Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 9,881
- 20,020
kuna watu wameishi NHC miaka zaidi ya 50, wanalipa kodi ndogo na hela wanazopata wanakula, hawajengi. ukitaka kuwaondoa wanasema twende wapi? mnatuonea rais tusaidie, mara mimi nimeishi miaka yote hapa mnataka niende wapi? tunahitaji NHC itoe semina kwa wapangaji wote kama ifuatavyo:
1. wapangaji wajue NHC ni shirika la serikali, zile nyumba zote ni za serikali, maana yake ni nyumba za watanzania wote hata wale ambao hawajawahi kupanga.
2. NHC iwaambie shirika lipo pale kufanya biashara, sio kutoa msaada, na wana uhuru kuendeleza.
3. wapangaji wakipata nafasi, wajue kuna siku watatakiwa kuondoka, hivyo wajiandae hapo sio kwao
4. ni haki ya NHC kufanya maendelezo na kupangisha mtu wanayemtaka. watu wasumbufu kama hao sisi watanzania hatutaki kuendelea kuwapangisha, hizo sio nyumba za msaada ambazo watu hata wakifa wanarithiana, ni nyumba zetu sisi walipa kodi.
5. sio wao tu ndio wenye haki kukaa humo, watanzania wengi sana huwa wanapenda kuishi kwenye hizo nyumba kwasababu ni za bei ya chini, ila hawapati nafasi kwasababu hao wanaoishi humo wakitaka kuhama huwa wanawauzia watu nafasi kwa pesa ndefu sana. biashara ndani ya biashara.
6. watu wanaokaa humo wanapohama, wanapofariki n.k, NHC waache kuchukua rushwa ili kumpa mwingine, inakuwaje mtu amekaa miaka 60, manake amerithishwa na hana mawazo ya kuhama, hapo ni kwake, sio pa NHC.
NB: kuna siku naamini serikali itaamua kufanya jambo kwenye hizi nyumba. watu wasipange zaidi ya miaka 10, kwasababu zinalemaza sana. wakati sisi wengine tunajinyima kula tujenge, wengine wanakula bata wakitegemea kuishi kwenye nyumba zetu kwa bei nafuu bila kuhamishwa tukitaka kufanya maendelezo. NHC NI NYUMBA ZETU WATZ, NHC NI NYUMBA ZETU WATZ, NHC NI NYUMBA ZETU WATZ kwasababu hilo ni shirika la serikali na serikali ndio sisi, hao wanaozuia maendelezo sio tu wanalihudumu taifa, wanatuhujumu wananchi wengine ambao tuna umiliki wa kitaifa kwenye hizo nyumba.