Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,080
Kwenye vita za zamani kulikuwa kuna utaratibu kabla vita haijaanza inabidi kila upande ukae umbali wa takribani mita 400 (viwanja vinne vya mpira), hivyo kulikuwa na eneo kubwa la wazi kati yao, kila upande ulipeleka mpignaji wao mahiri katikati ya hilo eneo la wazi kupigana ANA KWA ANA mpaka kifo kwa kutumia ngumi, mateke, sambamba na kutumia silaha kama mapanga, rungu, visu, ngaao, mkuki, n.k , baada ya hapo ndio vita ilianza.
Daudi alichaguliwa awe mwakilishi wa pambano hilo huku upande wa pili walimchagua Goliati kwa umahiri wake wa kupigana ana kwa ana, ila cha ajabu Daudi alienda na silaha ya masafa marefu kwenye mapigano ya ana kwa ana, kwa mbali alipoona Goliati anakuja akaweka jiwe kwenye kombeo akalenga kichwa cha Goliati, Kwa wale waliowahi kuuona uwezo wa jiwe la kombeo wanajua kombeo linabeba jiwe kubwa kuzidi manati na jiwe linafika mbali zaidi kwa nguvu zaidi, jiwe moja kombeo linaweza kuua nyati !
Ukiwaona watu wanavyomsifia Daudi kuwa ni shujaa kunaibua sana maswali, utasikia "alimpiga kwa kombeo jiwe moja tu kichwani"
Kuna watu wanatetea kwamba Daudi alijitolea hakuwa mwanajeshi, Hata wanajeshi wetu wa wa JWTZ huwa wanaanza kwa kujitolea JKT, hata vita ya Kagera wanajeshi kibao walijitolea, hata nae Daudi aliingia jeshini kwa kujitolea. hata kama hakuwa na mafunzo kitendo cha jeshi kumruhusu ashiriki vita tena kwenye combat roles huyo tayari ni mwanajeshi.
Pia kutetea Daudi alikuwa kijana mdogo ni hoja dhaifu, kwa wastan tunaweza kukadiria alikuwa na miaka 16, nchi zilizo vitani ni kawaida kukuta watoto wenye miaka 10 wanafundishwa kutumia silaha za mbali kama bunduki kuzitumia kushambulia watu wazima.