mr pipa

JF-Expert Member
Jul 26, 2021
2,331
4,857
Kiufupi Serikali inapaswa iwajibishwe, na ishitakiwe kwa uzembe unaofanya huwezi kupoteza muda wa mtu kwa kisingizio cha elimu na ikiwa elimu yenyewe haina msaada kwa muhusika.

Kwa nini haina msaada kwasababu wanafunzi au wahitimu "wanalisomea taifa badala ya kusomea maisha yao" sasa kama wanalisomea taifa na elimu yetu imewatengeneza ili waje waajiriwe, basi kuna umuhimu kwa wale waliokosa ajira walipwe fidia ili waendeshe maisha yao kwa kupoteze muda wao.

Na ili hili lifanyike, inapaswa wale mliotoka vyuo na hamjaajiriwa yawapasa mkastaki mahakamani, ili sasa Serikali ione usumbufu mwisho itoe elimu ambayo inamuwezesha muhitimu, kupambana na maisha hata akitoka chuo, tofauti na sasa tuna wasomi wenye degree ambapo hata hizo degree hazina sehemu ya kuzipeleka zaidi ya huko walikofundishwa.
 
Ni bora ukoloni wa kisiasa kuliko kutawaliwa ufahamu ,wazungu wanafurahi sana kutufanya wajinga kwa kiwango hiki Ujinga ambao hata kuandika vya maana hakupo tena.
 
Ajabu Sana wanatoa vyeti na kumuita mtu muhitim na hajui lolote kuhusu huo uhitimu.
Anapewaje cheti ?
 
Back
Top Bottom