Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
- Thread starter
- #21
Embu tuangalie sera yao ya elimu kwa mfano. Kwa miaka ishirini iiliyopita wamekuja na kila mpango wa kuinua elimu na kuboresha sekta ya elimu. Wakiongozwa na MKUKUTA na mipango meingine ya MMEM n.k tulitarajia kuwa elimu yetu ingekuwa bora zaidi. Je, tunaweza kusema kuwa mipango yetu mingi ya kuinua elimu ambayo imekunywa fedha nyingi sana za umma imefanikiwa kuboresha elimu ya TAnzania hasa ukizingatia mfano wa juzi tu ambapo nusu ya wanafunzi waliofanya mtihani wa sekondari nchini wamefeli?