Ni hatua gani za kisheria naweza kuchukua iwapo Tin namba yangu itakuwa imetumika kutengeneza Till za uwakala bila ridhaa yangu?

goodfool

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,664
993
Poleni watanzania wote kwa misiba iliyotufika mwezi huu.

Natumai hamjambo.

Kama nitakuwa nimeeleweka, Naomba kwa mwenye kufahamu nililowasilisha anisaidie kutafsiri sheria au anipe mawazo.

Je iwapo nimepeleka viambata vyote husika kwa muhusika anayeshughulikia masuala ya code za uwakala (Till) kwa kampuni husika, na taarifa hizo (attachments) zikatumika kuzalisha Till zaidi ya moja nakuuzwa kwa watu wengine ni hatua gani za kisheria naweza kuchukua?

Kama ni malalamiko naweza yapeleka TCRA au kitengo gani?

Na kama sina ushahidi wa vidhibiti, nawezaje kuthibitisha madai yangu,

Je naweza kutumia kitu gani kama kidhibiti endapo sijapata Laini husika?

Kwakuwa wapo watu wenye akili pana humu watakua wamenielewa na natumaini nitapata majibu ambayo ni ANTIBIOTIC because I know JF how it is.

Asanteni.
 
Nenda TRA kawaeleze, watakwambia uandike barua ya maelezo hayo yote kwenda kwa mkurugenzi, uchunguzi utafanywa wakijiridhisha kwamba hauhusiki kwenye hizo Till za uwakala watafanya kama kuiuisha TIN yako kwa kufuta baadhi ya uhusika wako kwenye hizo till
 
Kwahiyo hili ni jambo la kawaida kabisa?
 
Back
Top Bottom