Ngome ivue gamba,watumishi wa umma raia wanaopangishiwa nyumba uraiani halafu kodi hailipwi ni gamba

mayoscissors

JF-Expert Member
Nov 24, 2009
975
471
Watumishi wa umma tunaofanya hospitali za jeshi tunadhalilishwa na jeshi hili kwa kutolipa kodi kwenye nyumba tulizopangishiwa uraiani,HAYA NI MAGAMBA NA JESHI LIIGE MFANO WA CCM!
 
Poleni sana, kupangishiwa huku,kumefikia hatua kumeleta madhara kwa Jamii.Jeshi lilipaswa kukaa kambini na si uraini,kitendo cha watumishi na wanajeshi kuishi uraini kimechangia kuvunja maadili ya Jeshi.Tumeona Picha za wanajeshi [Blog ya Michuzi] sale zo zikiwa za tofautitofuati kwenye rangi na hawako smart kama inavyompasa mwanajeshi wa jeshi lolote lile kuwa.Kwa kuwa wako Uraini na hakuna ukakuzi kama ambao ungefanya wakiwa katika hadhi ya makambi yao basi kila kitu kinakua shaghalabagala kwa wanajeshi hawa.

Ukaaji wao huu mitaani umechangia familia hizi za kijeshi kuingiwa na tamaa ya kumilki thamani na vitu kadha wa kadha kama nyumba na magari, nakwa kuwa zinaishi na jamii ambazo kwa namna nyingine hazifanani kipato na familia ya mwanajeshi mhusika ambaye yuko uraini. basi zinarubunika kupata vitu hivyo ili kufanana au kuzidi jamii nyingine hapo mtaani

Hivyo ukosefu wa vitajwa hapo juu, katika familia ya kijeshi kunapelekea matamanio ya kuvimiliki, wakati uwezo na kipato cha mwanajeshi husika ni kidogo na hivyo kupelekea kuibua njia mbadala za kufanikisha upatikanaji wa matakwa ya familia husika ili kuondokana na aibu wanayopopata kutoka katika jumuhiya ya wanajamii uraiani.

Kama thread inavyosema, kama Kodi ya Pango inaleta utata kulipa, nimatarajio yangu mke na wanafamilia wa Mwanajeshi au Mtumishi wa Jeshi husika watanyanyapaliwa na wanajamii ambao wanaona mwanajeshi au mtumishi wa jeshi anastahiki kuishi maisha ya namna fulani.Na jamii yetu ilivyopoteza maadili na kwa kuwa kila mmoja anaishi kwa kipato chake bila kujaliwa uwezo wa jinsi gani amepata kipato hicho, familia hiyo inaiingia kwenye kusimangwa na kuchekwa kuwa si lolote, hivyo kuleta dharau kwa mwanajeshi husika. Hilo ni tatizo JESHI LITOE WANAJESHI WAKE NA WATUMISHI WAKE WANAOISHI MITAANI,NI AIBU KWETU WANANCHI KWA KUWA NI JESHI LETU.
 
Back
Top Bottom