Ni kitu gani ufanye pale unapofikwa na dhahama kwenye mapenzi (mapenzi chechefu)?

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
12,695
31,486
Wasalaam wana JF

Hakika maumivu ya mapenzi ni magumu sana, hayasikii pain killers, pombe, bangi, maombi na ata ushauri (nasihi). Wapo waliopoteza maisha au kupoteza muelekeo katika maisha waliyoyapoteza. Jambo hili ulione na kulisikia kwa wenzio, usiombe likukute.

Pamoja na magumu na machungu yake, zipo hali na namna ambazo mtu akijiweka na kufanya anaweza kupunguza au kuondoa maumivu ya mapenzi chechefu. Kwa uelewa wangu mdogo na uzoefu wangu wa muda mfupi naomba ni wasilishe haya ili tuendelee kuchakata:

Kutokuwa na matazamio na matumaini kwa mwenzako

Watu wengi wana matazamio na matumaini makubwa kutoka kwa wenzi wao (expectations). Kwamba mpenzi wangu atafanya hivi na vile na hawezi kufanya hili na lile. Matumaini hayo, ndiyo mwiba unaojitega ambao utakuchoma vibaya pale matumaini na matazamio yako hayatafikiwa. Kimsingi, usiwe na matumaini au matazamio yoyote, amimi kila kitu kinaweza kutokea na ujiweke tayari kwa lolote

Usifanye maamuzi ukiwa na furaha au hasira

Mikwamo mingi katika mahusiano inatokana na hisia, maamuzi mengi yanafanywa wakati wa raha. Uamuzi wa kuoa unafanywa baada ya ngono safi au maamuzi ya kuacha yanafanywa baada ya disappointment. Chukua muda, tafakari na ufanye maamuzi wakati ukiwa na utimamu wa akili na hisia zako zikiwa neutral

Tambua sababu ya wewe kuwepo duniani

Jitathmini nini hasa sababu ya wewe kuwepo duniani na kama haujui jipe sababu, weka malengo na unuie kuyafikia. Maisha yako siyo kwaajili ya kukojolesha wengine, kufanya kazi na kuumiza akili na mwili ili wengine wafurahi au wale bata, la khasha, ni kuboresha humanity. Tenda yaliyo mema na usaidie wahitaji lakini uache alama na kama wewe ni kiongozi basi, uache legacy,

Amini kwamba mapenzi ni kama basi la abiria

Daima, ukikosa basi moja, utapanda lingine ( when you miss one bus, you will catch another). Basi si moja, halikadhalika, kufa kwa mapenzi ya leo ndiyo mwanzo wa mapenzi ya kesho. Tuliza nafsi na ujiamini. Dont do anything stupid, relax muda ni jibu la kila kitu.

Usicheze mchezo wowote kama wewe si nahodha

Dont play a game if you are not a captain. Usimuache mtu unayempenda, utajiabisha. Hakikisha unamalizana naye kihisia, yaani akiondoka aondoke kweli moyoni na akilini. Dont play mind games, you will be outplayed. Unapokua caught off guard, pambana urudishe status quo, rudi mchezoni alafu rekebisha makosa usubiri opportunity moment.

Omba upate mtu sahihi

Maisha ni kama puzzle, ni mazuri unapo match ni mabaya when miss matched. Omba upate mtu mtakaye share vision. A convenient person. The rest will be history.

Now, what is your story?
 
Noted.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom