Ni kijotijoti ama ni ki tom and jerry

Mau

Senior Member
Apr 8, 2009
176
10
Wakuu nimekuwa nikisikitishwa sana na usanii wa wasanii wa kitanzania, tumekuwa tukiwapa watu majina na sifa za kibunifu kumbe wizi mtupu hakuna ubunifu. Ninayemuongelea hapa kwa hasira ni Joti wa Orijino Komedi, alionekana mbunifu sana na bado anaendelea kujichukulia sifa zisizo zake kwa ile motion ya kushtua ambayo siku hizi wanaiita (kijotijoti)

Kwa ufuatiliaji mdogo niliofanya nimegundua kwamba kijana huyu (Joti) ameiga motion hiyo kutoka kwa katuni za Tom and Jerry zilizotengenezwa na mtaalam Fredy Quimby.

Angalia hii link hapa chini jinsi Jerry anavyoshtua kwenye motion yake hiyo halafu uniambie ubunifu wa Joti ni upi. hii imetokea kwenye catoon nyingi sana za Fredy Quimbi moja hii hapa na nyingine nitawawekea au mwenye nazo kwa haraka azishushe hapa janvini

Inaumaaaaa

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=jrTyxX9odnU[/ame]
 
Yes Mau hiyo niliiona nikala jiwe, siunajua kibongobongo. Waigaji si kina joti tu hata wanamuziki ni wataalamu sana kwa kuiga. Kazi ipo
 
yani hapo ndo umeona Jerry katembea kijoti? Joti katembea Ki-jerry. we vipi bana. asante though nimeangalia katuni kidogo, nimecheka.
 
mwache aige tu bwana kama anauza kuna tatizo ..kizuri huigwa
Sawa hata kama umeiga kwa kuonyesha uzalendo unatakiwa useme umeiga wapi sio kutudanganya kuwa ni style yako mpya. wenzetu wanaoziahamu wanatushangaa sana eti tunajisifu na mambo yaliyofanyika zaidi ya miaka kumi iliyopita. Firstlady Joti ni Dada yako nini?
 
Sawa hata kama umeiga kwa kuonyesha uzalendo unatakiwa useme umeiga wapi sio kutudanganya kuwa ni style yako mpya. wenzetu wanaoziahamu wanatushangaa sana eti tunajisifu na mambo yaliyofanyika zaidi ya miaka kumi iliyopita. Firstlady Joti ni Dada yako nini?

SINA HATA UKOO NAE

lakini kumbe weye ulitaka aje atangazie uma kwamba style yake ni ya Tom & Jerry :)
Noooooooooooooooooo!
 
Kwa nini msidai ameiba/copy kwenye movie za POLICE ACADEMY?
 
huo mwendo wa kijoti mbona ss tumetembea primary school! hakuna baya lolote alilfanya kutembea kama katuni, ww hujui COMEDY! kama una uwezo wa kuwafurahisha na kuwavunja watu mbavu kwa vimbwanga tayari comedia tayari. wenzio kuchekesha muda wa masaa matatu tu wanakula 10mil-na gharama zote chakula, malazi na usafiri kwako.kama hupendi utajiju
 
Back
Top Bottom