Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,268
- 17,097
Anachokosea ni kujaribu kumuiga Jenerali

mmmhhhhhhh kweli mie simuelewi. Sasa nimemuuliza hajibu. Nikiandika vibaya anatishia kujinyonga. Mi nadhani naomba nimuazime kamba akajinyonge kisha akishamaliza kujinyonga anirudishie kamba yangu.
huyo hata kufikiria kwenye boksi hayupo... labda anafikiria some place which doesnt existMaggid,
Anapata wakati mgumu sana katika hii forum, kwani hapa anakutana na watu wanaofikiria nje ya boksi;
I vowed not to reply to Maggid's posts but let me ask rather than replying him
is there a way you can improve you presentation skills? tumasoma habari nyingi sana ndefu lakini hatuchoki, ya kwako inakosa kitu fulani, its like you are struggling even to understand yourself
Au basi unaweza ukawa unatoa summary ya hizo barua zako?
huyo hata kufikiria kwenye boksi hayupo... labda anafikiria some place which doesnt exist
naskia anataka kujiua, ni kweli?
Maggid, sijajibu post bali nimeuliza swali... hivi kusibu na kuuliza ni sawa??Acid ndugu yangu,
Kuna wanaojibu kwa kuuliza. Nami nakuuliza; Je, umevunja kiapo chako cha kutokujibu posts zangu?
Maggid,
Anapata wakati mgumu sana katika hii forum, kwani hapa anakutana na watu wanaofikiria nje ya boksi; zaidi ya yote, watu wengi hapa wameweka maslahi ya taifa mbele. Mimi nachukizwa sana na article nyingi za huyu Mheshimiwa kutokana na upendeleo wa zairi anaouonyesha kwa Kikwete na chama. Huyu mtu anasafiri vijijini kila siku, ameona mateso ambayo mamilioni ya watanzania waishivyo vijijini wanayopitia lakini anashindwa kuona uwiano katika ya umaskini na sera mbovu za chama tawala.
Ni juzi tuu, mtoto wa Kikwete alitimuliwa hapo Iringa, Maggid aliogopa hata kupost picha kwenye Blog yake. Rais alipokuwa Iringa na kumsafisha mtuhumiwa wa kesi ya rushwa Mwakalebela, Maggid kama kawaida yake alikula kobisi. Inapokuja kwa Dr. Slaa, Maggid anapinga tuu bila sababu za msingi ! Juzi alionyesha rangi zake za asili pale alipojaribu kumtie(kumjumuisha) Dr. Slaa na ugonjwa wa Mr. Kihovella, nilimwandikia email kali sana kwenye comments section ya blog yake na kawaida hakuipost.
Rufiji,
Unayoyaandika hapa hayana chembe ya ukweli. Ni hisia zako tu. Na huyo mgonjwa Mr. Kihovela ni nani? Halafu unashangaa kuwa comments zako hazikuchapwa kule Mjengwablog. Hebu rudi tena kwenye ulichokiandika, angalia facts halafu tuma comments zako, bila shaka zitachapwa.
Mjengwablog si jukwaa la majungu wala kuwatuhumu na kuwahukumu watu kwa kuwataja majina, bila ushahidi.
Ndugu zangu,
Wahehe wana msemo; Isenga imbofu na isenga indenyeefu.
Kwamba ngombe kipofu ni sawa tu na ngombe aliyevunjika mguu, wote watakufa njaa. Ngombe kipofu hawezi kuyaona majani, na yule aliyevunjika mguu naye hawezi kujikokota kwenda kutafuta nyasi za kula.
Tunavyoenenda kama jamii wakati mwingine ni sawa na ngombe kipofu na yule aliyevunjika mguu. Unaweza kuliona hilo nyumbani kwako, katika ukoo wako na hata mahala pako pa kazi.
Leo kuna wanaotafuta visingizio vya kuingia vitani. Kuna wanaodai wanapigana kuwatetea wanyonge walio gizani. Walio gizani nao wameanza kuona katika giza hilo hilo, maana wamekuwa gizani kwa muda mrefu.
Wameshtuka. Wanahoji mantiki ya vita vinavyopiganwa kwa niaba yao. Na walioamua kuingia vitani nao wanaonekana kutojiandaa vema na vita hivyo, wanaelekea kushindwa, maana wanapigana vita vya kinafiki. Na kamwe usiingie kwenye vita kama hujajiandaa.
Mwingine atasema; vita vingine havina budi kupiganwa hata kama hujajiandaa kupigana na kushinda. Hapana, huendi vitani ili mradi tu unakwenda vitani , kama vile unakwenda harusini. Vita si lelemama.
Katika dunia hii inasemwa; chagua vita vyako. Haina maana uchague vita kama unachagua mashati ya mitumba Kariakoo. Ina maana kubwa. Pima kwanza, soma alama za nyakati. Chagua vita inayoshindika, iliyo ya muhimu kupiganwa na unayokuwa na hakika ya kuwa umejiandaa vema kulipa gharama ya ushindi. Kwamba unachokipigania si cha kinafiki.
Angalia kwanza kwenye kabati lako, kabla hujaanza kutangaza kwa watu, kuwa kabati la jirani yako lina mzoga unaonuka, huenda nawe unao, umeanza kutoa harufu, lakini unahisi tu harufu ya mzoga wa jirani yako!
Wengi wetu tumekutana na hali ya kuwaona jogoo wawili wakipambana. Kawaida ya mpambano wa majogoo wawili ni kuvutia watazamaji. Na kila mtazamaji huwa na hulka ya kuchagua jogoo wake wa kumshangilia; kama ni jogoo mweusi na mwekundu, basi, kutakuwa na mashabiki wa jogoo mweusi na wale wa mwekundu. Yahitaji ujasiri kuamua kuwa katikati, kutochagua jogoo wa kumshabikia.
Na hutokea, kwa yule ambaye jogoo wake ameshindwa pambano, basi, atatoka mahali hapo kwa masikitiko, akiwa na unyonge, kisa? Jogoo wake kashindwa! Ni hulka ya mwanadamu. Yahitaji ujasiri kuamua kuwa katikati, kutochagua upande. Kutochagua jogoo wa kumshabikia. Wapo wanadamu wenye ujasiri huo. Pambano linapoendelea au linapomalizika, basi, huweza kutoa tathmini isiyoegemea upande mmoja.
Ndio, tunapaswa pia kutumia bongo zetu katika kutoa hukumu, na si kuongozwa na mapenzi ya moyoni tu. Hivyo ndivyo wafanyavyo mahakimu na majaji wanapoamua mashauri mahakamani. Usiishie tu kumlaani jogoo mwekundu anayeonekana kuwa na maumbile makubwa kwa kumtwanga jogoo wako mweusi mwenye maumbile madogo. Ukiumiza kichwa, unaweza kubaini , kuwa jogoo mwekundu alikuwa na sababu na haki za kumtwanga jogoo wako mweusi. Unatakiwa kuwa na ujasiri wa kuyaangalia mapungufu ya jogoo wako mweusi. Si wengi wenye kutaka kuifanya kazi hii ya kuumiza vichwa, kutafakari mapungufu yao na yale ya wanaowashabikia.
Naam. Maisha ni mapambano, kuna kushinda na kushindwa. Ushindi una gharama. Mwanadamu jiandae na gharama ya ushindi. Ushindi waweza kuwa ghali mno. Unaweza kupambana ukashinda, lakini gharama ya ushindi yaweza kuwa jamaa na marafiki wa wote uliowashinda watageuka kuwa maadui zako, yawezekana
watakuwa maadui kwako kwa muda mrefu tu. Watakukasirikia, watafanya yote nawe upate maumivu.
Hivyo, mwanadamu usifikiri tu gharama ya kushindwa, fikiri pia gharama ya ushindi. Na wakati mwingine, ni gharama inayostahili kulipwa. Franklin Roosevelt alikuwa Rais wa zamani wa Marekani. Alifahamu faida na hasara za kuwa na maadui. Waliompinga katika sera zake za kiuchumi aliwaita " Watiifu wa Kiuchumi" Na akasema; wamejiunga kwa pamoja kunichukia na nakaribisha chuki zao kwangu!
Kama unapigana vita ya muhimu, kama vita hivyo vyaweza vikawa vya kushinda (winnable). Na kwamba umejiandaa kulipa gharama ya chuki ya muda mrefu ya utakaowashinda, basi, ingia vitani, na kama la, tafuta suluhu au rudisha majeshi nyuma kimpangilio ( tactical retreat).
Swali ni hili; utafikiaje uamuzi wa ama kuingia vitani au la?
Miaka mingi iliyopita alitokea Mfalme wa Epilus aliyeitwa Pyrrhic. Mfalme huyu aliamua kuingia vitani kulikabili jeshi kubwa na lenye nguvu nyingi, ni jeshi la Warumi. Lakini kabla ya Mfalme kuingia baharini na vikosi vyake kuitafuta Italia ya Warumi, msaidizi wake wa karibu, Cineas, aliomba mazungumzo ya faragha na Mfalme. Alitaka kumwuliza maswali na kumshauri.
Cineas alimtamkia Mfalme; E bwana Mfalme, Warumi wanasadikika kuwa na jeshi kubwa , lenye nguvu na lenye mashujaa wengi. Ndio maana wameteka nchi nyingi. Je, Mungu akitusaidia, tukaja kuwashinda Warumi,
tutafanya nini na ushindi wetu? Mfalme akajibu: Mbona hilo ni swali jepesi sana. Mara ile tukiwashinda Warumi, hakutatokea jeshi kutoka mji wowote wa Italia litakaloweza kupambana nasi.
Cineas alitulia kidogo, kisha akamwuliza Mfalme: Tukishaikamata Italia ya Warumi, kipi kitafuatia?
Mfalme akajibu: Sicily ni kisiwa chenye hazina za thamani kubwa, itakuwa rahisi sana kukiteka kisiwa hicho.
Cineas aliendelea kuuliza: Bwana Mfalme, unaongea juu ya mambo ya kusadikika, lakini una maana kukitwaa kisiwa cha Sicily kutakuwa na maana ya kukoma kwa vita? Mfalme akajibu: Hapo tutakuwa tumeikaribia Afrika. Na tukishaikamata Afrika ni nani hapa duniani atathubutu kutukabili kivita? Hakuna Alijibu Cineas, kisha akauliza; Na baada ya hapo tutafanya nini?
Mpaka hapo Mfalme hakujua Cineas alikuwa anampeleka wapi kwa lojiki ya kifikra. Mfalme akajibu:
Baada ya hapo, tutapumzika, tutakula raha. Tutakula na kunywa. Tutabaki tukichekeshana na kucheka, siku nzima.
Kama ni hivyo, alisema Cineas; Ni kitu gani kinachotuzuia kufanya hayo yote sasa bila kwenda vitani?
Mfalme hakuielewa mantiki ya Cineas. Akakaidi ushauri. Akavipeleka vikosi vyake kupambana na Warumi. Baada ya vita ngumu, jeshi la mfalme liliwashinda Warumi. Hata hivyo, lilipata hasara kubwa ya kupoteza watu na kuwa na majeruhi wengi. Jeshi lake likadhohofika sana. Likajaribu kuitwaa Sparta, likashindwa vibaya sana. Mfalme aliwindwa na hatimaye akakakamatwa kama kuku na kuawa kwa kupigwa mawe kwenye mitaa ya Argos.
Isenga imbofu na isenga indenyeefu. Ngombe kipofu ni sawa tu na ngombe aliyevunjika mguu.
Na hilo ndilo Neno Leo.
Maggid,
Iringa.
Maggid, sijajibu post bali nimeuliza swali... hivi kusibu na kuuliza ni sawa??
Rufiji,
Unayoyaandika hapa hayana chembe ya ukweli. Ni hisia zako tu. Na huyo mgonjwa Mr. Kihovela ni nani? Halafu unashangaa kuwa comments zako hazikuchapwa kule Mjengwablog. Hebu rudi tena kwenye ulichokiandika, angalia facts halafu tuma comments zako, bila shaka zitachapwa.
Mjengwablog si jukwaa la majungu wala kuwatuhumu na kuwahukumu watu kwa kuwataja majina, bila ushahidi.
Kwa hiyo warumi ndiyo ccm eeeh?Ndugu zangu,
Wahehe wana msemo; Isenga imbofu na isenga indenyeefu.
Kwamba ng'ombe kipofu ni sawa tu na ng'ombe aliyevunjika mguu, wote watakufa njaa. Ng'ombe kipofu hawezi kuyaona majani, na yule aliyevunjika mguu naye hawezi kujikokota kwenda kutafuta nyasi za kula.
Tunavyoenenda kama jamii wakati mwingine ni sawa na ng'ombe kipofu na yule aliyevunjika mguu. Unaweza kuliona hilo nyumbani kwako, katika ukoo wako na hata mahala pako pa kazi.
Leo kuna wanaotafuta visingizio vya kuingia vitani. Kuna wanaodai wanapigana kuwatetea wanyonge walio gizani. Walio gizani nao wameanza kuona katika giza hilo hilo, maana wamekuwa gizani kwa muda mrefu.
Wameshtuka. Wanahoji mantiki ya vita vinavyopiganwa kwa niaba yao. Na walioamua kuingia vitani nao wanaonekana kutojiandaa vema na vita hivyo, wanaelekea kushindwa, maana wanapigana vita vya kinafiki. Na kamwe usiingie kwenye vita kama hujajiandaa.
Mwingine atasema; vita vingine havina budi kupiganwa hata kama hujajiandaa kupigana na kushinda. Hapana, huendi vitani ili mradi tu unakwenda vitani , kama vile unakwenda harusini. Vita si lelemama.
Katika dunia hii inasemwa; chagua vita vyako. Haina maana uchague vita kama unachagua mashati ya mitumba Kariakoo. Ina maana kubwa. Pima kwanza, soma alama za nyakati. Chagua vita inayoshindika, iliyo ya muhimu kupiganwa na unayokuwa na hakika ya kuwa umejiandaa vema kulipa gharama ya ushindi. Kwamba unachokipigania si cha kinafiki.
Angalia kwanza kwenye kabati lako, kabla hujaanza kutangaza kwa watu, kuwa kabati la jirani yako lina mzoga unaonuka, huenda nawe unao, umeanza kutoa harufu, lakini unahisi tu harufu ya mzoga wa jirani yako!
Wengi wetu tumekutana na hali ya kuwaona jogoo wawili wakipambana. Kawaida ya mpambano wa majogoo wawili ni kuvutia watazamaji. Na kila mtazamaji huwa na hulka ya kuchagua jogoo wake wa kumshangilia; kama ni jogoo mweusi na mwekundu, basi, kutakuwa na mashabiki wa jogoo mweusi na wale wa mwekundu. Yahitaji ujasiri kuamua kuwa katikati, kutochagua jogoo wa kumshabikia.
Na hutokea, kwa yule ambaye jogoo wake ameshindwa pambano, basi, atatoka mahali hapo kwa masikitiko, akiwa na unyonge, kisa? Jogoo wake kashindwa! Ni hulka ya mwanadamu. Yahitaji ujasiri kuamua kuwa katikati, kutochagua upande. Kutochagua jogoo wa kumshabikia. Wapo wanadamu wenye ujasiri huo. Pambano linapoendelea au linapomalizika, basi, huweza kutoa tathmini isiyoegemea upande mmoja.
Ndio, tunapaswa pia kutumia bongo zetu katika kutoa hukumu, na si kuongozwa na mapenzi ya moyoni tu. Hivyo ndivyo wafanyavyo mahakimu na majaji wanapoamua mashauri mahakamani. Usiishie tu kumlaani jogoo mwekundu anayeonekana kuwa na maumbile makubwa kwa kumtwanga jogoo wako mweusi mwenye maumbile madogo. Ukiumiza kichwa, unaweza kubaini , kuwa jogoo mwekundu alikuwa na sababu na haki za kumtwanga jogoo wako mweusi. Unatakiwa kuwa na ujasiri wa kuyaangalia mapungufu ya jogoo wako mweusi. Si wengi wenye kutaka kuifanya kazi hii ya kuumiza vichwa, kutafakari mapungufu yao na yale ya wanaowashabikia.
Naam. Maisha ni mapambano, kuna kushinda na kushindwa. Ushindi una gharama. Mwanadamu jiandae na gharama ya ushindi. Ushindi waweza kuwa ghali mno. Unaweza kupambana ukashinda, lakini gharama ya ushindi yaweza kuwa jamaa na marafiki wa wote uliowashinda watageuka kuwa maadui zako, yawezekana
watakuwa maadui kwako kwa muda mrefu tu. Watakukasirikia, watafanya yote nawe upate maumivu.
Hivyo, mwanadamu usifikiri tu gharama ya kushindwa, fikiri pia gharama ya ushindi. Na wakati mwingine, ni gharama inayostahili kulipwa. Franklin Roosevelt alikuwa Rais wa zamani wa Marekani. Alifahamu faida na hasara za kuwa na maadui. Waliompinga katika sera zake za kiuchumi aliwaita " Watiifu wa Kiuchumi" Na akasema; wamejiunga kwa pamoja kunichukia na nakaribisha chuki zao kwangu!
Kama unapigana vita ya muhimu, kama vita hivyo vyaweza vikawa vya kushinda (winnable). Na kwamba umejiandaa kulipa gharama ya chuki ya muda mrefu ya utakaowashinda, basi, ingia vitani, na kama la, tafuta suluhu au rudisha majeshi nyuma kimpangilio ( tactical retreat).
Swali ni hili; utafikiaje uamuzi wa ama kuingia vitani au la?
Miaka mingi iliyopita alitokea Mfalme wa Epilus aliyeitwa Pyrrhic. Mfalme huyu aliamua kuingia vitani kulikabili jeshi kubwa na lenye nguvu nyingi, ni jeshi la Warumi. Lakini kabla ya Mfalme kuingia baharini na vikosi vyake kuitafuta Italia ya Warumi, msaidizi wake wa karibu, Cineas, aliomba mazungumzo ya faragha na Mfalme. Alitaka kumwuliza maswali na kumshauri.
Cineas alimtamkia Mfalme; " E bwana Mfalme, Warumi wanasadikika kuwa na jeshi kubwa , lenye nguvu na lenye mashujaa wengi. Ndio maana wameteka nchi nyingi. Je, Mungu akitusaidia, tukaja kuwashinda Warumi,
tutafanya nini na ushindi wetu? Mfalme akajibu: " Mbona hilo ni swali jepesi sana. Mara ile tukiwashinda Warumi, hakutatokea jeshi kutoka mji wowote wa Italia litakaloweza kupambana nasi."
Cineas alitulia kidogo, kisha akamwuliza Mfalme: " Tukishaikamata Italia ya Warumi, kipi kitafuatia?"
Mfalme akajibu: Sicily ni kisiwa chenye hazina za thamani kubwa, itakuwa rahisi sana kukiteka kisiwa hicho."
Cineas aliendelea kuuliza: " Bwana Mfalme, unaongea juu ya mambo ya kusadikika, lakini una maana kukitwaa kisiwa cha Sicily kutakuwa na maana ya kukoma kwa vita?" Mfalme akajibu: "Hapo tutakuwa tumeikaribia Afrika. Na tukishaikamata Afrika ni nani hapa duniani atathubutu kutukabili kivita?" "Hakuna" Alijibu Cineas, kisha akauliza; " Na baada ya hapo tutafanya nini?"
Mpaka hapo Mfalme hakujua Cineas alikuwa anampeleka wapi kwa lojiki ya kifikra. Mfalme akajibu:
"Baada ya hapo, tutapumzika, tutakula raha. Tutakula na kunywa. Tutabaki tukichekeshana na kucheka, siku nzima."
Kama ni hivyo, alisema Cineas; " Ni kitu gani kinachotuzuia kufanya hayo yote sasa bila kwenda vitani?
Mfalme hakuielewa mantiki ya Cineas. Akakaidi ushauri. Akavipeleka vikosi vyake kupambana na Warumi. Baada ya vita ngumu, jeshi la mfalme liliwashinda Warumi. Hata hivyo, lilipata hasara kubwa ya kupoteza watu na kuwa na majeruhi wengi. Jeshi lake likadhohofika sana. Likajaribu kuitwaa Sparta, likashindwa vibaya sana. Mfalme aliwindwa na hatimaye akakakamatwa kama kuku na kuawa kwa kupigwa mawe kwenye mitaa ya Argos.
Isenga imbofu na isenga indenyeefu. Ng'ombe kipofu ni sawa tu na ng'ombe aliyevunjika mguu.
Na hilo ndilo ‘Neno Leo.'
Maggid,
Iringa.
Mimi pamoja na elimu yangu nimeisoma na kusoma na kusoma na bado sijamuelewa. Mwenye elimu inayopita yangu maana hapa tunazidiana anisaidie kuifahamu. Na ikiwezekana yeye Maggid afanye hivyo nisije potoshwa. Asante.