Ni benki gani inatoa mkopo bora kati ya NMB na CRDB

Hakuna kitu mbaya kama pesa ya mkopo kuitumia kuanzisha project ni mbaya sana mkuu bt pesa ya mkopo hutumika kukuza project na hapa ndipo watumishi wengi walokimbilia bank huanza kujuta

my take! anza kilimo hata kwa nusu ekari kwa kutumia mshahara wako then baadae kupitia zao hilo hilo utakuwa ushajua abc zake ingia bank komba pesa kawekeze

all the best
That's True coz hakuna kitu tamu kama mkopo
 
Wanakudanganya Mkuu
hata aliyekupa wazo kuwa ukalime matikiti maji.
wewe upo latila ajira ya serikali na unataka uende kijijini ukalime mpunga na matukutu maji.
UNALO SOKO????
mbona uanataka hiyo pesa ikukate na uibiwe
halafu uje JF na mrejesho wa kilio
nakushauri km huna kz nazo achana na mpango
Ni kweli kabisa Mkuu
Zingatia ushauri wangu utakusaidia:
Usikope kwenda kuanzisha biashara kwa kua biashara inachangamoto nyingi, kopa kwaajili ya kuboresha biashara kwa kua utakua na uzoefu na unazijua changamoto za hiyo biashara na kuwa na uhakika wa kupata faida na kurejesha.
Watoa ushauri walio wengi hawakuambii changamoto za hicho wanacho kushauri na kukupigia hesabu rahisi na kukuaminisha kuwa kuna super profit .
 
Nenda bank zote 2 onana na afisa mikopo atakufanyia hesabu, linganisha wapi utapata unafuu.

Pia kama walivyotangulia kusema wachangiaji wengine, usipende kuanza biashara kwa kukopa pesa, anza kwa kushirikisha nguvu zako mwenyewe kidogokidogo mpaka pale utakapo ona inalipa na chamgamoto zake umezimudu, ndipo unaweza kukopa bwana mwalimu.
 
Nakushauri usikope fedha na upeleka kwenye kilimo.
Sababu za kukuambia hivyo ziko nyingi kati ya hizo Ni:-
a) Hatuna Sera nzuri zinazosimamia kilimo, nikiwa na maana hii, viongozi wenye dhamana muda wowote wanasema chochote, kama kuzuia mazao kuuzwa nje ya nchi.
b) Kati ya sekta zinazoadhiriwa na mabadiliko ya Tabia nchi Ni kilimo, hii inamaana risk ni kubwa kwenye kilimo.
c) Nguvu ya soko, katika nchi yetu bei ya bidhaa inabadilika mno kukiwa na sababu za ndani na nje(internal and external factors) mfano zao LA nyanya mwezi wa sita box moja la kilo 25 liliuzwa tsh 45000, mwezi mmoja baadae box hilohilo liliuzwa tsh 8000. mwezi wa nane limeuzwa 2000mwanzoni na baadae zikaanza kuozea shambani.

Kama unataka kujikita kwenye kilimo fuata ushauri uliopewa wa kuanza kidogo kidogo ili kujifunza changamoto zilizopo eneo husika.
Asante
Huwezi kukua bila ya kukopa
Ukiwa bondia usiogope manundu!
 
Heshima kwenu.

Mimi ni mwajiliwa wa serikali na mwezi huu natimiza mwaka mmoja.

Niko kijijini na kuna fursa kubwa ya kilimo cha mpunga na tikiti maji so nimeamua kulima kilimo cha kisasa.

Nataka nikope walau m13 kutoka benki za NMB au CRDB kwani ndo zipo maeneo ya karibu.

Hivyo basi wadau, naomba ushauri wapi pa kukopa kwa riba nafuu bila ya usumbufu wa kuombwa rushwa.

Natanguliza shukrani.

NB: Mshahara wangu ni D kwa viwango vya serikali.
Nakushauri usikope kwanza anza kilimo kwa mtaji mdogo kwanza ambao utatoka ktk mshahara wako.
Ili ujifunze changamoto za kilimo
ukishazijua ndio uchukue mkopo.
 
The higher the risk the higher the return. Kinachorudisha peaa si faida unayoiona kwenye biashata au project. Kinachorudisha faida kinatokana na idea ya project unayotaka kufanya. Ukiona umekubaliwa kuchukua mkopo kutokana a business idea unayotaka kuifanyia basi elewa wataalam wanaona kuna manufaa. After all duniani kote mitaji inapatikana kwa kukopa. Biashara ni idea na plan. Ukiwa na poor planning hata ukikopa kwaajili ya kuiendeleza biashara utakwama tu. Tatizo wengi wanakosa uthubutu. Anyway, kati ya CRDB na NMB uzuri wao unategemea na aina ya mkopo ibaotaka kukopa mfanp morgage au unsecured. Nimeskia kwa morgage nmb is better than crdb. Insecured siwezi kuwapima crdb sababu waliacha kutoa kwa muda kama wameanza ni recent. Ila nmb wapo good pia kwa uzoefu. Kopa kwa malengo.
 
Tanzania Postal Bank ( TPB ) hutojuta!!
hawa jamaa riba yao ni kubwa me naoona wako poa ni equity ile ya kenya ila huko cdhani kama ipo crdb na nmb bora nmb ila kaka kweli m13 ukalime tikiti? asee labda ungenambia ununue mashamba na viwanja ukae baada ya miezi 6 unauzaunanunua tena au ununue mashamba upande miti isisahau kuwa na mradi ambao utakufanya ile gap ya mshahara usiione me nina kiduka kidogo kinansogeza na nlinunua viwanja so nasubiria mwakani nianze kuviuza nijenge
 
Back
Top Bottom