Ni Kweli Machunde kajitoa Kamati ya Madini?

Sasa ikiwa kila anayesemwa na upinzani au specifically CHADEMA (kama alivyodai Bwana Machunde) ataacha kulitumikia taifa sijui itakuwaje?

Yeye aseme tu kwamba kuna "conflict of interest" ndio maana kajitoa haya mengine yote ya ohh wamenisema, nimefadhaishwa, blah blah blah ya nini???
 
Mwakilishi,

tatizo la wasomi wetu wengi ni uvivu wa ku deal na hoja...wengi hudeal na watoa hoja. Hayo ndiyo madhara ya kusoma ili ufaulu mtihani tu na upate cheti.
 
Tuliambiwa "Machunde anatoka DSE"...kumbe Vertex International Securities? this is very embarrassing indeed. Inamaana mkuu wa kaya hatofautishi DSE na madalali wa soko? Nani walimshauri uongo huu wa wazi? Je credibility yake juu ya maamuzi ya namna hii itapanda au kushuka machoni mwa jamii?

Dhamira yake i wapi juu ya mwelekeo huu ktk kutafuta suluhisho la matatizo ya waTz?

This man now needs to show some seriousness in his office.

Pamoja na ushahidi huu wa link ya machunde na Nazir, bado huyu Machunde anaona si issue ya kupigiwa kelele? Kisa ni Chadema wamesema? Chadema siyo Watanzania?

Huu ni ujinga wa wazi wazi, inawezekana anafanya makusudi, huwezi kuwa mjinga kiasi hicho halafu ukajifanye unaongelea maslahi ya taifa. Hii nchi inaenda wapi jamani?
 
Haya ni baadhi ya maigizo ya JK et al kujaribu kuokoa serikali yake ambayo inazama.

Nimepata pia taarifa kuhusu huyu machunde kuwa kuna kitu waliwahi kuanzisha wakiwa watu kumi na serikali kila mwaka inachangia milioni mia nne kwenye mfuko huo.(400,000,000)per year,haponi mtu hapa ni nondo tuu,waizi wakubwa hawa.

CHADEMA kazeni buti tuu nyuma yenu ,na nitaendelea kuwapa nondo .
 
Bravo JF kwa ma breaking news!

Bravo Chadema.. hata wakisema mwapiga kelele.. matunda ya kazi yenu yanaonekana! Machunde anajiuma uma mwenyewe si kweli kwamba haelewi 'mgongano wa maslahi binafsi'!

Anaogopa tu yaliyo funikwa yatazidi funuliwa! nadhani huu mkakti wa kuwafunua mafisadi madudu yao ni mzuri sana! Walau utawapunguza kasi! Kwa mara nyingine wana anza tingishika!
 
Binafsi naona Machunde kafanya la maana kujitoa kwenye hiyo kamati maana baadhi ya watu na chama cha siasa wamelalamikia uamuzi wa yeye kuwa mjumbe kwa maana kwamba kuna conflict of interest.

Kitu tu ambacho naona Watanzania tukiangalia ni kwamba sio kila Mtanzania mwenye mafanikio ni mwizi. Tujiepushe kuwatuhumu sana Watanzania wenzetu hasa pale ambapo hakuna ushahidi maana tutakakoishia ni kubaya zaidi, mali zote kuwa chini ya wageni.

Kwa Mtanzania kufanikiwa TZ ni kazi ngumu sana hasa kwa wafanyabiashara maana wanakumbana na matatizo kila sehemu, kwa mazingira kama hayo kuna siku watafanya baadhi ya mambo ambayo labda sio safi sana lakini bado naona ni bora uchumi wetu kuwa mikononi mwa Watanzania kuliko hao wageni.
 
ia Jumamosi Nov 24, 2007

Imetolewa mara ya mwisho: 24.11.2007 0107 EAT

•
Kamati ya Madini yaanza kumeguka

sogeza Habari Zinazoshabihiana
• Kikwete amteua Zitto 14.11.2007 [Soma]
• Wampongeza Kikwete kuhusu mikataba ya madini 13.04.2006 [Soma]
• Wanawake watakiwa 'kujitosa' kuchimba madini 08.03.2006 [Soma]

*Mjumbe ajiondoa ni iliyoundwa na Kikwete
*Aitupia lawama CHADEMA kwa maneno maneno

Na Mwandishi Wetu

MMOJA wa wajumbe 12 wa Kamati ya Kupitia Upya Mikataba ya Madini ametangaza kujitoa.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, mjumbe huyo Bw. Peter Machunde, kutoka Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), alisema tayari amewasilisha barua yake kwa Rais.

Bw. Machunde alisema alifikia uamuzi huo kwa masikitiko makubwa na moyo mzito na kuomba ridhaa ya Rais amkubalie ingawa alimteua kwa heshima kubwa kuwa mmoja wa wajumbe.

Alisema uamuzi wake huo umetokana na kusikia maoni na wasiwasi wa baadhi ya watu, ambao alisema walionesha shaka na au kutoridhishwa na uteuzi wake na hivyo kumfanya atafakari kwa kina, kama kuwapo kwake katika Kamati kusingeipunguzia uwezo na uhalali wake miongoni mwa wanajamii.

Bw. Machunde alisema kilichomsikitisha sana ni maoni na wasiwasi wa baadhi ya watu wakishabikiwa na CHADEMA, waliopinga ushiriki wake kwenye Kamati.

"Binafsi nisingependa kuona kuwapo kwangu ndani ya Kamati kunawapa watu hao na chama chao kisingizio cha kumzuia mwanachama mwenzao ashiriki," alisema akimaanisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe.

Alisema hata hivyo kimsingi, Kamati ya Rais ilipokewa vizuri na Watanzania walio wengi kwa kuwa kuundwa kwake kulizingatia maslahi ya Taifa na ni Kamati iliyojumuisha watu wenye uwezo mkubwa na wanaotoa uwakilishi mpana wa jamii.


"Ni kwa sababu hii nimesikitishwa sana na ninashindwa kuelewa, pale baadhi ya viongozi wa CHADEMA wanapoingiza ajenda za kisiasa na kuhusisha chama chao katika suala zito na muhimu kwa maslahi ya nchi yetu.

"Huu ni upungufu kwa chama ambacho kimetumnia suala hilo kwa muda sasa hapa nchini, kuelezea upungufu wa sera na sheria na iweje sasa Rais anapounda Tume kwa maslahi ya Taifa, wao tena ndio wawe kipingamizi cha suala hilo," alisema.

Akizungumza kwa masikitiko, Bw. Machunde alielezea kusikitishwa kwake na mwelekeo wa mtizamo wa baadhi ya Watanzania kushutumiana na kutoaminiana na kujenga mazingira ya wao kujionesha kwenye jamii kwamba wana uchungu na nchi hii, ikiwa ni pamoja na raslimali zake, kuliko wengine.

"Ni imani yangu, kwamba wote tunaipenda nchi yetu kwa kiwango kinacholingana...nimeumizwa na kufadhaishwa sana na dhana inayojengwa na kuenezwa na viongozi wa CHADEMA, kwamba katika ushiriki wangu kama mjumbe wa Kamati hii, nisingeweka maslahi ya nchi yetu mbele.

"Hakuna tusi kubwa kama kudhaniwa kwamba unaweza kuisaliti nchi yako na kuitambua heshima na imani uliyopewa na Rais," alisema na kuwafananisha CHADEMA na genge la wababaishaji.

Alieleza kusikitishwa kwake na kuwapo hila za makusudi za kutaka kuidhoofisha Kamati hiyo kimamlaka, kwa kutumia mbinu chafu za kutumia majina ya watu kukidhi matakwa yao kisiasa.

Alisema huko ni kutojiamini na kutoamini mtu mwingine, licha ya kuwa wana mwakilishi wao Katika Kamati na tena ni kiongozi wa ngazi za juu kabisa.

Bw. Machunde ni mtaalamu wa masuala ya fedha, uwekezaji miradi na masoko ya mitaji mwenye Shahada ya Juu ya Uhasibu (CPA) na ambaye amekuwa mjumbe wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu (NBAA) kwa miaka sita mfululizo.

Alimalizia akisema yeye si mwanasiasa na wala hana jukwaa la kisiasa, la kuelezea na kutetea rekodi yake ya mapenzi, uzalendo na utumishi kwa nchi yake.

"Rais aliponiteua kuingia Kamati hii, niliamini kwamba Kamati ina jukumu kubwa na muhimu kuliko sifa na heshima ya mtu mmoja au chama chochote cha siasa na bado nitaendelea kuamini hivyo, hata nikiwa nje ya Kamati," alisema.

Wajumbe waliosalia kwenye Kamati hiyo ni Mwenyekiti wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu, Jaji Mark Bomani, Bw. Zitto, Mbunge wa Bariadi Mashariki, Bw. John Cheyo na Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe.

Wengine ni Mbunge wa Msalala, Bw. Ezekiel Maige, Bw. David Tarimo wa Kampuni ya PriceWater Coopers na Bibi Maria Kejo ambaye ni Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa katika Wizara ya Katiba na Sheria.

Wajumbe wengine ni Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Bibi Salome Makange, Kamishina wa Sera wa Wizara ya Fedha, Bw. Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi katika Wizara ya Ardhi, Bw. Edward Kihundwa na Mbunge wa zamani wa Ilala, Bw. Iddi Simba

Source: Majira
 
Tumeona, tunamshukuru kwa kujitoa, ila hatukubaliani na propaganda zake za kisiasi ilhali anajinadi kuwa si mwanasiasa....kwa ushahidi huu hapa, inabidi ahojiwe zaidi huenda kuna mengi yamefichika nyuma ya pazia....manake si jambo dogo mwajiriwa wa waziri wa madini kuwa kwenye kamati ambayo inatakiwa kupitia mikataba ya madini ambayo baadhi yake yenye utata kasaini waziri!
 
Mwakilishi,

tatizo la wasomi wetu wengi ni uvivu wa ku deal na hoja...wengi hudeal na watoa hoja. Hayo ndiyo madhara ya kusoma ili ufaulu mtihani tu na upate cheti.

Hili tatizo litakapotibiwa ndipo Tz itaanza mwendo wa kusaka uchumi bora kwasasa hali ilivyo hakuna cha CCM wala CHAMGEMA i mean CHADEMA Itakayo badirisha msimamo wa ligi ya umasikini nchini TZ.

Angalia CHADEMA kitu kisichojadirika yani maamuzi madogo kabisa eti mpaka harimashauri kuu .

Hivi Zito kateuliwa kama mwakirishi wa CHADEMA KTK kamati ama kateuliwa kama Mtanzania mtetea haki??
Hili suala lilitegemea tu Zito mwenyewe kama yeye ni Kondoo ndani ya mbwa mwitu achangamane ama asichangamne sasa hapa CHADEMA imeingia je??

CCM nao madudu ndio sara zao za asubuhi na jioni .

Ama kweli kuwa na Taifa lisilo na wasomi ila lina watu wanaomiliki karatasi kama vyeti ni Taabu tupu
 
Hili
Hivi Zito kateuliwa kama mwakirishi wa CHADEMA KTK kamati ama kateuliwa kama Mtanzania mtetea haki??
Hili suala lilitegemea tu Zito mwenyewe kama yeye ni Kondoo ndani ya mbwa mwitu achangamane ama asichangamne sasa hapa CHADEMA imeingia je??

Ama kweli kuwa na Taifa lisilo na wasomi ila lina watu wanaomiliki karatasi kama vyeti ni Taabu tupu

i) Pamoja na sifa zingine,Zitto kateuliwa kama mpinzani, na anatokea CHADEMA. Ndio kusema asingekuwa CHADEMA/upinzani angekosa sifa muhimu ya kuteuliwa.

ii) Hapana ndugu, watanzania wengi wasomi wamesoma kisawasawa, sio tu eti wanamiliki makaratasi, jenga hoja hapa tukusome acha kukashfu elimu za watu ndugu ehee.
 
"Alimalizia akisema yeye si mwanasiasa na wala hana jukwaa la kisiasa, la kuelezea na kutetea rekodi yake ya mapenzi, uzalendo na utumishi kwa nchi yake.

"Rais aliponiteua kuingia Kamati hii, niliamini kwamba Kamati ina jukumu kubwa na muhimu kuliko sifa na heshima ya mtu mmoja au chama chochote cha siasa na bado nitaendelea kuamini hivyo, hata nikiwa nje ya Kamati," alisema.
"

Sawa, lakini lengo hilo, hata lingekuwa safi kiasi gani, tuna mashaka kuwa haliwezi kutekelezeka ikiwa wewe ni mwajiriwa wa anayeongoza Wizara ambayo mikataba yake mnatakiwa kuichunguza!!

Ni bora ujiondoe kwa kusema wazi kuwa una hoja ya conflic of interest, jamii itakupongeza, kuliko kuwasingizia wengine.
 
Tukio hili la kujiuzuru kwa mjumbe huyu linaturudisha palepale pa mwanzo. Umakini na dhamira ya mteuzi wa kamati hiyo na kuwa na nia ya dhati kutafuta ukweli kamilifu kuhusu jambo linalochunguzwa.

Inazidi kuonekana kuwa juhudi zote hizi ni kutafuta kuzima moto tu na kuyaacha mambo yaendelee yalivyo.
 
Hivi RAISI AMETUDANGANYA WATANZANIA ?,Iweje atuambie huyu bwana ni mwajiriwa wa DSE, NI NINI KILIKUWA KINAFICHWA HAPA?
 
Big UP CHADEMA!Ninapenda wanasiasa wanapofanya homework zao na kutoa mambo yanayoeleweka!Hakuna siasa hapa ila ni facts.
GOOD RIDDENS.....it is clear maslahi yake yako wapi.
Waandishi wetu hata kudesa hapa mmeshindwa???? onyesheni conflict of interest....au ndio kama wanavyosema mmm....na R,..
 
Katika hili, JF ianbidi tujipongeze, wakati mwingine madebe yetu tupu yakipiga kelele yanaamsha watu usingizini. Maadamu tupo karne ya utandawazi, hakuna siri tena.

Washauri wa Rais waliompelekea jina la Machunde walimdanganya. Rais kama kweli anayo nia ya kuliendeleza Taifa letu hana budi kuwawajibisha wale wote waliohusika kwa kumdanganya.

tuhamishieni makombora kwa hao wawili waliobaki ili kamati ibaki na watu clean.

Napendekeza Nafasi yake sasa apewe Prof Shivji.
 
ii) Hapana ndugu said:
Ukweli siku zote huwa kashifa
Niambie msomi hata mmoja kutoka tz aliyegudua hata kuandika theory/law ambayo itadhaniwa kuwa kweli.
acha kujidaganya ndugu yangu wamesoma kisawawasa nithibitishie hilo kwa vigezo.
otherwise nitajikita pale pale HAKUNA MSOMI ,ila wapo wataalamu wa kukalili ambayo wasomi wenzao waliyogundua na kuandika.
 
kama usomi ni uvumbuzi na uandishi wa theory/law zinazokubaliw mbona nchi nyingi tuu zitakuwa na wamiliki karatasi weeegi! ila nasikia kuna watanzania ambao wameshiriki/wanashiriki kwenye tafiti mbali mbali ambazo zimechangia ufumbuzi katika nyanja mbalimbali. ndugu tuwape heshima zao wasomi wetu.
 
link ya Karamagi na Machunde hii hapa,
Business & finance More in this Category!
Sale of Barclays bond starts Wednesday
Abduel Kenge
Daily News; Monday,October 09, 2006 @00:03

Barclays Bank Tanzania will start selling its bond to the public starting Wednesday.

The offer will last for two weeks and will be known as the Barclays Bank Bond Primary Offer. The bond will last for five years.

Vertex International Securities are the sponsoring broker of the medium term bond.
Vertex’s Executive Director, Mr Peter Machunde, said the bond totalling about 10bn/- under a floated rate mechanism would be paid twice in a year.


‘‘The coupon rate is pegged on Treasury bill of the six-month during the payable period,’’ Mr Machunde said. He said the bond redemption year is 2011.

Mr Machunde said the medium term bond was good news to investors because they can compare its maturity with that of other fixed-income securities.

‘‘All other factors being equal, the coupon rate on MTN will be higher than those achieved on short-term notes,’’ Mr Machunde said.

Currently, he said, interest rates are based on floating rate to give ‘‘either side flexibility unlike in the previous ones whereby the investor had to choose between fixed and floating rates.’’

‘‘Bonds attract more serious players like institutions and not individuals, but the first two Barclays bonds were oversubscribed at between ten and 20 per cent,’’ Machunde said.

Kama rais hafahamu hata anaowachagua au anataka kuleta mazingaombwe basi inabidi hili jambo lishughulikiwe na bunge ambalo ndio chombo muhimu kwa sababu ndio hasa wawakilishi wa wananchi. THIS IS VERY SERIOUS.
 
Huyo Machunde aondoke, na wenzie wanaofanana naye ni bora wakafuata mfano wake. Hivi visingizio vya ati kelele za CHADEMA ndizo "zimemfadhaisha" havina maana yoyote kwani siyo CHADEMA iliyomteua. Ni dhamira yake imemsuta baada ya kugundua kwamba kumbe "ukaramagi" wake unajulikana, sasa anaona haya huyoooo! Tuendelee kuwasakama "wakaramagi" wengine popote walipo, mpaka kieleweke.

Kwa pamoja tutaushinda ukaramagi.
 
Back
Top Bottom