Ngoja nikwambie sasa, sisi wahuni wa miaka ya 90 na tulivyo sasa

kwa mtazamo wangu, pamoja na yote, hapo (kwenye nyekundu) ndipo ilipo hoja kuu ya mtoa mada......nikitumia maarifa ya o'level ya uchambuzi wa kazi za kifasihi naona kabisa mtoa mada anasumbuliwa na aina ya maisha iliyopo sasa kwa vijana wetu;

mifumo ya maisha imebadilika badilika, imevurugwa vurugwa! hakuna ukakamavu wala kugangamala....vijana wamekuwa lainiiiiii, wanashindana na dada zao kutembea na vioo vya kujirembea kwenye vipochi na hatimae ushoga umetapakaa.....wajanja wa siku hizi ni wale wanaoweza kucheza video games vizuri au kuyaelezea mavazi ya kina diamonds vizuri, lakini si wale tena wanaofanya, angalau, mambo ya kishujaa.

watoto wa kiume sasa wanalindwa kama wanavyolindwa watoto wa kike maana ukishangaa tu utakuta wameraruliwa malinda, hawawezi hata kujitetea.....wako lainiiiiii. kijana wa kidato cha nne anagoma kwenda shule eti kisa mama yake hajamtumia hela ya kutumia shuleni.

kijana wa kidato cha nne anaomba ruhusa shule aende kwa mama yake ili akamshonee suruali yake iliyotatuka kidogo mapajani.


mnaokejeli uzi huu mmenishangaza sana!

ahsante sana mtoa mada, umenitafakarisha sana kuhusu yajayo ya vijana wetu hawa!!
Wakulungwa tunaelewa mbona.
 
Unajua nawacheki vijana wa kisasa naona kama wanaigiza uhuni kuliko uhalisia. Sisi tuliishi nyakati za hatari miaka ya 90 halafu bado tumebaki na akili za kusimulia vijana.

Umetoka Ubungo ukapita External, ukapita Garage kituo kinachofuata ni Tabata Relini (Mwananchi)

Ukishuka pale unavuka barabara unaingia kulia unafuata barabara au unaambaa ambaa na reli ile mpaka unaposhuka tena kulia na kupandisha kamlima kadogo ukiacha ile Bar ya Mtaita. (Pale walikuwa pia wanauza Sambusa nzuri sana za Nyama miaka ya 90) ukiendelea mbele utakutana na uliokuwa MJI MPYA.

Ukitembea sana utakuja kutana na Uwanja wa Twiga. Mimi ndo ulikuwa uwanja wangu wa kuangalia mpira jioni, mazoezi au mechi.

Miaka hiyo kuna team ta Twiga iliyokuwa na jersey za utumbo zenye namba kubwa mgongoni 60, 78, 86, 97 n.k

Pale mlangoni ulikuwa unamkuta gollie mmoja mbabe sana anaitwa Omary. Sijui yu wapi huyu bwana. Nataman sana kumwona. Jamaa alikuwa anapendeza sana mlangoni, hasa kwa udakaji wake na alivyokuwa akiwagonga vichwa wachezaji pinzani kwa usiri mkubwa sana.

Kulikuwa na wachezaji wazuri wenye speed mmoja wapo alikuwa Martin Kiberenge. Huyu jamaa alikuwa anakimbia na mpira balaa. Maskini alikuja ishia kuwa mpiga picha tu. But huyu jamaa hakupaswa kucheza soka la Bongo.

Alikuwepo Kiruguru. Huyu alikuwa amekomaa sana na mfupi asiye na woga uwanjani. Kisha unakuja kutana na Mluguru mwingine mrefu ambaye miaka hiyo wenzake wanacheza mpira wamevaa viatu yeye alikuwa anacheza peku na alikuwa anaçhana sana mipira kwa miguu yake.

Alikuwa na nguvu na amekomaa sana. Mechi zilikuwa zinachezwa huku refarii ameweka panga kiunoni maana ilikuwa kipigo nje nje kwa marefa. Kama refa unaonekana umeshindwa kuumudu mchezo basi wananchi wanaonesha wanaweza kukumudu.

Mara nyingi sana kulikuwa kunatokea vipigo vya mawe, mapanga n.k so si ajabu wakati wa kumaliza mpira refa akawa ameenda simama eneo ambalo anajua anaweza chomoka kwa urahisi kukimbia kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.

Wakati huo kundi kubwa la masela lina check mpira huku linavuta bhangi pembeni ya uwanja. Sasa usiwe na kiherehere ukataka uangalie mpira peke yako kwa kusimama na kuwaziba wengine. Utapigwa makonzi mpaka kichwa kibonyee halafu baadaye ndo kivimbe utadhani ndani kimewekwa kokoto pasipo mpangilio maalum.

Maisha mtaani yalikuwa ya ubabe. Demu unampata kwa ubabe na unadumu naye ukiwa mbabe, otherwise watu watakuchukulia tu.

Nakumbuka miaka hiyo ndo kukatokea kutokuelewana katika team ya Twiga ikavunjika na kuwa na Team Mbili. Twiga (Wastaarabu) na Begeju (watoto wa Mbwa) ilikuwa inapigwa game zikikutana team hizi mbili ni hatari na nusu. Na mwishowe si ajabu kutokea kipigo

But kumbuka ni team za hapo hapo na zinatumia uwanja mmoja. Mimi walikuwa mara nyingi wakinishawishi niende nao tunapoenda kucheza mechi mbali,Temeke, Ubungo n.k ili ikitokea tunahitaji kuchapana mkono nami niwape msaaada wangu.

Mimi nlikuwa napenda ugomvi.napenda sana miaka hiyo nmemaliza shule ya Msingi Makubuli/Mabibo then nasoma Tambaza ( wababe wa Dar) so nlikuwa mbabe ila nina akili.

Kulikuwa na wapiga mnanda maarufu miaka hiyo akina Furahisha(alikuja kuwa teja) Fikirini, Ali, Masud na wengine nmewasahau. Bhangi, Mademu na Pombe.

Mimi sasa naonekana mambo safi mtoto wa kidosi ila niliyechangamka.maana nlikuwa naweza kugonga sana ngumi.jamaa wengi kitaa walikuwa wanaishia darasa la saba na wengine hawamalizi hata hilo darasa la saba.

Late 2000 nikiwa mwaka wa 2 UDSM. Mzee aliamua tuhame tuhamie Sinza ambako pia tulikuwa na nyumba na ilikuwa wazazi wanakaa kule sisi na baba mdogo tunaishi huku Tabata Kimanga. Nakumbuka ile picha iliyokuwa na maneno HII NGUNA LAZIMA IISHE LEO,IWE IWEJE!

Miaka ile mitaani ulikuwa huwezi kuta shoga.utampata wapi na vijana tulifunzwa ukakamavu mapema sana? Nilikuwa mhuni sana ambaye leo hii natamani niende fanya visiting yale maeneo niwatafute wana. Zaidi ya miaka 20 sijafika tena huko.

Najitizama najiona nmebadilika sana.nlichange kwa ghafla sana katika maisha na leo hii nmekuwa hivi nilivyo mpole na mwenye aibu sielewi sababu ni nini hasa.
ya kale dhahab aiseee..!!
 
Naona umezungumzia mpira tu alafu una jiita mhuni...mkuu wewe hujafanya uhuni wowote!
 
Sasa uhuni ukowapi hapo? naona yalikuwa maisha ya kawaida tu ya vijana hayo hata vijana wa sasa wanayaishi tena kuzidi hayo.
 
Sasa uhuni ukowapi hapo? naona yalikuwa maisha ya kawaida tu ya vijana hayo hata vijana wa sasa wanayaishi tena kuzidi hayo.
utemi wa zamani si kama wa sasa, siku izi polisi wapo karibu sana,

zamani wahuni wanaweza kufunga mtaa siku nzima wanafanya wanacho taka, saa ivi kidogo tu wamekutia pingu
 
utemi wa zamani si kama wa sasa, siku izi polisi wapo karibu sana,

zamani wahuni wanaweza kufunga mtaa siku nzima wanafanya wanacho taka, saa ivi kidogo tu wamekutia pingu
Sasa hao wanatofauti gani na panya road? Ikifika 2050 watakaokuwa hai vijana watasimuliwa stori za panya road wakati huo tena kutakua na wahuni wengine wa miaka hiyo. Kila miaka na wahuni wake na wote wanazidiana au wanatofautiana namna walivyofanya uhuni wao.
 
Watu wa zaman huwa mnajidai nyie ndo bora sana kuliko vijana wa Sasa lakin mlikuwa washamba tu
Hahahaa but to be honest maisha ya miaka 80s 90s yalikuwa yana usela mavi mnoo...

Yaani watu kupigana mapanga vyupa au vile viti vya chuma ilikuwa kawaida sana watu wakishinda maskani story zao ni kuzamia tu kwenda abroad .. kama ulizaliwa miaka hiyo halafu ukanusurika kuto kuharibika aisee ishukuru dunia wewe ni special
 
Mkuu huo uhuni fresh.....lkn kwa miaka hio hio nikikuletea mambo yaliokua yakitendeka pale Mbeya....haki utabaki mdomoa wazi....

Mbeya town pale nilishudia vijana maeno ya ilemi chini walikua kama nane hivi.....wanapigana kwa visu afu kumbe ni pambano kabisa walishaambiana wakutane wazichape......makundi mawili tofauti........watu watatu walifia pale pale.....!!!

Mzee moja jirani yetu alishushwa kwenye landrover yake kama masihara.....afu watu wakashika uskani wakasepa....kina Nani hao.....Jombi baba
Matukio kama hayo nimeya shuhudia sana miaka hiyo moro town sultan area ilikuwa balaa ...halafu waweza kukuta ugomvi wenyewe ni wakijinga tu

Watu wanagombania demu .kamari .Au wanataka u-brother hood miaka ya zamani ilikuwa watu wana mabeef yakishamba unakuta vijana wa mtaa huu hawa piti mtaa ule na wa mtaa ule hawapiti mtaa huu
 
Miaka hiyo (1995) kuna mtu aliniibia nguo zangu, kwa hasira tu nikausaula hadharani. Yaani nilivua chupi na kunya barabarani huku nikitembea uchi na dushe limesimama kwa hasira. Watu wakapiga kelele lakini wapi, akaja mshikaji kunishika mkono na kunipeleka kwake kujisitiri. Nashangaa jioni naona sanduku la nguo za mitumba naletewa nyumbani na pesa tasilimu kiasi cha 55,000 za kununua nikitakacho. Ilikuwa June 1995. Eti siku hizi mtu anajiita muhuni anapiga punyeto gizani, tena chumbani uvunguni mwa kitanda.
 
Vijana wa 95 kuja juu wengi wameharibika, kijana unavaa suruali inakubana ili iweje? Kuna nilikutana naye alinipa mgongo nikajua manzi kabisa nikataka msemsesha alipogeuka kumbe dume!!
kmmk
 
Miaka hiyo (1995) kuna mtu aliniibia nguo zangu, kwa hasira tu nikausaula hadharani. Yaani nilivua chupi na kunya barabarani huku nikitembea uchi na dushe limesimama kwa hasira. Watu wakapiga kelele lakini wapi, akaja mshikaji kunishika mkono na kunipeleka kwake kujisitiri. Nashangaa jioni naona sanduku la nguo za mitumba naletewa nyumbani na pesa tasilimu kiasi cha 55,000 za kununua nikitakacho. Ilikuwa June 1995. Eti siku hizi mtu anajiita muhuni anapiga punyeto gizani, tena chumbani uvunguni mwa kitanda.
 
Back
Top Bottom