Ni muda muafaka sasa serikali ikatoa hela na kugharamia upimaji na urasimishaji wa ardhi nchi nzima

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,105
3,619
Napendekeza, ni muda muafaka sasa serikali ikatoa hela na kugharamia upimaji na urasimishaji wa ardhi nchi nzima, ili wananchi wajenge kwa mpangilio, na ambao wamejenga ndiyo iwe mwisho wao kujenga holela.

Kama serikali imeweza kugharamia anuani ya makazi, iweje ishindwe kugharamia urasimishaji na upimaji wa ardhi?

Kipi kilipaswa kutangulia, anuani za makazi au upimaji na urasimishaji wa ardhi? Kuna maeneo vijijini wameweka anuani kwenye nyumba, ambapo katikati kuna kiwanja shamba hakijawekewa namba, hivyo huyu mtu akija kujenga kwenye shamba lake atajikuta namba ya mwisho ipo katikati, mfano mtaa wenye nyumba kumi utakuwa hivi: 1, 2, 3,4, 10, 5, 6 7, 8, 9. Anuani zingeenda kwa mtiririko mzuri endapo zoezi la kupima na kurasimisha ardhi ndilo lingeanza, ila hatujachelewa.

Hapo mwanzo, wizara ilipanga kutumia zaidi ya bilioni 600 kwa ajili ya anuani za makazi. Hapa walikuwa wanatumika wataalamu wa wizara, ila baadae wakaamua kulishusha zoezi ngazi ya halmashauri na kutumia bilioni 27.

Sasa, kama serikali ilikuwa tayari kutoa bilioni 600 kwa ajili ya anuani za makazi, sasa kwa nini ishindwe kutoa hizo bilioni 600 kwa ajili ya kurasimisha na kupima ardhi nchi nzima angalau kwa kuanzia mijini?

FAIDA ZA SERIKALI KUPIMA ARDHI YENYEWE;
1. Miji itajengwa kwa mpangilio, hivyo kupunguza ujenzi holela.

2. Kuzuia kuendelea kujenga holela mana watakaorasimishiwa watakuwa ndio wa mwisho kujenga holela.

2. Kuzalisha ajira za muda kwa vijana ambao ni wataalamu wa ardhi na wasiowataalam. Njia mojawapo ya kuleta mzunguko wa hela ni kuanzisha projects zenye tija kama hizi.

TAHADHARI;
Kuendelea kuacha kupima na kurasimisha ardhi, ni kuruhusu ujenzi holela kuendelea nchini. Watu wanahela za kujenga ila halmashuri hazina viwanja, na kama vipo basi unakuta ni porini, hakuna huduma muhimu ambazo ni maji, umeme, barabara nk.

Sheria ya ardhi ya mwaka 1999 inasema ardhi yote ya kijiji msimamizi wake ni mwenyekiti wa kijiji

Watu wanatumia fursa hii kujenga holela kwenye vijiji ambayo vipo ndani ya manispaa, na kamwe hawawezi kubomolewa wala kuulizwa kibali cha ujenzi, kwani ardhi haijapimwa na vijijini mnajipanga wenyewe tu chini ya mwenyekiti wa kijiji na kamati yake ya ardhi.

Wizara na Wakurugenzi wa Halmashauri wanalijua hili, ila wapo kimyaa kwa baadhi ya halmashauri.

Kwa mfano, fuatilia kama ulishawahi kuona jengo limeandikwa "leta kibali" kwenye jengo lolote lililopo kwenye kijiji ambacho kipo ndani ya manispaa. Siyo kwamba, watu wa ardhi hawayaoni hayo majengo, bali sheria ya ardhi ya kijiji inawabana.

Kuna vijiji ambavyo vipo ndani ya manispaa, unakuta mwenyekiti wa kijiji yupo sirias, ndiyo unakuta wamejenga kwa kujipanga, ila hali ni mbaya kwa vijiji ambavyo viongozi wao ni corrupt.
 
Unataka waangalie wanakupigaje tena maana serikali yako itaangalia ukifinyaje ili ufanye malipo indirectly ukizani inalipa serikali kumbe wewe mwenye

Sizungumzii tozo
 
SERIKALI KWA MIKONO yake alikwisha HARIBU MIJI YETU hebu Fikiria Jiji la DAR JINSI LILIVYOHARIBIKA wakati ni Makao makuu ya Nchi? Serikali ipo Wizara zote zipo ni VIGUMU kurekebusha Miji yetu Wacha iendelee kuwa Kama manzese

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom