Ni ajabu: Hatujahesabiwa

Maseto

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
944
545
Wana jf, ni ajabu ilioje kutokuhesabiwa familia ya watu 7 huku mtwara.tupo jirani sana na ofisi za wilaya ya masasi. Tumetoa taarifa kwa wahusika zaidi ya mara 3 lakini hadi muda wa sensa unaisha hajatokea mtu wa kutuhesabu.tumeulizia kama ni sisi tu tumeambiwa kuwa ni kaya nyingi tu huku mtwara hazikupitiwa. Kuna tatizo kubwa.inawezekana hata taarifa kuwa 95% wamehesabiwa si za kweli.
 
Nadhani serikali itaendekea kuchukua data zake Wikipedia au TEC
 
Mtwara waislamu ni wengi sana, watakuwa walifikiria kuwa nyie ni waislamu na mmegoma wakaona wasijisumbue kuja huko.
 
Wana jf, ni ajabu ilioje kutokuhesabiwa familia ya watu 7 huku mtwara.tupo jirani sana na ofisi za wilaya ya masasi. Tumetoa taarifa kwa wahusika zaidi ya mara 3 lakini hadi muda wa sensa unaisha hajatokea mtu wa kutuhesabu.tumeulizia kama ni sisi tu tumeambiwa kuwa ni kaya nyingi tu huku mtwara hazikupitiwa. Kuna tatizo kubwa.inawezekana hata taarifa kuwa 95% wamehesabiwa si za kweli.

Bora hamkuhesabiwa kwa sababu isinge make difference. Mimi familia yangu aliyetoa taarifa ni binti wa kazi na alipowaomba warudi jioni watukute tumerudi toka kazini walikataa wakamlazimisha binti wa kazi kusema uongo kwa kukadiria umri wa members 5 wa familia yangu. Sensa imepoteza bure fedha za wahisani
 
kila m2 mjanja. Wanakula kuanzia kwa huyo meneja wa sensa had kwa wasimamizi.
 
Nilikutana karibu na nyumbani kwangu tukasalimiana vizuri nikamuuliza kama ndo amekuja kutuhesabu akasema siji kwenu nimekuja kuchukua chenji yangu hapo kwa jirani yako wewe umeshahesabiwa nikashangaa amepata wapi taarifa zangu wakati mimi nilikuwepo nyumbani muda wote nikiwasubili na sikuwaona. Hii sensa ya mwaka huu ni kituko sana nadhani walikuwa wanahesabu kama inavyofanyika misibani ili kukadilia chakula ina maana hakukuwa na haja ya kuandika majina, umri na wala taarifa zingine?
 
asa weye unataka kutufukizisha kazi?
Ungekuja ofisini mwenyewe usisubiri kufuatwa.
Kesho basi au vp?
VEO
 
Mimi pia na Mke wangu na Mtoto hatujahesabiwa...
Walipita tukawaona wanaongea na wapangaji wenzetu,si wakatukapotezewa wakasepa...
 
Kwani si ilitangazwa kama hukuhesabiwa uwasiliane na mtendaji/mwenyekiti wa mtaa au vijiji?
Ulifanya hayo?
 
sensa ilikuwa siku saba tu.hizo siku nyingine zilikuwa siku za shading kama unabish waulize wasimamiz na makaran kuwa walilipwa cku ngapi za kazi.!!
 
Sensa inamapungufu makubwa sana, hapa ninapokaa kuna wageni (Sio watanzania ) kama Familia nne na zina idadi ya watu sio chini ya 12, wahesabuji walifika na kuchukua details bila kuuliza kama ni Watanzania ama Laaa, sasa hizo Takwimu za kuchukua kila mtu bila kujua utaifa wake ni balaa kabisa
 
Unashangaa huko, sisi Mtaani kwetu Kunduchi Mtongani hatujahesabiwa, tumetoa taarifa serikali za mitaa mara 4 wanaahidi kuja na hawajaja. Kuna kaya kiasi cha 50
 
Back
Top Bottom