Ni mambo gani ya kuzingatia wakati wa kuchagua mwenza na uchumba unapaswa kudumu kwa muda gani kabla ya kufunga ndoa?

clearmind

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
424
724
Ukisoma threads nyingi hapa jukwaani zinahusu mahusiano ya wanandoa, utagundua kwamba wengi waliingia bila kujua ni nini hasa walipaswa kufanya kabla ya kufikia maamzi mazito ya kuoana.

Niwaombe mliopo kwenye ndoa mtusaidie mambo kadhaa tunayotakiwa kujua hasa wakati wa uchumba na je, uchumba unapaswa kudumu kwa muda gani kabla ya kufunga ndoa?
 
Hakuna formula ila kama mwanaume upo katika late 20's to 30's na hauna mpenzi unatafuta mke, kua makini na wadada ambao upo nao rika moja 26+ hawakupi room ya kuwajua vyema wanachotaka ni ndoa na wanakupressurize sana hiyo process. Hawashindwi hata kuigiza tabia njema au kunasa mimba kwa kusudi ili mradi tu apate hiyo ndoa. Ni Mungu tu atusaidie katika hiyo group
 
Nakupa hii mwanamke ambaye kasadate na jamaa wengi sana hafai kuoa ,kuwa makini kweny uchumba maigizo ni mengi sana.
 
Ukitaka kujua tabia ya mtu chunguza wazazi wake, maisha ya ndoa ya mtu ni photocopy ya wazazi walivyoishi. Ukitaka kujua tabia ya binti mchunguze mama yake. Uchumbani KILA mtu huwa malaika, chunga Sana ogopa Sana wajifanyao watu wa ibada Sana au binti anazuga hakuombi hela au unampa anakataa.
 
Kama unatafuta mke ..kipindi cha uchumba jitahidi sana ku mchumbia mama yake kwanza... Kama mama yake alikua mkorofi kwa mume wake na alikua anapenda maisha ya usawa au kumkalia mwanaume, na kama alikua single mama, au mama yake alikua mjeuri sana asie na adabu wala utii kwa mume..huyo mwanamke hafai kuolewa cz mwanamke anarithi tabia kwa mama yani anacopy...

KAMA MWANAMKE ANAMCHUKIA SANA BABA YAKE MZAZI , HANA HESHIMA KWA BABA YAKE HATA KWAKO ITAKUA HIVYO HIVYO. HUYO MKWEPE SANA HAFAI KUA MKE cz heshima mwanamke anayo mpa baba yake na wewe hivyo hivyo kama mume utaipata

Kama unatafuta mume kipindi cha uchumba, Chumbia kwanza baba yake ndio utapata tabia za mumeo cz nae ni hivyo hivyo anacopy
KAMA MWANAUME ANACHUKI NA MAMA YAKE MZAZI JUA WAZI KABISA NA KWAKO ITAKUA HIVYO HIVYO ,HUYO HAFAI KABISA

Nb: kama unaweza oa muundo mzima wa familia yao yani isome sana background ya familia ya huko unako taka kuoa / kuolewa utapata tabia ya unae taka kumuoa/ olewa nae..

Bila kusahau angalia na aina ya marafiki alio nao huyo mchumba wako utapata kujua tabia yake..


ukikamilisha haya yote kwa muda usiopungua miezi sita na ukajiridhisha basi Mungu awatangukie

NAKAZIA MWANAUME KAMA UNAJUA KABISA HAUNA AKILI SIKUSHAURI KUOA
 
Ijue historia ya mke wako mtarajiwa ipasavyo. Ijue historia juu ya familia yake, katika nyanja za kiuchumi, utamaduni, elimu, mapenzi, mahusiano ma watu wengine n.k.

Baada ya kuoa si muda wa kutafuta historia tena.
 
Sidhani kama kuna formula... Walokaa miaka kumi uchumba wanaachana mwaka mmoja baada ya ndoa,walokaa miezi 6 uchumba huachana vile vile...... Kikubwa kaa na mtu wako angalia vya muhimu unavyo taka kujua .....ukiona poa nendeni mkaishi na Mungu awatangulie.

comment ya kibabe sana hii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom