Ngeleja kupokelewa Kifalme!!

Baada ya Mh. Jk kumpiga chini katika Baraza lake la Mawaziri. Chama Cha Mapinduzi katika jimbo lake la Sengerema kinamuandalia mapokezi ya kifalme hapo kesho, ambapo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara.


Kwenye red hapo chumvi imewekwa nyingi karibia inaharibu chakula.
 
Hao watu nao hawana akili kama huyo mbunge wao,
kashindwa kafukuzwa kazi, nyie mnamwandalia sherehe,
vipi nyie akina mwanangosha.
 
Ila akumbuke kumuomba radhi yule askari mlinzi aliyemfukuzisha kazi pale Harbour View!

Malipo ni hapa hapa duniani, nguvu ya umma imemlipia yule mlinzi aliyefukuzishwa kazi na Ngeleja. Ni somo kwa wengine wote ukiwa juu usimdhalau wa chini kwani ni swala la muda tu naye anaweza fika huko na wewe ukawa chini
 
unapopanda mnazi kumbuka kuweka fundo ili utakapokuwa unatelemka uwe na vituo vya kusimama kwanza kuliko utoke juu hadi chini puuuuuu! binadamu tuna tabia ya kujisahau. Mungu anasema utakapofankiwa usimsahau yeye aliyekufanikisha. hivyo watu walifanikiwa wakasahau hata aliyewapa sasa wametelemka ogopa sana Mungu akikutelemsha utajuta........
 
Du!
Mkuu Bondpost,
umekumbuka ishu ya zamani namna hii?...Nakumbuka ilikuwa ni baada ya kuanza kazi tu akamharibia jamaa mlalahoi aisee!

Sio zamani sana mkuu......January 2010

Na Sadick Mtulya


HATIMAYE Pascal Mnaku, mlinzi wa kampuni ya Ultimate Security aliyepambana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kwenye mashine ya kuchukulia fedha (ATM) jijini Dar es Salaam, amefukuzwa kazi na muajiri wake huyo.


Mnaku alijikuta kwenye mpambano mkali na waziri huyo baada ya kumtaka asogee pembeni ya mashine hiyo ya Standard Chartered ili kupisha wateja wengine baada ya Ngeleja kuonekana akitumia muda mwingi kuongea na simu akiwa ndani ya chumba cha mashine hiyo.


Kwa mujibu wa habari tulizozipata kutoka Ultimate na kuthibitishwa na Mnaku, uamuzi wa kumfukuza kazi ulitolewa mara baada ya kikao cha nidhamu cha kampuni hiyo kilichofanyika jana kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi jioni kwenye ofisi za Ultimate.


"Ni kweli nimefukuzwa kazi na hivi ninavyoongea na wewe ndio nimetoka katika kikao cha nidhamu na uamuzi uliofikiwa ndio huo,"alisema mlinzi huyo ambaye hakutetereka wakati Waziri Ngeleja alipohoji kama anamfahamu ni nani wakati akitakiwa kutoka kwenye ATM.


"Na hii ni kutokana na kitendo changu cha kumtaka Waziri Ngeleja awapishe wateja wengine kwenye ATM,"
alilalamika Mnaku.


Jana jioni Mnaku aliliambia Mwananchi kuwa anatakiwa aende kuchukua barua yake ya kutimuliwa kazini Januari 30.


Hata hivyo, mara baada ya gazeti hili kuripoti sakata hilo, Ngeleja alikiri kutokea kwa mtafaruku huo na kujitetea kuwa Mnaku ndiye aliyekuwa chanzo cha mtafaruku huo uliotokea kwenye mashine ya fedha iliyo kwenye jengo la Harbour View (zamani JMall).


Mwananchi iliripoti kuwa waziri huyo alikaribia kuzichapa na mlinzi huyo kwenye baada ya kuombwa asogee pembeni kupisha wateja wengine.
 
Hata Mramba alipokelewa kwa pilau lkn 2010 tupa kule, na ngeleja naye ni walewale na utasikia wenzake akina must na ezekia wakianda pilau kwa ajili ya mapokezi ili kutupiga varnish 2015 tupa kule.
 
Nafananisha hili na Mtu kujitekenya mwenyewe na kucheka mwenyewe!Cost za show born from Ngeleja himself!
 
Ile laana ya yule mlizi itamtafuna hadi mwisho,sidhani kama anaweza fikiria adha ya familia ya mlizi yule baada ya kufukuzwa kazi,sitashangaa akiishia gerezani,mbya sana kuwaonea wanyonge kwa kuwa tu wewe una nafasi fulani
 
Baada ya Mh. Jk kumpiga chini katika Baraza lake la Mawaziri. Chama Cha Mapinduzi katika jimbo lake la Sengerema kinamuandalia mapokezi ya kifalme hapo kesho, ambapo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara.

Nguvu anazo na UWEZO anao pia baada ya kufisadaizi sana.....nenda baba ukafanye Siasa kwani hakika umeshiba.
 
Baada ya Mh. Jk kumpiga chini katika Baraza lake la Mawaziri. Chama Cha Mapinduzi katika jimbo lake la Sengerema kinamuandalia mapokezi ya kifalme hapo kesho, ambapo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara.


Mkutano haujafanyika unauita mkubwa! Unatumia kipimo gani mwenzetu?
 
anahutubia anawaambia nini? atawaeleza zile tanzanite ambazo amekua akizichota pale mererani kazificha wapi au atawaambia nini hasa...
 
mkuuu haw wanalipa wanao kwenda kuwapokea nasikia na maige anapokelewa naye kifalme madiwani wa huko waanaongoza mapokezi
 
Baada ya Mh. Jk kumpiga chini katika Baraza lake la Mawaziri. Chama Cha Mapinduzi katika jimbo lake la Sengerema kinamuandalia mapokezi ya kifalme hapo kesho, ambapo atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara.


Vipi, jimbo la sengerema limeendelea kiwango gani. Kwa vile kazi ya uwaziri imemshinda, ninadhani kuwa huenda kazi ya ubunge aliifanya vizuri. Niliwahi kusikia jamaa huyu akizuia ndege isiondoke Airport Mwanza kumsubiri hadi atoke Sengerema. Mheshimiwa Ngeleja alikuwa na matatizo fulani ya kutaka kuabudiwa kwani kila mara alikuwa anataka watu wamtambue yeye ni nani halafu wafanye anavyotaka yeye; alimfukizisha kazi mlizni wa benki kwa jambo dogo sana, na aliwahi kutishia mapailoti wa ndege za kibongo wasifanye kosa la kumwacha Mwanza awapo safarini hata akichelewaje.
 
nimeshaandaa ndizi kisukari mbili na pili pili mbuzi mfukoni. nakaa mkao wa kula. lazima nizamie hilo punga. issue si kuvaa tu kijani.
 
Back
Top Bottom