Ni haki kusoma message kwenye simu ya mpenzi wako?

hamna kitu nachukia kama kusoma mesej kwenye sim ya mpenz wangu, na yy kusoma msg kwenye sim yangu....why should i breach her privacy, why must she breach mine?
 
Naanza kuwa na mtazamo tofauti na nilivyokuwa nakufikiria katika michango yako ya awali ... anyway naendelea kukusoma!

Mh, Ashadii kwa kweli hapo umeniacha hoi, hata wewe shosti?

Madabwada ulikua na mtazamo gani awali??? lol

Ashadii ametoa scenario zinazoonyesha hali halisi haina maana kuwa ndicho anachokifanya,of which is very true.

haya bana, umepata wa kukutetea .... pamoja dii!
 
mke alichukua simu ya mumewe usiku amelala akaingia kwenye phonebook kila jina la kike akaliandika kesho yake akanunua laini mpya akatuma sms ya kuwatukana bila kujua alituma sms kwa wifi yake..... baada ya uchunguzi ikagundulika yule mke ndio aliyetuma hizo sms .........bado kidogo talaka ingemhusu ilibidi kufunga safari kwenda kwa wifi kuomba msamaha...... achana na simu ya mwenzako...... kusoma msg kwenye simu ya mwenzako sio dawa ya kuzuia madudu anayofanya...
anaweza kukupa simu yake kutwa nzima ukaamini ni salama kumbe loooooo
 
Kuna kitu kinaitwa Privacy.. mahusiano yasiokua na chembe ya Privacy ndo hio usumbua saana maana mnanyimana breathing space.. naamini kua mjanja wa kuchanganya wenza sio mzembe kiasi cha kuwasiliana nae kimahaba kwa message au kumsave under AshaDii.. zaidi zaidi ataweka Alex au hata Prof AshaDii kuonesha ni mtu na heshima zake ili usimhusishe katika mawazo yako ya kushuku... Wanokamatwa na messages ni wale ambao sio wataalam na kufanya kwa kuiga hivyo si fani yao...

Enways mitazamo imetofautiana...

Duh! akya amaulana!, kumbe ndio zinavyoseviwa hivyoeeh??!
 
kuna kila sababu ya kusoma sms kwenye simu ya mpenz wako bt isiwe ndio mchezo wako wa kila siku au jambo la kwanza ufanyalo pindi mkutanapo. Ukiendekeza hii tabia mwenzio atahisi humwamin tena so itakua ugomvi sana..
 
Mi nadhani sim ni private sana na kama mwenyewe hajakupa ruhusa ya kuikagua any time hutakiwi kuikagua.
Ni sawa sawa na mtu anae sema anataka niwe nampeleka popote niendapo ili aone na asikie naongea nini na nani. Nitakereka sana kama mpenzi wangu anasimama nyuma yangu ananisikiliza nikiongea na boss, na muuza vocha, na fundi chereani, na travel agent, na mdogo wangu alie boarding etc. kote nikienda ananiuliza huyu nani na mnaongea nini? kwa nini anakuita dear? etc
Ni mfano mzuri sababu naorganize maisha yangu kupitia sim na naongea na watu wengi. sifichi chochote ila nahitaji space kidogo ili nijiorganize bila pressure. Na kama mtoa mada alisema it goes both ways. hata mimi siwezi mlazimisha mpenzi wangu anipe sim yake kama sina sababu za msingi na hata nikipewa ruhusa ni mara moja tu, next time naomba tena. sio green light ya milele.
 
kwa upande wangu nafuraia zaidi kama hamna mashart yeyote kuhusu sim. especially kwa wana ndoa, kwani ukitaka kutumia sim ya mwenzio wakati umeishwa hela kuna ubaya gani, nayo mpaka uombe ruhusa masaa kabla. why should it be an issue in a relationship? yani unakuta mtu sim yake hata akiisahau mahali roho inamtoka utafikiri kapoteza mamillion.
Kama kwenye relationship mnapendana na kuaminiana swala la sim haltakuwa big deal. Na uaminifu unajengwa na watu wenyewe? Kama ukinipa sababu za kukutilia mashaka sim yako nitaipekua na nitatumia kila njia niwezavyo kutafuta ukweli. if there is no reason to doubt, hata ukiacha sim yako mwaka mzima sitaigusa...hiyo ndio hali halisi.

alafu, if you want your relationship to work, there should not be secrets, siri ndio zinasababisho matatizo kibao kwenye mausiano. kwani kuna ubaya gani mkeo akiona matani yako na marafiki au work mates, tena sometimes you can even volunteer to share na yeye acheke lol!
 
Kwa watu wanaoaminiana hakuna mipaka kwenye matumizi ya simu,lakini ni kukosa uaminifu kuchukua simu ya mwenzio kwa lengo la kumkagua,tayari unakuwa haumwamini,ni ujinga kuishina mtu usiemwamini na mtu mwaminifu haendi kuoga na simu yake,hata ikiita kama mke/mume yupo sio marufuku kupokea na anapopokea anatakiwa kusema"samahani mwenye simu anaoga"hata kama aliyepiga ni oposite na sex ya mwenza wako,sio unaanza 'wewe nani?'unamjuaje mwenye simu?'na maswali mengine ya kuonesha utupu kwenye kufikiri kwako!Mwisho wa yote kila mtu atumie simu kama yake,sio unataka ujue majina ya fonbuku ya mkeo/mumeo hiyo simu sio yako mwache mwenye simu atumie kama yake,kama humuamini ni bora mkaachana kwani hakuna maisha ya furaha kama hamuaminiani!

Umejibu vizuri sana Darling! Mungu aibariki nchi yetu iwe na wanawake wengi wenye uelewa wa kiwango chako ili ndoa zidumu. Kutumia simu ya mpenzi/mume/mke si tatizo ila huyo anayesoma sms, kupokea simu na kukagua simu ya mwenza wake ajipime mwenyewe. Kama nia yake ni kutaka kumchunguza mpenzi wake basi asidhanie watu kumwunga mkono hapa jamvini ndiyo uhalali wa uharamia wake. Anachokifanya ni kosa tena kubwa maana wengi wa watu wa aina yake wameishia kuishi kwa tabu na wengine kuachika wakati ukiwauliza wenye simu utasikia wanalalamikia maswali ya kutoaminiana kila wakati yanayotakana na majina ktk simu, nk vitu ambavyo vimewachosha na kupungua mapenzi.
Tusidanganyane wapendwa; kila mtu anapenda aaminiwe na mpenzi wake hata kama ni kicheche kweli. Mapenzi ni pamoja na kuaminiana na si dozi tu eti hata kama inafanyika katika mazingira ya masononeko na kero.
 
Naanza kuhofia uwezo wa kufikiria.
Ndo kusema ukitoka kazini mumeo akataka kutia kidole ktk engine kupima oil kwa madai ya hofu ya gari lake kutumika kabla halijafika nyumbani kwako sawa tu? Mume kuchungulia madirisha ya ofisi ya mkewe kwa hofu ya bosi kumshika mkewe wewe poa tu?
Mumeo kukuzuia kwenda sokoni bila yeye kwa sababu ya wivu kwako bado ni sawa tu..? Kwanza nakuomba usitake kuhalalisha upunguani wa watu kwa kisingizio cha mapenzi. Kama unasoma simu ya mpenzi wako kutaka kumdhibiti nakupa pole maana siri kubwa ya wachakachuaji ni moja kadri anavyozidi kuwa mwingi wa habari ndivyo anavyozidi kuwa msiri kwa hiyo pole sana! Mimi ni mwanaume na nitakupa uhakika kwamba mimi binafsi na wengine ninaowajua waliacha uchakachuaji si kwa sababu walibanwa bali kwa sababu walinogewa na mapenzi + tabia njema za wenzi wao na mojawapo ya tabia hizo ni heshima. Mwanamke na mwanaume wenye heshima hawashiki simu za wenza wao kwa sababu za wivu bali mapenzi. Mfano wewe unaweza kupoke simu ya jamaa yako ili kumdanganya mtu kuwa jamaa yuko bafuni wakati ukweli ni kwamba mnataka faragha ktk wakati huo. Nendeni unyagoni mjifunze na si kuamini kila kitu ufundishwe Academia au Shule za Kata. Ktk Biology kuna reproduction na hakuna Love/Mapenzi wala mahusiano ya wanao-reproduce.

ujui kama wivu ni kidhibitisho cha mapenzi ya kweli?
 
Simu ni kitu kidogo sana lakini kimekuwa ni chanzo cha talaka na kuvunjika ndoa na relationships nyingi.
Kama kweli unampenda mkeo/mumeo then utamwamini, ukimwamini hutaanza kuvizia kusoma texts zake ama e-mails bababu huo ni ujinga. Jiulize, kwanini umpende ama uishi na mtu ambaye humwamini?
But....if you think, and only if you believe that you have valid reasons which make you suspicious about something going on.....yes, you can go ahead and make your own investigation which includes checking his/her e-mals and texts etc. because cheating is always associated with somebody's email/phone habits
 
kuna kila sababu ya kusoma sms kwenye simu ya mpenz wako bt isiwe ndio mchezo wako wa kila siku au jambo la kwanza ufanyalo pindi mkutanapo. Ukiendekeza hii tabia mwenzio atahisi humwamin tena so itakua ugomvi sana..
sasa unasoma sms za mwenzio za nini na wewe una simu yako? Basi uzeni simu mmoja mtumie mmoja ili mshee vizuri.
 
dah,me c afiki kabisaaa,manake hzo ni stress unajitakia.kama mkeo hpo sawa lkn ka ni mpenz 2 yn dem umeumia manake waweza ji2ndika ukakosa raha za maisha
 
Baeleze! Utani hauwezi kukunyima usingizi mpaka ukaoge na simu mkononi. Tuwe huru, tuwe na mpenzi mmoja wajameni. Mpenzi wako hawezi kugombana nawe kwa sababu ya sms ya utani. Kwa hiyo kwangu mimi kama wewe ni mwaminifu unaweza hata kubadilishana simu na mwenza wako kwa wiki nzima na bado msigombane. Tatizo siku hizi uaminifu ZEROOO.

tatizo kubwa linaloyumbisha ndoa nyingi ni SIRI. na kwa maisha ya siku hizi yanachangiwa zaidi ni hizo simu zenu; kuwa huru tu hata kama unataniwa kama ni kweli utani hakuna atakayekasirika
 
Inategema ndugu..mie nina vimeo kadhaa kwenye cmu nikikomaa kuingilia privacy yake itakula kwangu..ila kawaida repecting somebodys privacy inaonesha kua unamwamini
 
Back
Top Bottom