Ni kweli Kakakuona anatabiri?

mhondo

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
968
342
Naona ameonekana DSM na anaoneshwa kwenye taarifa ya habari ya Clouds Tv. Kuna watu uwa wanaamini kwamba ana uwezo wa kutabiri je ni kweli ana uwezo huo?
 
Kaka kuona kuonekana tanzania makongo juu dsm je hii inaashiria nini?source clouds tv
 
Umeuliza swali kama ataonekana makongo au ni taarifa kaonekana makongo
 
Acha ushirikina wewe haina maana yoyote ni mnyama tu yule kama wengine

Watu wataendelea kubisha tu hata wingu zito likitanda juu na huku kuna upepo mtulivu hawatakubali kwamba kuna mvua kubwa yaja kunyesha.

Ninyi ndio mnaorudisha nyuma tafiti ambazo zinasaidia kujenga na kuimarisha mfumo wa kusoma ishara za nyakati.

Hata biblia Nabii Issa alisema mtakapoona ishara za taifa moja kulishambulia jingine, matetemeko ya ardhi na mengineyo ujue mwisho wa dunia unakaribia.

Hii ina maanisha kuna mambo mengi kadhaa na matukio kadhaa ambayo huashiria kitu fulani kwa wajuzi wa kusoma. Unakumbuka Joseph alivyomtabiria Farao Misri miaka 7 ya neema na itafuata miaka 7 ya dhiki na njaa? Yalitokea, angepuuzi unabii huo angejua kuzaliwa.
 
si siri hi radio inataka kuchukua nafasi iliyoachwa na shehe Yahaya Hussein loh
 
Watu wataendelea kubisha tu hata wingu zito likitanda juu na huku kuna upepo mtulivu hawatakubali kwamba kuna mvua kubwa yaja kunyesha.

Ninyi ndio mnaorudisha nyuma tafiti ambazo zinasaidia kujenga na kuimarisha mfumo wa kusoma ishara za nyakati.

Hata biblia Nabii Issa alisema mtakapoona ishara za taifa moja kulishambulia jingine, matetemeko ya ardhi na mengineyo ujue mwisho wa dunia unakaribia.

Hii ina maanisha kuna mambo mengi kadhaa na matukio kadhaa ambayo huashiria kitu fulani kwa wajuzi wa kusoma. Unakumbuka Joseph alivyomtabiria Farao Misri miaka 7 ya neema na itafuata miaka 7 ya dhiki na njaa? Yalitokea, angepuuzi unabii huo angejua kuzaliwa.

Kwa hivyo kaka kuona ni nabii kama Musa? kama kweli anatabiri vitu kwanini asichukuliwe ahifadhiwe awe anatabiri kila siku?
 
Jamani mnanikumbusha yule pweza wa ujerumani aliyekuwa anawatabiria ushindi tu kwenye mpira, siku alipowatabiria kinyume waliamua kumuua.
 
Kwa hivyo kaka kuona ni nabii kama Musa? kama kweli anatabiri vitu kwanini asichukuliwe ahifadhiwe awe anatabiri kila siku?

Mapokea ya mnyama Kakakuona ni kuonekana kwake kwa nadra mno isivyo kawaia kitu ambacho huashiria jambo fulani katika jamii kutokea. Tofauti ya mtazamo wako ni kwamba huyu kakakuona achukuliwe awe anatabiri kila siku jambo ambalo umekwenda kinyume cha maana ya tukio hilo. Tafsiri ya kuonekana kwa nadra kakakuona linatafsiriwa hivyo kutokana na pale anapotokea pasipotegemewa na wenye uzoefu wa kumsoma hupata tafsiri ya kuashiria kitu au jambo fulani kuhusianisha na jamii.

Kwamba afugwe haita leta maana tena kwa vile akifugwa hatatokea kwa bahati ya pekee akama inavyotokea bali ni kuonekana kila siku kitu ambacho hakitatuletea tafsiri kadiri ya ishara za nyakati alizotuandalia Muumba wetu. Jaribu Sabayi kukuza kipaji chako cha critical thinking. Thanks.
 
huyu mdudu ni muhimu sana na kuonekana kwake ni mara 1 ktk miaka zaidi ya 10, huwa anatumika kama mtabiri i.e anawekewa unga, bunduki etc akichagua bunduki ujue hali ya amani itakuwa tete na akichagua unga basi ujue kuna njaa kubwa inakuja,,, na pia kipande cha gamba lake kilikuwa kikiuzwa kwa bei mbaya sana kikiaminika kumletea mtu bahati anapotembea nacho, biashara, siasa etc
 
Watu wataendelea kubisha tu hata wingu zito likitanda juu na huku kuna upepo mtulivu hawatakubali kwamba kuna mvua kubwa yaja kunyesha.

Ninyi ndio mnaorudisha nyuma tafiti ambazo zinasaidia kujenga na kuimarisha mfumo wa kusoma ishara za nyakati.

Hata biblia Nabii Issa alisema mtakapoona ishara za taifa moja kulishambulia jingine, matetemeko ya ardhi na mengineyo ujue mwisho wa dunia unakaribia.

Hii ina maanisha kuna mambo mengi kadhaa na matukio kadhaa ambayo huashiria kitu fulani kwa wajuzi wa kusoma. Unakumbuka Joseph alivyomtabiria Farao Misri miaka 7 ya neema na itafuata miaka 7 ya dhiki na njaa? Yalitokea, angepuuzi unabii huo angejua kuzaliwa.

Kuonekana kwa Ngakakuona nako ni utafiti?
 
huyu mdudu ni muhimu sana na kuonekana kwake ni mara 1 ktk miaka zaidi ya 10, huwa anatumika kama mtabiri i.e anawekewa unga, bunduki etc akichagua bunduki ujue hali ya amani itakuwa tete na akichagua unga basi ujue kuna njaa kubwa inakuja,,, na pia kipande cha gamba lake kilikuwa kikiuzwa kwa bei mbaya sana kikiaminika kumletea mtu bahati anapotembea nacho, biashara, siasa etc

Inaelekea huyu mdudu ana uelewa mkubwa kuliko binadamu right?
 
Ushirikina na kutafuta majibu rahisi kwa maswali magumu tu.

Tungefikiria sayansi ni ushirikina yasingegundulika yote haya, leo unajua kama alasiri saa kumi kuna mvua, basi huu nao ni ushirikiana? Baadhi ya watoto wanapozaliwa kuna mambo fulani yasiyo ya kawaida kuwepo au mtoto kuonyesha ishara zisizo za kawaida ingawa ni ishara za wakunga na wazazi lakini kuna kitu kinachoashiria upekee wa mtoto katika maisha yake ndani ya jamii inayomzunguka au dunia.

Hata maskini Lazaro alipokuwa anahangaika kuokota masazo ya tajiri yule aliona ni haki yake. Siku alipokufa Lazaro, tajiri naye yakamkuta yayo baada ya maskini Lazamo kuwa kifuani mwa Abraham, tajiri alivyotaabika kule ahera na kutamani Abraham amtume lazaro walao amtilie tone la maji ndani ya kinywa chake kukata kiu. Alikatishwa tamaa kwamba kati yao hakupitiki na yule tajiri aliashiria basi Lazaro afufuke akawatahadharishe ndugu zake wasifanya aliyomfanyia Lazaro.

Jibu lililomkatisha tamaa ni kwamba, wapo manabii huko, wasipowasikiliza hao, hata aliyefufuka kutoka kuzimu hatasikilizwa pia.

Kwa nini wengine huwa wazito kuukubali ujumbe wa wazi? Kazi kwelikweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom