Ngara: Mume aua mama mkwe, ajeruhi mke kisha ajilipua kwa moto kisa wivu wa kimapenzi

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
mume.gif

Ngara. Mfanyabiashara, mkazi wa Kijiji cha Rusumo wilayani hapa mkoani Kagera, Joseph Medard (33) amemuua mama mkwe wake na kumjeruhi mkewe kisha kujimwagia mafuta ya petroli na kujilipua kwa moto kutokana na wivu wa mapenzi.

Taarifa za awali zilieleza kuwa Medard alikuwa na mgogoro wa kifamilia na mkewe na Machi 16 mwaka huu kulikuwa na kikao cha pande mbili za mwanaume na mwanamke ili kuwasuluhisha.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Rusumo, Dausoni Kadende alidai kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku baada ya mfanyabiashara huyo, kumvamia mama mkwe wake, Elizabeth Simoni na kumkata shingo.

Alidai pia mkewe, Elisi Joseph (28) alijeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye shavu la kulia na kutokea kushoto na amelazwa katika Hospitali ya Murugwanza wilayani Ngara akipatiwa matibabu.

Alidai kuwa ugomvi wao ulianza mwishoni mwa Februari kutokana na masuala ya ndoa na mwanamke kulazimika kuomba hifadhi kwa mama yake ambaye aliuliwa na Medard.

“Ugomvi wao ulikuwa ni kulaumiana wakituhumiana kila mmoja kuwa na mpenzi wa pembeni, lakini ilibidi mwanamke aondoke na kuishi kwa mama yake na sisi viongozi hatukujua kinachoendelea,” alidai Kadende.

Ndugu wa marehemu, Danieli Medard alidai kuwa wanandoa hao walikuwa na watoto wanne, mmoja alifariki dunia na kubakiwa na watatu.

Alidai kuwa ndugu yake amekuwa akimtaka mkewe warudiane lakini hakuweza kumsikiliza hata hiyo juzi alikuwa akimsihi wasikae vikao vya familia akimtumia ujumbe wa maandishi kwa simu (sms) lakini hakujibiwa.

“Walioana mwaka 2003 na wameishi vizuri wakilenga kuinua familia na kusomesha watoto wao huko Bukoba lakini kuanzia mwezi wa pili mwishoni walihitilafiana kwa masuala ya ndoa na mkewe kuondoka,” alidai Daniel.

Baba mzazi wa marehemu Joseph, Medard Zephania alisema mwanaye alikuwa na tabia ya kutishia kujiua mara kwa mara.

Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael Mtenjele ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama alikiri kuwapo tukio hilo lakini alisema mwenye kuthibitisha zaidi ni jeshi la polisi wilaya au mkoa.

Jeshi la Polisi Wilaya ya Ngara lilifika eneo la tukio na kuruhusu maiti kuzikwa wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustino Olomi alithibitisha vifo hivyo na kuwahimiza wananchi kutojichukulia sheria mkononi bali watumie vyombo vya sheria kutatua matatizo yaliyoko kwenye jamii husika.

Chanzo: Mwananchi
 
Sometimes huwa ni rahisi sana kuhukumu kama hayakukuta.

Naamini wote tungepewa bunduki tukaishi nazo ndani wakati wa misukosuko ya mapenzi na kifamilia, ingebidi ifunguliwe mahakama maalumu ya kesi za mauaji ya mapenzi.
 
Back
Top Bottom