- Thread starter
- #21
Mimi Muislam na nimeoa ndoa ya kiislamu kutapo tokea Muungu aipushe mbali mgogoro kati yetu
Ni lazima tuyamalize lishera kama uislam unavo sema sasa jee
Sheria ya ndia ya 1971 inatambua ndoa za kiislam kuhukumiwa kwa taratibu hizo ? Jawabu hapana upo ushahidi wa kesi nyingi kuamuliwa kufata mazingira ya ushahi na kuamuliwa kinyume chake
Sasa jee ni lazima kuwe na mahakama ya kadhi ? Mawazo yangu sio lazima ila tunaweza kubadilisha sheria ya ndoa na kuweka kipemgele cha kutambua ndoa za kiislam na kuweka sheria ya kuwa ndoa hizo zitahukumiwa na taratibu za kiislam
Na sheria hizo ndo ziwe juu ya sheria nyengine
Ni kama vile Customary law zinavotambuliwa kwa baadhi ya makabila
Hivo tunaweza kubadilisha tu sheria ya ndoa kukidhi haja hii ya waislam bla ya kuingiza gharama nyengine
Ama kuhusu kujiunga na OIC sio lazima hasa kwa Tanzania kuna upinzani kutoka upande wa pili
Hoja yao ni kuwa huu ni umoja nchi za kiislam na tanganyika sio nchi ya kiislam so sio lazima
Lakini hili linaweza likubaliwe katika katiba mpya kwamba ushirikiano wa nje usiwe ni jambo la muungano hivo Zanzibar ni nchi ya kiisllam
Kwa wingi wao wanaweza kujiunga
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
kwanza tuwekane sawa hapa...sheria za ndoa ziko wazi kabisa zinatambua ndoa za kiislamu,..pia hata inapofikia talaka kwenda mahakani ni tayari BAKWATA wameshafanya maamuzi ambayo yanatambulika kisheria hivyo mahakama inakamilisha tu mchakato,ukija ishu ya mirathi iko wazi pia kwamba mahakama lazima ifuate sheria za kiislamu kuhusu mgawo ambao upo kwenye Quaran takatifu,kwa maana hiyo hadi sasa hakuna mapungufu yanayofanya mwislamu akose haki zake