Ni kweli Papa Wemba kauawa na sumu iliyowekwa kwenye Mic?

Powder

JF-Expert Member
Jan 6, 2016
4,417
5,441
Wakuu nimetizama video moja kwenye account ya Mwanamuziki WA Kikongo, ikionyesha Papa wemba yupo mbele ya steji akiongea na mashabiki akitumia Mic ya nadhani ya Wireless aloshika mkononi, baadaye anakuja mtu na kuiondoa Stand na mic alokua anatumia Papa Wemba, anaondoka nayo back steji, anaonekana anakuja tena huku ameshika Stand Na mic nyingine Na kuiweka nyuma ya Papa Wemba,

Baada ya Show kuendelea baadaye anaonekana Papa Wemba anaanguka chini, show inasimama Na Wanamziki wenzake wanamzunguka kujaribu kutoa msaada, then anaoneka mtu yule yule aliyeleta Mic mwanzo anakuja Na kuibeba Ile Stand Na mic yake alokuja nayo mwanzo, nakuondoka nayo Back steji.

I hope baadhi Wakuu mmeitazama video hiyo! Kuna ukweli kinachoonekana? Kama Kuna mdau anayo anaweza itupia hapa Ili watu waitazame!

===================

Video
 
Nimeiona hyo video ...inawezekana ni kweli aliuwawa
Umeona eeh! Pilika za jamaa zinaonekana 3 times, 1.Akija kutoa Mic ambayo Papa Wemba alikua anatumia, Na Ni baada Tu ya Papa Wemba kusogea mbele kuongea Na Mashabiki... 2.anaileta Stand Na Mic nyingine... 3.anakuja kuondoa Ile mic aloileta baada ya papa wemba kuanguka! Na unaona wakati watu wote wanahangaika Na Papa aliyekua kalala chini, yeye peke yake anaonekana akijishughurisha Na kuondoa Ile mic
 
Nadhani Admin wanaweza kutusaidia, kuileta video hapa! Coz imewekwa Na Mwanamziki WA Kikongo kule fb, Na imeteka hisia za watu kule fb Na imekua mjadala mkubwa!
 
Wakuu nimetizama video moja kwenye account ya Mwanamuziki WA Kikongo, ikionyesha Papa wemba yupo mbele ya steji akiongea na mashabiki akitumia Mic ya nadhani ya Wireless aloshika mkononi, baadaye anakuja mtu na kuiondoa Stand na mic alokua anatumia Papa Wemba, anaondoka nayo back steji, anaonekana anakuja tena huku ameshika Stand Na mic nyingine Na kuiweka nyuma ya Papa Wemba, baada ya Show kuendelea baadaye anaonekana Papa Wemba anaanguka chini, show inasimama Na Wanamziki wenzake wanamzunguka kujaribu kutoa msaada, then anaoneka mtu yule yule aliyeleta Mic mwanzo anakuja Na kuibeba Ile Stand Na mic yake alokuja nayo mwanzo, nakuondoka nayo Back steji, I hope baadhi Wakuu mmeitazama video hiyo! Kuna ukweli kinachoonekana? Kama Kuna mdau anayo anaweza itupia hapa Ili watu waitazame!
Aiseeee! Mkuu hizi ni habari toka kwa wanahabari vilaza, few weeks ago Papa Wemba alianguka (Paris) akashauriwa na Dr. apumzike, baadae alipopona akapewa go ahead tena ya kuendelea na kazi yake.
Pia yeye mwenyewe alijitabiria kifo chake (aliwish afe akiwa stejini).
Tatu tutaishi tupendavyo lakini kifo hakizuiliki. Mda wa Mzee Wemba karudisha amana kwa muumba wake ulifika.
 
Aiseeee! Mkuu hizi ni habari toka kwa wanahabari vilaza, few weeks ago Papa Wemba alianguka (Paris) akashauriwa na Dr. apumzike, baadae apopona akapewa go ahead tena ya kuendelea na kazi yake.
Pia yeye mwenyewe alijitabiria kifo chake (aliwish afe akiwa stajini).
Tatu tutaishi tupendavyo lakini kifo hakizuiliki. Mda wa Mzee Wemba karudisha amana kwa muumba wake ulifika.
Mkuu nazungumzia kuhusu video Na kinachoonekana, sizungumzii hisia Kama zako!
 
Kwani Papa wemba alijihusisha na siasa? wamuue ili wapate nini, alikuwa na ugomvi na nani? au hakuheshimu wake za watu, tuelezeeni kwanza maisha yake kwenye jamii iliyomzunguka yalikuwaje?

Ndipo tutapata pa kuanzia kujiunga nanyi ku speculate.

Kwa maana hata mwanamuziki mkongwe wa reggae Joseph Hill "culture" alifia stajini huko ujerumani.

Nimeweka hiki kipambanuzi ili kuubaini uwezekano wa kufia kwenye stage ukiperform.
 
Joseph Hill - Wikipedia, the free encyclopedia

Nimeweka hiki kipambanuzi ili kuubaini uwezekano wa kufia kwenye stage ukiperform.
Mkuu kila mtu ana maadui, kama ni kweli kinachoonekana kwenye ile video, kufikia watu kusema Papaa kauwawa, huwezi kujua kwa haraka nini chanzo, kumbuka watu hawasemi kwa hisia, wanasema kadri ya kile walichoona kwenye Video.
 
Aiseee. Ok mkuu aliwekewa sumu ktk mic.
Mkuu baada ya Mic kubadirishwa haukupita muda Papa Wemba anaanguka chini, then baadaye unaona mic ikiondolewa, unaona mwenyewe kila kitu, sio story za hisia, yani unaona kwa macho yako.
 
Mkuu kila mtu ana maadui, kama ni kweli kinachoonekana kwenye ile video, kufikia watu kusema Papaa kauwawa, huwezi kujua kwa haraka nini chanzo, kumbuka watu hawasemi kwa hisia, wanasema kadri ya kile walichoona kwenye.
Mtushawishi kupitia video kuwa mic iliyobadilishwa haikuwa na tatizo lolote la kiufundi, lakini pia huyo aliyebadili hiyo mic alikuwa au hakuwa miongoni mwa mafundi mitambo hapo stejini, pana hatua gani zishachukuliwa kwa maana malalamiko kunako vyombo stahiki i.e polisi.
Otherwise hizi ni hallucinations.
 
Mkuu baada ya Mic kubadirishwa haukupita muda Papa Wemba anaanguka chini, then baadaye unaona mic ikiondolewa, unaona mwenyewe kila kitu, sio story za hisia, yani unaona kwa macho yako.
Daaaah! Hahahahah ok mkuu
 
Mtushawishi kupitia video kuwa mic iliyobadilishwa haikuwa na tatizo lolote la kiufundi, lakini pia huyo aliyebadili hiyo mic alikuwa au hakuwa miongoni mwa mafundi mitambo hapo stejini, pana hatua gani zishachukuliwa kwa maana malalamiko kunako vyombo stahiki i.e polisi.
Otherwise hizi ni hallucinations.
Watu wanasubiri uchunguzi WA Mwili WA Marehemu, kinachofanya watu wajadili hii issue Ni Ile video, ambapo hata wewe ukiangalia utawaza mengi zaidi ya ulosema.
 
Wakuu nimetizama video moja kwenye account ya Mwanamuziki WA Kikongo, ikionyesha Papa wemba yupo mbele ya steji akiongea na mashabiki akitumia Mic ya nadhani ya Wireless aloshika mkononi, baadaye anakuja mtu na kuiondoa Stand na mic alokua anatumia Papa Wemba, anaondoka nayo back steji, anaonekana anakuja tena huku ameshika Stand Na mic nyingine Na kuiweka nyuma ya Papa Wemba, baada ya Show kuendelea baadaye anaonekana Papa Wemba anaanguka chini, show inasimama Na Wanamziki wenzake wanamzunguka kujaribu kutoa msaada, then anaoneka mtu yule yule aliyeleta Mic mwanzo anakuja Na kuibeba Ile Stand Na mic yake alokuja nayo mwanzo, nakuondoka nayo Back steji, I hope baadhi Wakuu mmeitazama video hiyo! Kuna ukweli kinachoonekana? Kama Kuna mdau anayo anaweza itupia hapa Ili watu waitazame!

Pole sana Mkuu kwa kuwa na mashaka ya Kifo cha Jules Shungu Kikumba Pene Wembandio alias PAPA WEMBA na pole pia kwa wale wote walioguswa na huu msiba wa JABALI la Afrika ambalo lilibaki la Kizazi cha kwanza baada ya Franco, Tabu Ley, Kabasele Yampanya PEPE KALLE, Madilu System.

Ukweli wa sababu ya Kifo chake ni MSHTUKO wa MOYO kwani imegundulika kuwa wiki moja kabla ya kwenda Abidjan alikuwa anaumwa sana BP na alipewa tiba ambayo ilimlazimu apumzike kwa angalau wiki mbili ndipo arejee kuendelea na muziki lakini mara baada ya PAPA WEMBA kuona kapata nafuu na huku tena Watu wa Kundi la Muziki maarufu ya nchini Ivory Coast la MAGIC SYSTEM ambao ndiyo walikuwa waandaji wakuu wa lile TAMASHA kumpelekea mwaliko aliona asikose kwenda kwani alitaka kuitumia hiyo siku pia kutambulisha album yake.

Kwa mnaoingia sana katika kumbi za muziki nadhani mnatambua aina ya sauti kubwa ambayo inaambata na mitambo mikubwa kabisa na spika za kufa mtu ambazo zinapiga kiasi kwamba kama una matatizo ya kushtuka kwa moyo au kisukari huwezi kukaa pale hivyo hata Marehemu PAPA WEMBA wakati amepanda pale stejini huku akiwa ana siku tano tu tokea atoke kwa Daktari wake kwa matatizo ya moyo ilikuwa ni dhahiri kuwa ile sound set up ya pale ingemuathiri.

Kujibu swali lako kwamba labda aliwekewa SUMU baada ya kuona yule Mtu anakuja kuitoa ile Mic pale na baadae kurudi na nyingine si kweli kwamba ni SUMU bali kila Mwanamuziki Kiongozi wa Bendi huwa na Mic yake MAALUM ambayo husetiwa KIUTAALAM sana na Band Sound System Engineer na hufanyiwa test mara kwa mara ili Bwana mkubwa akipanda nayo tu pale mbele isimumsumbue na huwa haiwi moja bali huwa mbili.

Na pia tambua kuwa kila Mwanamuziki Kiongozi wa Bendi hasa za Kikongo huwapa jukumu MAALUM watu wanaowaamini sana na mno la kukaa au kutunza hizi mic ili kuepuka hujuma kwani kwa msiojua hakuna Watu ambao huwa Wanarogana katika muziki kama Wakongo na ikumbukwe kuna wakati Werrason alimchezea mchezo JB Mpiana katika TAMASHA ambapo katika huo Uwanja kulinyesha mvua kubwa sana lakini cha kushangaza pembezoni na huo uwanja JUA KALI lilikuwa linawaka ( mfano wake ni kwamba pale ukumbi wa Diamond Jubilee sasa pawe wazi halafu inyeshe mvua kubwa lakini maeneo ya jirani kama Makao Makuu ya SKAUTI, Makao Makuu ya Jeshi, Shule ya Msingi ya Muhimbili na yale maeneo mengine kote kuwe na jua kali na linawaka kisawasawa ) hivyo kupelekea JB Mpiana kutofanya onyesho lake na alipokuja kugundua kuwa alifanyiwa ule mchezo na Werrason na yeye JB Mpiana akalipiza ambapo siku moja Werrason na bendi yake ya Maison Mere walikuwa na onyesho lao na cha kushangaza kila Werrason akishika Mic sauti haitoki lakini akiondoa tu ile Mic sauti inarudi na hata alipobadilishiwa Mic zingine tatizo lilikuwa ni lile lile hali ambayo ilipelekea sasa vipande vyote vya uimbaji vya Werrason aviimbe mwanamuziki wake aitwae Herritier lakini cha moto alikiona.

Mshika Mic mkuu wa Koffi Olomide ni yule Mkewe wa sasa aitwae Cindy ambaye ni Mwanamuziki wake pia japo hapo kabla mshika Mic wake alikuwa ni yule muimbaji aitwae Gibson a.k.a Kardinale huku mshika Mic mkuu wa Werrason ni yule mpiga drums wake maarufu aitwae PAPII KAKOL huku JB Mpiana mshika Mic wake mkuu akiwa ni Rapa wake kipenzi aitwae Gentamycine au Antibiotique Lisimo. Hao washika Mic wao wote ndiyo Watu ambao WANAAMINIKA nao kuliko Mtu yoyote katika bendi zao zote hizo na ndiyo wenye sauti kuu pia ya KIMAAMUZI ndani ya hizo bendi za hao MANGULI wa muziki tajwa hapo hivyo kuwekewa SUMU ni jambo gumu mno Mkuu na hawa jamaa Wakongo wanajilinda na vingi na hasa hasa ni NDUMBA.
 
Asante mkuu kwa Maelezo yako mazuri kabisa! Je! Umepata nafasi kuitizama huyo video?
 
Kusema ukweli sijapata nafasi ya kuitizama ila kidogo Mkuu wangu nina uzoefu na hawa Wanamuziki hasa wa miziki hii ya dansi ya Kikongo na hata hapa kibongo bongo kwa hizi bendi zetu pia. Sitaki uamini 100% yale maelezo yangu kwani yawezekana ikawa ni Sumu kama usemavyo ila nimekuelezea tu kwa uzoefu wangu na ni ngumu mno kuwekewa SUMU katika Mic anayoenda kutumia isipokuwa ungeniambia kuwa alifanyiwa UCHAWI ningekuamini kwa asilimia zote kwani hakuna Mwanamuziki unayemjua Wewe wa DR Congo ambaye HAROGI. Kuna siku nitakuja na UZI hapa nikuambie UCHAWI wa wote hao hasa hasa Koffi Olomide, JB Mpiana, Werrason, Roga Roga wa Bendi ya Extra Musica, Zaiko Langa Langa, Hayati Pepe Kalle, Hayati Madilu System na hawa vijana wa sasa wawili Fally Ipupa na mwenzake Fere Gola. Mkuu nikikuambia wanayoyafanya unaweza hata ukaogopa kulala au ukazichukua dvd zao hapo ulipo sasa na ukazichoma moto! Wanamuziki ambao najua walikuwa HAWAROGI ni Hayati Franco na Hayati Tabu Ley pekee.
 
Ok, najua unafahamu mengi kuhusu wanamuziki WA kikongo, video ipo hapo juu, comment no. 36, ipitie hafu uje utuambie kila ulichoona Na uzoefu wako kwa mambo haya! Coz kwenye vyombo vya habari vya Kongo habari ndo hiyo video, Na wanamuziki wakubwa WA Kongo wanasema jamaa kauwawa! Wewe Ni mfatiliaji WA muziki WA kongo, nataka kusikia toka kwako baada ya kuicheki hiyo video.
 
Back
Top Bottom