NGOMA ZETU: Mganda jamani, balaaa....

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,062
Wangoni ni kama Wanyamwezi.

Video zao kuzipata ni shida saana maana kila uchaguzi mnachagua .................

Umeme wala vitu kama YOUTUBE ni vya shida sana. Ila kuna mtu alifanikiwa kuchukua picha kadhaa. Labda watu tuanze kitabia cha tukienda vijijini, tuchukue Camera na tuchukue video na kuziweka kwenye mtandao.

Unaweza ukakuta kundi ulilopiga video, linapata deal nzuri sana.


Sikonge,

Tuletee na Mganda kama unazo pamoja na gombe sugu.
 
Last edited by a moderator:
Hapa Wangoni wanakuja na ngoma ya Lizombe......

Ninakumbuka ule wimbo wa "nilipokuwa mwenyewe, mlikuwa hamnisemi x2. Nikiondoka kidogo, nyuma mwanisengenya ehh......."

Mnazidi sana Wangoni kwa kuikumbutia CCM. Mtakufa na umasikini wa kuabudu watu na vyama zao......... Wangini bana, ushamba mtupu.

 
Last edited by a moderator:
Haya basi, kwa leo zinatosha. Nyingine zitafuata baadaye mara Wangoni mtakaponipa MJI ahhh, Mke..............





 
Last edited by a moderator:
Gombe Sugu ni ngoma pia ya Wazaramo. Inasemekana akina mama wanavaa Suruali.

Mdundiko au Mganda wakati wa ukoloni ulipigwa marufuku na Wakoloni.

Wazaramo wakabadili jina na Style kidogo na kuita Gombe Sugu.

Ukiangalia hapa chini, Video ya kwanza kama sikosei ni Gombe Sugu ambayo iko kidogo FAST na inakaribia sana na Mchiriku....



Wimbo hapo juu, umekaribia sana na Disco Chakacha hasa ule wimbo wa "...... mama naumia, ahhh pole mwanangu."


Wimbo huu wa chini ndiyo umekaa haswa kimdundiko na hata kuvaa utagundua kuko tofauti. Hapo juu wanavaa kishughuli haswa....
Nakumbuka mambo ya "Ki-luxury ki-luxury, Pugu Kariakoo au ule wa Kishtobe niba..........(watoto hawajalala) au wa Athmani Maumba...

 
Last edited by a moderator:
Kwa mimi Mzaramo, umenikumbusha kwetu Kimanzichana.

Asante manang'wa Sikonge
 
kwa kweli sikonge umenikonga moyo wangu vibaya mno

hizo video za wazaramo zinanikumbusha mbali sana wakati huo kila wiki mtaani kwetu chini ya miembe kulikuwa lazima kupigwe hayo magoma, vanga, chakacha na mkole(wawakinamama) ila kwenye mkole sie raha yetu ilikuwa kumwangalia mwali anavyonema tena wakati mwingine matiti yakiwa nje

mdundiko by then ndo ilikuwa mziki wa kiswahili hasa, wamama walikuwa wakiacha masufuria yanaungulia kisa kwenda kucheza mdundiko na
iwapo ngoma hiyo ikipita mtaani watoto hujikuta wakisombwa wakija kukumbuka wako kama kilomita mbili au tatu toka nyumbani na wakati mwingine hupotea
dah; kweli sasa twaishi dunia nyingine kabisa, vitu hvyo siku hzi watu hawavishabikii sana huku mijini labda huko pembezoni samvula chole,masaki,na kama alivyosema max kimanzichana
 
YouTube - Tatunane - Msewe

Tatu nane hao,

Kama kuna mtu ana Chezimba, nahitaji vimbwanga vyao. Na kama kuna mtu anajuwa alipo Bruno D Njohole wa chezimba, nipe infor yake please. Au Noriega na/au Ralpha. Mkuu Muddy upo wapi? Muto wa gwan?
 
Hahahahahahaha,Sikonge umenipat rahaaaaaaaaaaa sana kwani napenda sana Mganda na kijiji hicho ambacho wanacheza ni Nyumbani kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. Umenikosha moyo kweli Wakunyumba.
 
Kwa watani zangu ambao mmeburudika, basi nimefurahi sana maana hupenda kuleta furaha kwenye mioyo ya watu.

Ila lazima niseme kuwa Wakwere ni WAZEMBE sana. Yaani hawako makini hata kwenye kucheza.

Kama huamini, hebu angalia ngoma na chezaji yao..... Ovyoooo kabisa.

Bahati mbaya, sina utani na Wakwere maana Kihistoria, Wakwere ni Wanyamwezi waliolowea Pwani.

 
Last edited by a moderator:
hahaaa wakwere bwana?
mambo ya mganda eeh ngoma safi sana hii majirani zetu
afu awa wanacheza sawa na wamanda/wakiss???
 
na nyie kila kitu cha Songea ni wangoni. mganda ni wa WANYASA AKA WANYANJA na wa MANDA. WANGONI AKA TRIBE OF WAR kuna lizombe ligihu na ligwamba kuna chomanga nk. wa hyao na wa KAMBINDI NZURI VIBAYA MNOOO kwa vijana hasa ipo km mdundiko flani hivi lkn yenyewe mwake mnooo. kuhusu ccm naona wanabadirika kidogo kidogo coz nchimbi hakushinda walichakachua matokeo. so wadau ntaanzisha shule ya kucheza ligihu na ligwamba na beta halafu tukichoka tunajipa nguvu na MANGATUNGU na mapwete.
 
Back
Top Bottom