Ni Kweli Sera za CCM zimekuwa ni janga kuu la taifa? Tunavuna tunachopanda...?

Matatizo ya Tanzania ni zaidi ya sera. Ki ukweli sera zooooote ni nzuri, tatizo liko kweye utekelezaji. Na utekelezaji unaanzia kweye mfumo wenyewe wauendeshaji nchi. Chama kama CCM kinapotata ushindi kinaunda serikali ambayo inatarajiwa kutekeleza hizo hizo sera. bahati mbaya sana chama kama chama haki fanyi ufuatiliaji wa utekeleza wa hizo zera. CCM kwa mfano hawana kitengo cha ufuatiliaji na tathmini (Monitoring and eveluation) ambacho kinaweza kika kikafanya upembuzi wa kisayansi kuona kama sera zake zinatekelezwa. Hii inatokana na sababu mbili, kwanza Mwenyekiti wa CCM ndo huyo huyo mkuu wa Serikali. Hivyo sioni namna ambayo mwenyekiti wa CCM anaweza kuruhusu hilo lifanyika maana atakua ana jivua nguo mwenyewe.

Pili watanzania kwa ujumla ni watu wa chukua chako mapema, Watanzania wengi wa sasa kwa nafasi walizonazo kila mtu anajali masilahi binafsi. wenyewe wanasema bora mkono unaenda kinywani. Wakishapata nafasi hawataki kujisumbua akili wa kusumbuka kwa namna yoyote ile. watendaji wengi wa serikali hawako kwa masilahi ya taifa bari kwa masilahi yao wenyewe. na wala siyo kweli kwamba wako chadema na wanaihujumu serikali. Hawapendi kabisa chadema kwa sababu wananufaika na mfumo uliopo. Hawaulizwi na wala hawawajibishwi, wanakula nchi kwa kwenda mbele.

Tatizo lingine la serikali/chama tawala ni kutekeleza mipango mingi isiyotekelezeka. Mara Mkukuta, mara milleniun goals, mara ilani ya uchaguzi, maagizo ya raisi n.k. Kwa kuwa na mipango mingi ni vigumu kupima ufanisi wa utekelezaji. Kunatakiwa kuwe na mpango mmoja tu, na hakuna haja ya kuwa na mipango mingi.

CCM haina vichwa, CCM haina watu wanaoweza kuandika sera na kufuatilia utekelezaji. After all wanajua kuwa watanzania hawachagui chama kwa sababu ya sera. Kama wangekua wanachagua sera basi Kikwete asingejaguliwa kwa maana katika kampeni zilizopita haku nadi sera bali alikuja na staili ya ahadi za papo kwa hapo.
 
Ccm na zinazoonekana sera nzuri zimetekwa na vikundi maslahi..na imekuwa ni kama kansa mbaya kulindana yaani m/kiti taifa hadi shina wanahangaika kuweka watu/mifumo itakayowalinda ndani ya chama...sasa imekuwa ni imani ya wanachama/taifa kuwa atainuka mtu na kuisafisha ccm mara!..lipo tumaini jingine(kufikirika?) kuwa wanaccm watakitwaa chama chao 2012... M/kijiji nikiri tu sera za ccm zimeshindwa.. "viatu vya Mlw. vimekuwa vikubwa mno"...
 
Jamani kama ramani ya nyumba imekosewa haijalishi mjenzi ana ujuzi gani na haijalishi kama mtu anaisifia kwa kiasi gani ukweli ni kuwa nyumba ikijengwa choo na jiko vitakuwa vimeingiliana na mlango wa chumba kikuu ukawa unatokea uwani! Sera ni ramani ya nini tunataka hivyo haziwezi kupuuziwa hata kidogo. Bila sera ni kuwa taifa linaenda bila ramani; sasa hata tuweke mabilioni ya shilingi - ndivyo tunavyofanya - ukweli ni kuwa ramani imeshakosewa!

Si kwamba hatutaweza kujenga ukuta tutaweza, siyo kwamba tutashindwa kuweka sehemu za madirisha tutaweza lakini kukamilisha nyumba haitakamilisha. Mnaweza mkaamua kubadili mjenzi na mshauri mjenzi lakini kama huyo mshauri hatataka kuangalia ramani ya nyumba atawalia fedha zenu tu!

Tunachokiona sasa siyo kushindwa kwa watu - kama baadhi ya watu wanataka tuamini - ni kushindwa kwa sera! Ni mara ngapi wamebadilisha watu lakini mambo yamekuwa ni yale yale? Wizara ya Afya imewahi kuwa na madaktari, wasomi wengine n.k lakini matokeo yake yamekuw ani yale yale. Wizar aya Elimu imewahi kushikwa na maprofesa lakini kiko wapi sasa?
 
Mkuu MMJ Tatizo la Tz Sio sera... Tatizo ni ujasiri wa kusema embe ni embe na Sio tunda lenye ikakasi.. Tatizo la Tz ni kutokusimamia mapato ya madini, rasilimali zingine Kama utalii, gas na hata vyanzo vingine...tumekadhania Kuwabana wananchi na kutembeza bakuli na kuacha rasilimali Zetu zikiibiwa.. Sasa tutatekeleza VIPi sera bila pesa?
 
Hapana mkuu! Tatizo si sera za ccm zinazofanya viongozi wake wafeli,tatizo ni wanaccm wenyewd na misingi aliyoacha Mwl Nyerere! Kama CCM hawana sera kwanini watanzania hawajafanya mabadiliko kupitia kura hadi leo ingawa mara kadhaa wamejitokeza watu makini kugombea kupitia vyama vingine? Mwl Nyerere aliachia madaraka kwa mtindo kama wa kuzira hivi(sipendi sana kusema hivi) pale alipoona maono yake hayato timia! Alipaswa kuendeleza mapambano ya fikra zake kwa kuacha mfumo bora(ikiwemo katiba nzuri).tulianza kuokoteza sera na miongozo ya kibepari kuanzia pale alipostaafu! CCM ikiwa ni moja ya majanga mazito kwa kuachiwa mustakbari wa taifa hili bila na kuwa mfumo mbadala ulio bora! Tunatokaje kuanzia hapa naogopa kusema nikaitwa mhaini!
M
 
sema tu, mhaini ilikuwa zama zile.
 
Sasa utawezaje kuwa na fedha kama hauna sera ya jinsi ya kupata pesa hizo na kuzitumia?
 
Hapana mkuu! Tatizo si sera za ccm zinazofanya viongozi wake wafeli,tatizo ni wanaccm wenyewd na misingi aliyoacha Mwl Nyerere! Kama CCM hawana sera kwanini watanzania hawajafanya mabadiliko kupitia kura hadi leo ingawa mara kadhaa wamejitokeza watu makini kugombea kupitia vyama vingine? Mwl Nyerere aliachia madaraka kwa mtindo kama wa kuzira hivi(sipendi sana kusema hivi) pale alipoona maono yake hayato timia! Alipaswa kuendeleza mapambano ya fikra zake kwa kuacha mfumo bora(ikiwemo katiba nzuri).tulianza kuokoteza sera na miongozo ya kibepari kuanzia pale alipostaafu! CCM ikiwa ni moja ya majanga mazito kwa kuachiwa mustakbari wa taifa hili bila na kuwa mfumo mbadala ulio bora! Tunatokaje kuanzia hapa naogopa kusema nikaitwa mhaini!
M

Huwezi kuwa na mfumo mzuri wa utawala kama sera ni mbovu; kwani mfumo wa utawala unakuwa preceded na sera nzuri zinazotekelezeka. Huwezi kujenga mfumo bila sera!

Mfumo wa wakati wa Ujamaa uliwezekana kwa sababu ulikuwa unaendana na sera za kijamaa!
 
Mkulo ananukuliwa hapa kuthibitisha my assertion kuwa sera za CCM zimefeli! Hata wao wenyewe wanajua kuwa zimefeli!

DailyNews Online Edition - Mining policies for immediate review
Amelalamikia "lack of expertise" so bado hawataki kukubali kuwa tatizo ni sera, rather wanadhani sera zinakwamishwa na utekelezaji, this time mkulo anadai tatizo ni wataalam.

Hadi sasa kwenye mjadala huu kuna wanaosema tatizo ni sera na wengine ni utekelezaji, kwenye utekelezaji, kuna migawanyiko, wengine wanasema ni viongozi, na sasa viongozi wanasema ni wataalam, so mpira bado wanatupiana tu, na as long as they can count something coming in, ie wanavyojiongezea posho nk, nothing will change.

Swali lako kwaujumla litachochea mjadala mrefu sana hapa, hopefully the positive one.

Let me wait and see, shida ni kwamba hawawezi kukubali kuwa sera ndo zimeshindwa, hence theory yangu kuwa wataendelea kulaumiana kisiasa na kubadlishana vijiti kuwa "somewhat valid."
 
Amelalamikia "lack of expertise" so bado hawataki kukubali kuwa tatizo ni sera, rather wanadhani sera zinakwamishwa na utekelezaji, this time mkulo anadai tatizo ni wataalam. Hadi sasa kwenye mjadala huu kuna wanaosema tatizo ni sera na wengine ni utekelezaji, kwenye utekelezaji, kuna migawanyiko, wengine wanasema ni viongozi, na sasa viongozi wanasema ni wataalam, so mpira bado wanatupiana tu, na as long as they can count something coming in, ie wanavyojiongezea posho nk, nothing will change. Swali lako kwaujumla litachochea mjadala mrefu sana hapa, hopefully the positive one. Let me wait and see, shida ni kwamba hawawezi kukubali kuwa sera ndo zimeshindwa, hence theory yangu kuwa wataendelea kulaumiana kisiasa na kubadlishana vijiti kuwa "somewhat valid."
...Tatizo sio wataalamu. Hawa tunao wa-export nchi za nje wanaenda fanya nini? kucheza ngoma?. Nakubaliana na wale wanaoona kuwa tatizo lipo kwenye uongozi, tena wa ngazi zote chini kabisa hadi juu. We need a practical, focused, determined and decisive leadership at all levels.
 
Huwezi kuwa na mfumo mzuri wa utawala kama sera ni mbovu; kwani mfumo wa utawala unakuwa preceded na sera nzuri zinazotekelezeka. Huwezi kujenga mfumo bila sera! Mfumo wa wakati wa Ujamaa uliwezekana kwa sababu ulikuwa unaendana na sera za kijamaa!
...Hapana! Mfumo mzuri ndio hutekeleza sera, not the other way around. By the way, you can go borrow lots of policies from friends and localize them, to suit your needs.
 
Jamani kama ramani ya nyumba imekosewa haijalishi mjenzi ana ujuzi gani.
...Mjenzi akiwa ni mjuzi wa fani yake atagundua na kudokeza dosari au kurekebisha kosa katika ramani. Hatokubali kuharibu kazi yake!
Wizara ya Elimu imewahi kushikwa na maprofesa lakini kiko wapi sasa?
...Tunao madereva waliofuzu vizuri kabisa chuo cha usafirishaji, lakini wanaendesha magari kihuni kabisa mjini, achilia mbali kuvunja sheria za barabarani.
 
...Sijakuuliza wewe. Nime-respond kwenye hoja ya Mkullo. Sawa sawa?
Siyo sawa swa, kama ulirespond kwenye hoja ya mkulo mbona ulinquote?
What is this?

quote_icon.png
By jmushi1
Amelalamikia "lack of expertise" so bado hawataki kukubali kuwa tatizo ni sera, rather wanadhani sera zinakwamishwa na utekelezaji, this time mkulo anadai tatizo ni wataalam. Hadi sasa kwenye mjadala huu kuna wanaosema tatizo ni sera na wengine ni utekelezaji, kwenye utekelezaji, kuna migawanyiko, wengine wanasema ni viongozi, na sasa viongozi wanasema ni wataalam, so mpira bado wanatupiana tu, na as long as they can count something coming in, ie wanavyojiongezea posho nk, nothing will change. Swali lako kwaujumla litachochea mjadala mrefu sana hapa, hopefully the positive one. Let me wait and see, shida ni kwamba hawawezi kukubali kuwa sera ndo zimeshindwa, hence theory yangu kuwa wataendelea kulaumiana kisiasa na kubadlishana vijiti kuwa "somewhat valid."

...Tatizo sio wataalamu. Hawa tunao wa-export nchi za nje wanaenda fanya nini? kucheza ngoma?. Nakubaliana na wale wanaoona kuwa tatizo lipo kwenye uongozi, tena wa ngazi zote chini kabisa hadi juu. We need a practical, focused, determined and decisive leadership at all levels.
 
...Hapana! Mfumo mzuri ndio hutekeleza sera, not the other way around. By the way, you can go borrow lots of policies from friends and localize them, to suit your needs.

Mfumo hautoki hewani; unatokana na sera ambayo nyuma yake kuna itikadi. Itikadi ya chama hutangulia sera za chama; kutokana na mabadiliko mbalimbali katika jamii sera huweza kubadilishwa badilishwa kufuatana na mahitaji. Sera zinatangulia sheria na uundwaji wa vyombo mbalimbali (mfumo). Ukishajua unataka kufanya nini kwenye kilimo na vipi unatoka kwenda kuanza kutengeneza miundombinu ya utekelezaji wa sera hizo. Ukiweka mkazo mkubwa kwenye miundo mbinu unaweza kujikuta unavyovitu vyote muhimu vya mfumo lakini havifanyi kazi kwa sababu havijakubaliana vinataka kufanya nini vipi na na kwanini.

Kwa mfano, ukisema sera yako ya elimu ni kutoa elimu ya bure kwa kila mtoto wa shule ya msingi na sekondari kinachofuatia ni kubadilisha sheria na kuunda vyombo vitakavyotekeleza vitu hivyo na kupata watu watakaotekeleza sera hiyo. Utafikiria utapata wapi pesa za kugharamia kazi hiyo na utafanya vipi. Kumbe sera kama nilivyosema hapo juu ni ramani ambayo inaonesha wazi nini kinatakiwa kufanywa, vipi kinatakiwa kufanywa na wahusika wa kukifanya wawe vipi. Sheria inaweka sasa mifupa katika sera kwa kuunda vyombo vya elimu n.k na kutengeneza sheria za kusimamia elimu hiyo na kuhakikisha inakuwa bora.

Sera hutangulia mfumo au miundo mbinu yoyote ya utendaji. Ukishakosea kwenye sera - kuweka malengo yasiyo wazi, yasiyofikika au yanayokinzana - utaunda yvombo ambavyo vitakuwa na majina mazuri lakini vitakavyoshindwa kufanya kazi. Mfano mzuri ni sera ya kuchangia elimu ya juu. Sera hii ilipokuja iliandikwa vizuri sana na watu waliamini basi matatizo ya elimu ya juu yangekuwa yametatuliwa lakini leo hii tumeona jinsi gani yombo mbalimbali vilivyoundwa vimeshindwa kuitekeleza sera hii na kuisababisha ishindwe huku ikichangia matatizo mengi zaidi kwenye sekta hiyo. Sasa hata ukiwafukuza waliopo sasa bodi ya mikopo tatizo litakuwa pale pale.

Ndio maana Mkurugenzi mpya wa Tume ya Uchaguzi alisema kilichowazi kuwa hakuna kitakachobadilika kama uchaguzi utafanyika sasa kwa sababu sera ni ile ile na miundo mbinu yake ni ile ile. Hata kama angetaka kubadilisha hawezi kwa sababu wanatekeleza sera ya CCM. Sera ya CCM inasema kura za Rais zikishatangazwa hakuna wa kuhoji! Well, haijalishi nani anaingia au ana uwezo gani wa kiakili ukweli huo wa sera utaendelea kumtumbulia macho.
 
...Mjenzi akiwa ni mjuzi wa fani yake atagundua na kudokeza dosari au kurekebisha kosa katika ramani. Hatokubali kuharibu kazi yake! ...Tunao madereva waliofuzu vizuri kabisa chuo cha usafirishaji, lakini wanaendesha magari kihuni kabisa mjini, achilia mbali kuvunja sheria za barabarani.

pointi nzuri kabisa, niambie lini umewahi kusikia msomi hata mmoja au mtendaji hata mmoja anasimama kukosoa sera ambazo anatakiwa kuzitekeleza? Wote wanaingia na kujaribu kufanyia kazi kitu ambacho wanakijua hakiwezi kufanikiwa. Sasa hawa ni wajuzi kweli? Ni sawa na fundi ambaye anajua kabisa kuwa hata akijenga nyumba nzuri kiasi gani au mbaya kiasi bado atalipwa! Yeye kapewa ramani na ramani inamuambia ajenge hivi, akikosoa anaambiwa "hii ramani ni nzuri kama hu!
wezi kujenga to specification tutatafuta mtu mwingine" na yeye anataka kula anawajengea matokeo yake? Nyumba ikiisha inaonekana mbaya kweli na kuamuru kubomolewa!

Mfano, ni suala la ujengi karibu na barabara! sera yao iko wazi kabisa lakini miaka nenda rudi watu wamekuwa wakijenga - na wengine ni taasisi za umma - karibu na barabara! Sera yao ni kuwahamisha watu lakini wamewaacha wajenge na vibali vinatolewa humo humo ndani. Lakini anapokuja mwingine anasema tutabomoa. Wanabomoa na kujenga barabara mpya. Wakishamaliza kando ya barabara zile mpya watu wengine wanaanza kujenga!!! Miaka 20 baadaye itakuja bomoa bomoa nyingine!
 
...Tatizo sio wataalamu. Hawa tunao wa-export nchi za nje wanaenda fanya nini? kucheza ngoma?. Nakubaliana na wale wanaoona kuwa tatizo lipo kwenye uongozi, tena wa ngazi zote chini kabisa hadi juu. We need a practical, focused, determined and decisive leadership at all levels.

wanaenda kutekeleza sera zinazotekelezeka! Sera nzuri kulinganisha na walizoziacha nyumbani. Hata uwe na viongozi wazuri kiasi gani kama huna sera nzuri matokeo yatakuwa ni kutokupatana kwa sera mbalimbali . Uongozi peke yake si suluhisho.
 
Back
Top Bottom