Ni Kweli Sera za CCM zimekuwa ni janga kuu la taifa? Tunavuna tunachopanda...?

Mimi nadhani mnazungushana sana ktk swala hili mkisahau kwamba sisi wananchi ndio tunaochagua vyama kutokana na Malengo tulokusudia. Chama kinatupa sera zake tu kutuonyesha ni wao watakao weza kutufikisha pale. Kwa maana hiuyo chama kinatuwekea sera zake ambazo ziwe za kweli ama uongo lakini kipimo cvha mafanikio hakitolewi na chama bali sisi wananchi na taasisi zinazoweka vipimo vya mafanikio kulingana na mahitaji yake.

Hizi fikra za kuwasilikiza CCM wakitwambia wamefanikiwa wapi halafu sisi ndio tunayachukua mafanikio hayo pasipo kuwa na kiwango chetu ndio maana meli yetu inazidi kuzama kama Mwanakijiji anavyosema. Kwa hiyo ni sisi ambao tunatakiwa kujiuza kama sera za CCM zimeweza maana CCM ni supplier na wenye demand ya maendeleo ni sisi wananchi.

Kutegemea CCM itupe hesabu za upande wa demand kama ndio majibu sidhani kama ndivyo inavyotakiwa. CCM watatueleza tu uwezo walioweza ku supply na sisi wenye mahitaji ndio tunajua wametosheleza au laa..They can only answer from their point of view as supplier kama tulivyoahidiwa Umeme na mikakati ya dharura. je, wametosheleza? mfano, ukiwauliza CCM watasema tumeongeza nguvu za umeme kwa asilmia 100% wakati demand yetu ktk umeme ulikuwa kwa asilimia 300.
 
Mkandara, umesema kitu kimoja kizito sana; watu wengi - na nimeona kwenye baadhi ya majibu ya watu hapa - wamepokea maelezo ya CCM kuwa "tatizo siyo sera ni utekelezaji wa sera" na wamekumbatia bila kuhoji. Matokeo yake watu wanarudia msemo huu maarufu kuwa "tatizo siyo sera" na hivyo hata kuziangalia sera zenyewe watu hawaziangalii tena na kuona mapungufu yake. Kwa vile watu waliambiwa "Titanic ni meli isiyozama" watu hawakuangalia mapungufu yake na wakati ilipoanza kuzama watu hawakuamini! Wapo watu wetu ambao wao hata kuziangalia sera za CCM hawataki kwa sababu wanaamini kuwa ni nzuri!

Ukiwauliza kwanini wanaamini hivyo hawawezi kutoa jibu zaidi ya kushindwa kukiri kwamba wanasema hivyo kwa sababu CCM na serikali yake wamekuwa wakisema "ni sera nzuri"!
 
Mwanakijiji:

Kwa maoni yangu binafsi. Sera hazipo Tanzania. Hii ni kwa sababu, sera ni lazima ziwe na charactristics zake. Na hizi characteristics ndizo zinazotenganisha sera na campaign slogans au propaganda.

Kwa mawazo yangu, moja ya characteristics ya sera ni financial resources, and human capital itakayotumika kuendeleza hizo sera.

Kwa mfano katika utangulizi wa hii thread, umetoa sera ya afya. Hutakiwi kuwa rocket scientist kuona kuwa waliokuwa wanapanga financial resources and human capital. Na kama walikumbuka, basi walikuwa wanategemea mfadhiri au mhisani.
 
Good point homeboy!
 
HIvi mmewahi hata kuuliza sera ya Tanzania ya mambo ya ulinzi na usalama inasemaje? au sera ya usafiri wa umma inasemaje? au kuna mtu amewahi kusoma sera ya Tanzania ya mambo ya inteligensia?
 
Kwa taarifa yako:
  1. Hakuna hata wakati mmoja serikali hii imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kufuata sera ya CCM bali inatekeleza kufuata matakwa ya watu binafsi au viongozi binafsi.
  2. Serikali yetu imekuwa hodari sana kwa kuiga mambo kutoka nje bila kufanya utafiti wa kutosha ili kubaini athari zake.
  3. Ahadi nyingi zilizotolewa na JK zinashindikana kupata fedha za kutosha ili zitekelezwe.
  4. Sera ya CCM haina mpango mkakati wa utekelezaji. Kilichotakiwa ni kuwa baada ya CCM kushinda uchaguzi mkuu na kupata ridhaa ya kutawala kilitakiwa kupitia upya ilani yake na kutengeneza mpango mkakati wa utekelezaji. Hivi sasa haupo ndiyo sababu inajigonga gonga.
 
Hivi sera inapotafsiriwa ni 'nzuri' kabla haijatekelezwa ina maana gani? Mimi nafikiri sera inapokuwa imetungwa(formulation), hatua ya pili inatekelezwa, baada ya muda fulani tathmini inafanyika juu ya outcome halafu conclusion kuwa ni nzuri au mbaya inafanyika. Sasa kama haijatekelezwa utajuaje ni nzuri au mbaya? Naomba nielimishwe.
 
Mfumo hautoki hewani; unatokana na sera ambayo nyuma yake kuna itikadi. Itikadi ya chama hutangulia sera za chama; kutokana na mabadiliko mbalimbali katika jamii sera huweza kubadilishwa badilishwa kufuatana na mahitaji. Sera zinatangulia sheria na uundwaji wa vyombo mbalimbali (mfumo). Ukishajua unataka kufanya nini kwenye kilimo na vipi unatoka kwenda kuanza kutengeneza miundombinu ya utekelezaji wa sera hizo. Ukiweka mkazo mkubwa kwenye miundo mbinu unaweza kujikuta unavyovitu vyote muhimu vya mfumo lakini havifanyi kazi kwa sababu havijakubaliana vinataka kufanya nini vipi na na kwanini.
...Majuzi kule Bungeni, Mhe. Makamba alitoa hoja juu ya upangaji nyumba, na kupendekeza marekebisho kadhaa. Nadhani unafahamu alichojibiwa na waziri wa ardhi, Mama Tibaijuka. Hakuna sera inayoshughulikia masuala ya kujenga, kupanga, n.k as far housing sector is concerned, lakini, kulikuwa au kuna sheria inayohusika.

... Sasa, hili ni kosa la sera [sera nzuri, kwa tafsiri yako] kutokuwapo au uongozi uliokuwapo toka awali kutoona upungufu huu na kuuchukulia hatua, toka enzi hizo?
Kwa mfano, ukisema sera yako ya elimu ni kutoa elimu ya bure kwa kila mtoto wa shule ya msingi na sekondari kinachofuatia ni kubadilisha sheria na kuunda vyombo vitakavyotekeleza vitu hivyo na kupata watu watakaotekeleza sera hiyo. Utafikiria utapata wapi pesa za kugharamia kazi hiyo na utafanya vipi. Kumbe sera kama nilivyosema hapo juu ni ramani ambayo inaonesha wazi nini kinatakiwa kufanywa, vipi kinatakiwa kufanywa na wahusika wa kukifanya wawe vipi. Sheria inaweka sasa mifupa katika sera kwa kuunda vyombo vya elimu n.k na kutengeneza sheria za kusimamia elimu hiyo na kuhakikisha inakuwa bora.
...Kwahiyo, hiyo sera nzuri ndio inayosimamia utekelezaji wa hayo yote?. Labda, niulize a philosophical question, nani mwenye uwezo wa kutunga na kutekeleza sera nzuri, kiongozi yeyote tu?. Au, sera nzuri hujizaa au hushuka toka mbinguni?
Sera hutangulia mfumo au miundo mbinu yoyote ya utendaji. Ukishakosea kwenye sera - kuweka malengo yasiyo wazi, yasiyofikika au yanayokinzana - utaunda yvombo ambavyo vitakuwa na majina mazuri lakini vitakavyoshindwa kufanya kazi. Mfano mzuri ni sera ya kuchangia elimu ya juu. Sera hii ilipokuja iliandikwa vizuri sana na watu waliamini basi matatizo ya elimu ya juu yangekuwa yametatuliwa lakini leo hii tumeona jinsi gani yombo mbalimbali vilivyoundwa vimeshindwa kuitekeleza sera hii na kuisababisha ishindwe huku ikichangia matatizo mengi zaidi kwenye sekta hiyo. Sasa hata ukiwafukuza waliopo sasa bodi ya mikopo tatizo litakuwa pale pale.
...Hoja yako kwenye hili ni nini?. Kwamba wanaosimamia shughuli za utoaji mikopo ni watendaji/viongozi wazuri kabisa na wanapaswa kuigwa mfano, tatizo ni sera, iliyoandikwa vizuri?.

...Kwahiyo, tukiifanyia marekebisho ya kuifanya iwe nzuri [hiyo sera] matatizo ya mikopo hii yataisha. Sivyo?.
Ndio maana Mkurugenzi mpya wa Tume ya Uchaguzi alisema kilichowazi kuwa hakuna kitakachobadilika kama uchaguzi utafanyika sasa kwa sababu sera ni ile ile na miundo mbinu yake ni ile ile. Hata kama angetaka kubadilisha hawezi kwa sababu wanatekeleza sera ya CCM. Sera ya CCM inasema kura za Rais zikishatangazwa hakuna wa kuhoji! Well, haijalishi nani anaingia au ana uwezo gani wa kiakili ukweli huo wa sera utaendelea kumtumbulia macho.
...Hii sera ya CCM unayoizungumzia ni ipi? Ninachofahamu ni kuwa, vyama vya siasa vina ilani za uchaguzi, ambazo huzitumia kutengeneza sera mbalimbali za nchi, pale tu wanaposhika madaraka ya serikali.
 
Hivi sera inapotafsiriwa ni 'nzuri' kabla haijatekelezwa ina maana gani? Mimi nafikiri sera inapokuwa imetungwa(formulation), hatua ya pili inatekelezwa, baada ya muda fulani tathmini inafanyika juu ya outcome halafu conclusion kuwa ni nzuri au mbaya inafanyika. Sasa kama haijatekelezwa utajuaje ni nzuri au mbaya? Naomba nielimishwe.
...Ndugu, ulichosema ndicho sahihi. Wakati mwingi sera huwa nzuri kwa kundi fulani la jamii/wananchi na kwa wengine huwa mbaya. Nadhani unakumbuka sera ya kumwezesha mwafrika/mtanzania mweusi na utaifishaji mali binafsi, enzi za mwalimu.

...Au sera ya vijiji vya ujamaa, ambayo haikutekelezwa vizuri kwenye maeneo fulani na kuleta maafa. My argument is, kama ingetekelezwa vizuri, with some moderation, ingazaa matunda mengi zaidi. So yes, kama haijatekelezwa huwezi kuisemea sana, labda kama una mifano ya ilipotekelezwa ikafanikiwa au ikafeli na mazingira yanafanana.
 
Mkandara, umesema kitu kimoja kizito sana; watu wengi - na nimeona kwenye baadhi ya majibu ya watu hapa - wamepokea maelezo ya CCM kuwa "tatizo siyo sera ni utekelezaji wa sera" na wamekumbatia bila kuhoji. Matokeo yake watu wanarudia msemo huu maarufu kuwa "tatizo siyo sera" na hivyo hata kuziangalia sera zenyewe watu hawaziangalii tena na kuona mapungufu yake. Kwa vile watu waliambiwa "Titanic ni meli isiyozama" watu hawakuangalia mapungufu yake na wakati ilipoanza kuzama watu hawakuamini! Wapo watu wetu ambao wao hata kuziangalia sera za CCM hawataki kwa sababu wanaamini kuwa ni nzuri!
...Acha matusi ya reja reja. Tunaifahamu vizuri CCM, na kwahivyo hatuwezi kuaminishwa vitu sivyo ndivyo. Watu wanazifahamu hizo sera [za serikali, na si CCM] vizuri, pamoja na mapungufu yake.

...Tatizo la Titanic lilifahamika/linafahamika pia. Wakubwa hawakufuata ushauri wa wataalamu [nahodha alikataa kuongeza spidi sehemu iliyokuwa na uwezekano wa kuwapo mapande ya barafu, lakini hakusikilizwa] na watendaji wengine [kwenye look out] wakazembea. In history, every now and then, there is bound to be a Titanic. Reminds me of the financial crisis and "How the Mighty Fall".
 
pointi nzuri kabisa, niambie lini umewahi kusikia msomi hata mmoja au mtendaji hata mmoja anasimama kukosoa sera ambazo anatakiwa kuzitekeleza? Wote wanaingia na kujaribu kufanyia kazi kitu ambacho wanakijua hakiwezi kufanikiwa. Sasa hawa ni wajuzi kweli? Ni sawa na fundi ambaye anajua kabisa kuwa hata akijenga nyumba nzuri kiasi gani au mbaya kiasi bado atalipwa! Yeye kapewa ramani na ramani inamuambia ajenge hivi, akikosoa anaambiwa "hii ramani ni nzuri kama huwezi kujenga to specification tutatafuta mtu mwingine" na yeye anataka kula anawajengea matokeo yake? Nyumba ikiisha inaonekana mbaya kweli na kuamuru kubomolewa!
...Hapa ndipo jibu lilipojikita. Huu ni udhaifu wa kiuongozi, kuanzia anayetoa kazi hadi anayepewa bila kumsahau anayeikagua. Ukiangalia sera [tuseme, ya miundombinu] utakuta inaeleza vizuri aina ya barabara tunazohitaji kuzijenga, n.k. Kwa ufupi, kwenye huu ujinga, sera haihusiki.

...Ndio maana, hata Mhe. Magufuli alikataa kupokea barabara ya kilwa, kwa kuwa ilikuwa chini ya kiwango.
 
...Majuzi kule Bungeni, Mhe. Makamba alitoa hoja juu ya upangaji nyumba, na kupendekeza marekebisho kadhaa. Nadhani unafahamu alichojibiwa na waziri wa ardhi, Mama Tibaijuka. Hakuna sera inayoshughulikia masuala ya kujenga, kupanga, n.k as far housing sector is concerned, lakini, kulikuwa au kuna sheria inayohusika.

... Sasa, hili ni kosa la sera [sera nzuri, kwa tafsiri yako] kutokuwapo au uongozi uliokuwapo toka awali kutoona upungufu huu na kuuchukulia hatua, toka enzi hizo ?

Unathibitisha hoja yangu; sera hutangulia mifumo mingine yote. Hoja iliyoletwa Bungeni ilikuwa inataka kutengeneza sheria kabla ya sera! au kutengeneza vyombo vya kusimamia mambo hayo ya upangaji bila kuwa na sera. JIbu la Tibaijuka lilikuwa sahihi. Nani wa kulaumiwa kuwa hakuna sera ya upangaji? CCM!

Jiulize hivi umewahi kusikia sera ya ulinzi na usalama ya Tanzania?
 
Kwa taarifa yako:
  1. Hakuna hata wakati mmoja serikali hii imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kufuata sera ya CCM bali inatekeleza kufuata matakwa ya watu binafsi au viongozi binafsi.
  2. Serikali yetu imekuwa hodari sana kwa kuiga mambo kutoka nje bila kufanya utafiti wa kutosha ili kubaini athari zake.
  3. Ahadi nyingi zilizotolewa na JK zinashindikana kupata fedha za kutosha ili zitekelezwe.
  4. Sera ya CCM haina mpango mkakati wa utekelezaji. Kilichotakiwa ni kuwa baada ya CCM kushinda uchaguzi mkuu na kupata ridhaa ya kutawala kilitakiwa kupitia upya ilani yake na kutengeneza mpango mkakati wa utekelezaji. Hivi sasa haupo ndiyo sababu inajigonga gonga.

Mkapa alijidai kufuata sera zilizoko kwenye ccm manifesto..akawaambia hazitekelezeki..

Sera ni marketing tool hapa kwetu (zinaandikwa na wanazuoni kina Dr. Kitala et.al) from practical point of view

Hakuna Rais anaangalia hayo akishika dola, anaambia hazina kuna TshXXXXX?? weka upya priorities za serikali yako..

Bado external forces/internal forces zina shape sana govenment decisions; by the way nani anataka kuwa kama Qadafi???

Hivyo, mkuu serikali ya nchi maskini na hizi pressure za Illumanati kuna kazi kwelikweli kuzi handle..lol
 
Mkandara, umesema kitu kimoja kizito sana; watu wengi - na nimeona kwenye baadhi ya majibu ya watu hapa - wamepokea maelezo ya CCM kuwa "tatizo siyo sera ni utekelezaji wa sera" na wamekumbatia bila kuhoji. Matokeo yake watu wanarudia msemo huu maarufu kuwa "tatizo siyo sera" na hivyo hata kuziangalia sera zenyewe watu hawaziangalii tena na kuona mapungufu yake. Kwa vile watu waliambiwa "Titanic ni meli isiyozama" watu hawakuangalia mapungufu yake na wakati ilipoanza kuzama watu hawakuamini! Wapo watu wetu ambao wao hata kuziangalia sera za CCM hawataki kwa sababu wanaamini kuwa ni nzuri!

Ukiwauliza kwanini wanaamini hivyo hawawezi kutoa jibu zaidi ya kushindwa kukiri kwamba wanasema hivyo kwa sababu CCM na serikali yake wamekuwa wakisema "ni sera nzuri"!

Mwanakijiji,

Wanaosema kuwa tatizo sio sera, tatizo ni utekelezaji wanasahau kitu kimoja tu. Tanzania ni nchi ya amani kwa miaka 50 sasa na chama kimoja cha siasa kimekuwepo madarakani. Hivyo kwa ngazi za juu wapangaji na watekelezaji wa sera ni wale wale.

Upangaji na utekelezaji wa sera sio sayansi. Hivyo sera za mwanzo mara nyingi zitakuwa na matatizo kwa sababu hakuna knowledge base, na uzoefu wa kufanyia execution. Lakini siku zinavyokwenda ni lazima kuwe na perfection.

Toka tumepata uhuru Tanzania imekuwa na sera. Na katika Afrika, Tanzania ni moja ya nchi chache ambazo zimekuwa na sera bila kuwa na interruptions. Hivyo katika kipindi cha sasa, kushindwa utekelezaji sio kizingizio.

Nasema sio kisingizio kwa sababu katika kipindi cha sasa cha matatizo ya uchumi duniani tunaona nchi mbalimbali zinavyotatua matatizo yao. Nchi kama Greece wamejenga utamaduni wa kutatua matatizo kiujanjaujanja. Na nchi kama Ujerumani wanatatua matatizo yao kwa nidhamu.

Historia inaonyesha kuwa Tanzania inafuata trajectory ya Greece ya kutatua matatizo kiujanjaujanja na kufukia matatizo.
 
Umesema vitu vizuri kweli na mfano wa karibu watu hata hawataki kuukumbuka. Ni serikali hii hii wakati matatizo ya kiuchumi yalipoanza ilikuja na dudu mojaa linaitwa "stimulus package" ya kufufua kilimo. From "somewhere" wakaingiza dola bilioni 1 kwenye kilimo. Sasa ungetarajia kuwa kilimo chetu kingekuwa katika hali nzuri kweli...
 
"2.4.2 Ensure the availability of drugs, reagents and medical supplies and infrastructures.
Hii siwezi kuiita SERA bali ni AHADI! Manake haielezi ni jinsi gani hilo lengo lililokusudiwa linafikiwa.......
 
Hiyo ahadi/lengo iko kwenye "Objectives" za "Tanzania Health Policy"... kwa hiyo siyo ahadi tu ni mojawapo ya malengo ya sera yenyewe. Imefanikiwa?
 
Haijafanikiwa na haiwezi kufanikiwa sababu iko HEWANI...haielezi lengo hilo litafikiwa vipi, Huwezi kutengeneza sera kama hizi halafu unakuja na budget tegemezi kwa 50% hata ktk matumizi ya kawaida!
 
Back
Top Bottom