Nashukuru kwa kunijulisha hivyo mkuu mimi nilidhani Regia ndio Kulwa
VIONGOZI WA MICHEZO NA WADAU WAMUAGA MAREHEMU DOTTO MTEMANYENJE !
WAZIRI wa habari utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (mwenye miwani) aikuaga mwili wa mbunge wa Viti maalum (CHADEMA), Dotto Mtemanyenje katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Simba ambayo Alhaj Ismail Aden Rage (suti) nyeupe naye alikuwa mmoja ya walioshiriki kuaga mwili wa marehemu Dotto Mtemanyenje ambaye anatarajiwa kuzikwa kesho Ifakara, pembeni mwa Rage (kulia) ni aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Jaji Mkwawa.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya fedha ya Simba, Zitto Kabwe akimkumbatia pacha wa marehemu Dotto, Kulwa Mtemanyenje katika zoezi la kuaga mwili wa pacha mwenzake Regia (DoTo)ambaye pia alikuwa mwanachama wa Wekundu wa Msimbazi, Simba.
Ujumbe huo !
Mbunge wa Mbeya mjini (CHADEMA) ambaye pia ni msanii wa hip hop nchini, Joseph Mbilinyi 'Mr.11' naye pia alikuwemo.
MWENYEZI MUNGU AIPUMZISHE ROHO YA MAREHEMU PEMA PEPONI,
Ni kawaida Tanzania mapacha kuitwa Doto(Dotto ni mbwembwe tu hakuna double t!) na Kurwa ingawa wanakuwa na majina yao ya kawaida.
Miss you sister!
Msaada jamani kuna eneo nilipakana na marehemu, ingawa aliandika jina Remija au alimnunulia pacha wake 2011 nafikiri sasa muda umepita mjumbe ameona linakuwa pori analeta watu kuliuza. Please mwenye contact au jinsi ya kuwasiliana na nduguze aniwekee hapa naona sio vizuri kuona haki yake inapotea hivi hivi. Asanteni