Ni jambo gani la hatari ulishalifanya sababu ya mapenzi?

Duuuu mimi bwana nilimpenda dem mmoja primary sasa mambo yale ya kuandikiana barua nilijikuta kwenye daftari la kiswahili zimebaki kalatasi sita tu,yan nilichalazwa kipindi hicho ila sikusema kalatasi zilikoenda had nikaonewa huruma
Kingine Mambo ya kusubiria dem usiku kwenye giza na karibu na jikoni kwao, kumbe nimesimama kwenye njia ya siafu wakaanza kunipanda mimi bila kujua walivyoanza kuuma nikaanza kupiga piga miguu chini wakati nakimbia kumbe kumbe na waliokuwa jikon wakasikia na wao wakataka kukimbilia ndan ya nyumba chakula kikamwagika so siku hiyo walilala njaa.
 
Poleni Sana kwa maswahibu hayo sijawahi pelekeshwa na mapenz namshukuru Mungu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom