Malafyale
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 13,813
- 11,126
WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimebadili utaratibu wa kuwapata wagombea ubunge na udiwani kwa kuruhusu wanachama wao wote kupiga kura za maoni, uongozi wa chama hicho wilayani Sengerema, mkoani Mwanza umewapiga chenga wafuasi wao na kumpitisha mbunge wa Sengerema Mjini, Bw. William Ngeleja kuwa mgombea pekee katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Uamuzi huo umetangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa wa CCM wilayani humo, Bw. Masumbuko Bihemo, alipozungumza na waandishi wa habari jana, akitanabaisha kuwa hatua hiyo ilifikiwa na Halmashauri kuu ya CCM wilaya kilichokutana Mei Mosi mwaka huu.
Alisema kutokana na utaratibu uliowekwa na chama hicho, kikao Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ndicho kikao cha juu na chenye mamlaka katika kubaini viongozi wanaotekeleza shughuli za chama kama inavyotakiwa.
Hata hivyo, uamuzi huo unapingana na maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) iliyoketi Dar es Salaam Aprili 8, mwaka huu na kuamua yafuatayo kuwa: "(NEC) imesisitiza juu ya utaratibu mpya wa kura za maoni kwa wagombea ubunge, uwakilishi na udiwani kwamba kura za maoni zitapigwa na wana CCM wote kwenye matawi yao kwa masharti matatu; "Kwanza mwanachama awe amejiandikisha katika daftari la wanachama tawini, pili awe na kadi ya CCM iliyo hai (iliyolipiwa ada) na tatu awe amejiandikisha katika daftari la wapiga kura na awe na shahada."
Pia maamuzi ya viongozi hao yanakwenda tofauti na tarehe iliyopangwa ya kura za maoni ambayo ni Agosti 8, mwaka huu kwa matawi yote nchi nzima.
Lakini katibu huyo alibainisha kuwa uamuzi wao wa kumpitisha Bw. Ngeleja umeanzia katika ngazi za matawi, kata na kuzishirikisha jumuiya za chama ikiwamo ya vijana (UVCCM) na wazee wa chama hicho na wote walitoa mapendekezo ya kutaka mbunge huyo asiwe na mpinzani.
Alisema sababu pekee iliyowavuta na kufikia uamzi huo ni juhudi za mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini za utekelezaji ilani ya CCM na kuwatumikia wapiga kura wake ipasavyo.
My take:
Kamati kuu ya CCM ilitangaza kura za maoni ndani ya chama hicho ni mwezi August mwaka huu,iweje sasa Ngeleja awe kapita tayari tena bila kupingwa ili hali bado haujafika hata muda kisheria wa kila mwana CCM kuchukua fomu na kugombea kwenye jimbo hilo?