News Alert: Dr. Maua na wazalendo wafanya kweli tena!

niseme nini miye; ninawashukuru kwa moyo wa dhati wote mliojitolea na mnaoendelea kujitolea. Unajua misaada inahitajika zaidi baada ya kamera na waandishi kuondoka kama tunavyoona kule Haiti. Linapotokea janga watu wanashtuka mara moja na kukimbia kusaidia lakini baada ya muda emotionally watu hawawezi kuendelea kuwa katika "high" for too long.

Matokeo yake ndio watu wanaanza kuzembea na kuchoka, na watu wengine hupoteza maisha baada ya janga lenyewe kutokana na matatizo yanayokuja baadaye. Hii ndiyo sababu ya kufanya kampeni hii kuwa more sustainable badala ya haraka ya wiki moja halafu tunajiondokezea.

Kama mambo yanaenda vizuri tunatarajia kufanya angalau awamu nyingine mbili au tatu hadi ifikapo mwisho wa harambee hii.

Matarajio yangu tutafikia Tsh milioni 300 hivi hivi!
Yote kheri mkuu...inatia moyo kuanza kupanua wigo wa nini tunatakiwa kufanya zaidi ya michango ya harusi ambayo huwa haiishi kwetu huku mijini.
Nafanya hima nipige hodi TPN ili niwe mwanachama. Naona kama kuna nuru inaanza kuangaza pale!
 
Back
Top Bottom