Ni mila na desturi zetu vijana kuongoza wazee??

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Nina muda mrefu sana sijasikia kauli kwamba "VIJANA NI TAIFA LA KESHO" badala yake nasikia "HUU NI WAKATI WA VIJANA" n.k, Ninaamini kwamba Msimamo kwamba Vijana ni Taifa la Kesho linabeba ujumbe kwamba, Ujana sio Umri wa Kuongoza au kutawala, bali ni umri wa kujifunza namna bora ya kuongoza kwa mujibu wa mira, desturi na Majukumu ya Uongozi katika Jamii husika.

Historia ya Taifa letu inaonyesha kwamba, Mira na Desturi za Uongozi katika Jamii yetu haziwapi nafasi vijana kuwa viongozi, au wasemaji katika Jamii husika katika mambo mbalimbali ya mchakato wa maisha,kwa mfano, Mabarozi wa nyumba kumi walikuwa ni watu wazima, washenga na wasimamizi wengine wa michakato ya ndoa, wasuluhishi wa migogoro mbali mbali katika Jamii,na viongozi wa mabaraza tofauti tofauti ya Kijamii, wote walikuwa ni watu wenye umri wa mkubwa.

Hali imekuwa ni tofauti katika siku za hivi karibuni, na ninachokiona mimi ni kwamba, Vijana wameamua kwa makusudi ama kwa kujua ama bila kujua kutumia wingi wao katika kuchagua vijana katika chaguzi zote ambazo wanashiriki, sielewi hii inatokana na wao kuamini kwamba wanaweza wakazipatia Jamii zetu uongozi bora zaidi ya ule tuliozoea kutoka kwa wazee au la.

Zaidi ni kwamba, Vyama vya Siasa navyo vimeingia katika mkumbo huu, hawa wanaonekana kujua wanachokifanya, kutumia nguvu ya wingi wa vijana katika kujipatia madaraka ya kisiasa katika chaguzi za kupiga kura, Nikitolea Mfano wa Uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki hivi karibuni, Magazeti kadhaa yaliandika Wazee wa Arumeru wakilalamika kwamba wanadharirishwa na vijana pamoja na watoto kwa kuzomewa kila wanapopita, na kuna mengine yalimkariri Mwenyekiti wa Chama cha Democrasia na Maendeleo Mheshimiwa Mbowe akiwasihi vijana kutowazomea wazee waliovaa nguo za Kijani.

Hivi kweli kabisa, Inaingia Akilini kwamba Katika Kikao cha Familia Kijana ndio au msimamizi kwa maana ya kuamua nani aanze kuongea ama nani asiongee na mwishoni awind up kikao huku wazee wazima wakiwapo wanamsikiliza, Kwa nini tunaruhusu hili katika Siasa, Au Ndio maana watu wanasema siasa ni mchezo mchafu!!!
 
Nachukia sana watu wanaoharibu lugha...ati "mila" mtu anaandika "mira" bull shit!
 
Nachukia sana watu wanaoharibu lugha...ati "mila" mtu anaandika "mira" bull shit!

Hata kama alikuwa na mazuri ya kuandika huwa hamu ya kuyasoma inaniiishia kabisa. Wanaudhi kweli halafu wanajidai wanakipenda na kukienzi Kiswahili.
 
Hata kama alikuwa na mazuri ya kuandika huwa hamu ya kuyasoma inaniiishia kabisa. Wanaudhi kweli halafu wanajidai wanakipenda na kukienzi Kiswahili.

Aliyekuambia anakipenda na kukienzi kiswahili ni nani? Mimi Kiswahili ni lugha ya tatu, Ya kwanza ya Baba yangu, Ya pili ya mama yangu, alafu ufasihi katika kiswahili sio unaoniweka mjini, Mnajifanya kukipenda kiswahili huku mnajipa majina ya kidhungu. Kwanza wewe sitegemei ujadili hoja hii, sababu vijana wanakisumiza shimoni chama chako.
 
Kamsimulie mkeo basi kama hutaji kusahihishwa, hatutachangia mpaka ukubali makosa
 
Kamsimulie mkeo basi kama hutaji kusahihishwa, hatutachangia mpaka ukubali makosa
Kwa hiyo na wewe umeingia mkenge wa kujadili lugha badala ya hoja? Sina namna ya kukusaidia, acha kuchangia.
 
tofautisha uongozi wa ukoo/kabila na uongozi wa nchi........

Kwanza hao wazee wameongoza nini? Labda kwenye kutafuna nchi....

Ndo maana tz hatuendelei
 
tofautisha uongozi wa ukoo/kabila na uongozi wa nchi........

Kwanza hao wazee wameongoza nini? Labda kwenye kutafuna nchi....

Ndo maana tz hatuendelei

Mbona nchi za wenzetu hawazungumzii haya mambo? au wazee wetu pekee ndio hawafai?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom