NHC kutumia Tsh. Bilioni 466 mradi wa Samia Housing Scheme

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Shirika la nyumba za Taifa (NHC) limelenga kutumia zaidi ya Sh460 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 5,000 nchini, huku asilimia 50 ya nyumba hizo ikitegemewa kujengwa eneo la Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.

Mradi huo uliopewa jina la Samia Housing Scheme unatarajiwa kuanza kujengwa mwezi Oktoba mwaka huu ukilenga kuwa na nyumba za bei nafuu ambazo watanzania wa kawaida wataweza kumudu kununua.

Akizungumza kwenye maonyesho ya tano ya teknolojia ya madini yanayoendelea mkoani Geita, Ofisa mauzo na masoko mwandamizi kutoka NHC, Daniel Kure amesema mradi huo utatoa ajira kwa watu zaidi ya 26,000.

“Awamu ya kwanza tunaanzia Dar es Salaam na baada ya hapo tutahamia Dodoma.

“Mradi huu unaangalia vipato vya Watanzania wote wawe watumishi wa serikali, watumishi sekta binafsi au wafanyabiashara wote watapata maana zipo bei za chini na za juu,” amesema Kure.

Akizungumzia madai ya wananchi kuwa nyumba za shirika hilo haziendani na vipato vya wannachi wa kipato cha chini, ofisa habari wa shirika hilo Domina Rwemanyika amesema hiyo inatokana na maeneo husika kukosa miundombinu kama barabara, umeme na maji mambo ambayo hugharimu shirika.

“Tunalazimika kupeleka huduma na hizi gharama ndio huongeza gharama ya nyumba lakini sasa shirika limejitahidi kuhakikisha bei za nyumba zinaendana na kipato cha Mtanzania wa kawaida kabisa,” amesema Rwemanyika.

Mkazi wa mji wa Geita, Scolastica Herman akizungumza baada ya kutembelea banda hilo amesema mji wa Geita ni miongoni mwa miji ambayo bei ya kupanga nyumba iko juu na kwamba ipo haja kwa shirika hilo kuona umuhimu wa kuleta mradi kwenye mji huo.
 
Picha za baadhi ya majengo zitakavyokuwa 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220929-210757.png
    Screenshot_20220929-210757.png
    131.1 KB · Views: 38
Vipi yale majengo yaliyotelekezwa kule kawe, hadi yamepigwa ukungu......hakuna mwendelezo yaani, ni mwendo wa kutafuta kiki kwa mama.
 
Hapo wamedanganya, yaani Kawe ndo ufanikiwe kupata nyumba ya 50M? Haaah hapo Mbingu na Ardhi
Kama pale Morocco na voctoria apartment ziliuzwa mil. 200 hizo za kawe sijui kama zitakuwa chini ya mil 100. Sasa kwa mil. 100 ni watumishi wangapi wanaweza kukopeshwa pesa hiyo benki. Hapo bado makato unaweza kukatwa hadi kiinua mgongo. Nafikiri utaratibu wa awali wa kupangisha ndo unaweza kuwasaidia wafanyakazi na wakazi wengine wa mjini. Wakiwa wamepanga kwa mikataba na bei ambazo siyo za kinyonyaji kama ilivyo kwenye nyumba za watu binafsi ndo wanaweza kujichanga mdogo mdogo kujenga nyumba zao wenyewe.​
 
Shirika la nyumba za Taifa (NHC) limelenga kutumia zaidi ya Sh460 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 5,000 nchini, huku asilimia 50 ya nyumba hizo ikitegemewa kujengwa eneo la Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam.

Mradi huo uliopewa jina la Samia Housing Scheme unatarajiwa kuanza kujengwa mwezi Oktoba mwaka huu ukilenga kuwa na nyumba za bei nafuu ambazo watanzania wa kawaida wataweza kumudu kununua.

Akizungumza kwenye maonyesho ya tano ya teknolojia ya madini yanayoendelea mkoani Geita, Ofisa mauzo na masoko mwandamizi kutoka NHC, Daniel Kure amesema mradi huo utatoa ajira kwa watu zaidi ya 26,000.

“Awamu ya kwanza tunaanzia Dar es Salaam na baada ya hapo tutahamia Dodoma.

“Mradi huu unaangalia vipato vya Watanzania wote wawe watumishi wa serikali, watumishi sekta binafsi au wafanyabiashara wote watapata maana zipo bei za chini na za juu,” amesema Kure.

Akizungumzia madai ya wananchi kuwa nyumba za shirika hilo haziendani na vipato vya wannachi wa kipato cha chini, ofisa habari wa shirika hilo Domina Rwemanyika amesema hiyo inatokana na maeneo husika kukosa miundombinu kama barabara, umeme na maji mambo ambayo hugharimu shirika.

“Tunalazimika kupeleka huduma na hizi gharama ndio huongeza gharama ya nyumba lakini sasa shirika limejitahidi kuhakikisha bei za nyumba zinaendana na kipato cha Mtanzania wa kawaida kabisa,” amesema Rwemanyika.

Mkazi wa mji wa Geita, Scolastica Herman akizungumza baada ya kutembelea banda hilo amesema mji wa Geita ni miongoni mwa miji ambayo bei ya kupanga nyumba iko juu na kwamba ipo haja kwa shirika hilo kuona umuhimu wa kuleta mradi kwenye mji huo.
Safi sana kutokana na mradi huu wananchi watapata fursa za ajira
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom