Neno La Leo: Afrika Viongozi Hawana Shukrani!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Viongozi Afrika hawana shukrani

Na Maggid Mjengwa,

HISTORIA ni mwalimu mzuri. Nimekumbushia hilo mara kwa mara. Kabla ya kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Winston Churchill alipata kuwa waziri wa masuala ya majini ( Marine Minister). Ilikuwa ni wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Winston Churchill ambaye pia alikuwa askari mwanamaji, aliacha ofisi yake na kuongoza vikosi vya wanamaji katika vita hivyo. Na hata baada ya vita kwisha, Churchill akafanywa kuwa ‘ Waziri wa Vita’ ( Defence Minister). Baadae, Winston Churchill akaja kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza.
Pamoja na ukweli, kuwa Winston Churchill aliiongoza vema Uingereza na hata kuweza kufanikisha ushindi katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia, bado, Waingereza hawakumchagua Winston Churchill katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1945. Inaweza kusemwa, kuwa wapiga kura wa Uingereza hawakuwa na shukrani. Kwamba wapiga kura wa Uingereza hawakumpima Churchill kwa historia bali kwa yatakayokuja. Kuna cha kujifunza, maana, Afrika kiongozi ukihangaika ukawajengengea watu wako barabara na madaraja, kuna shukrani watakazokupa. Afrika Rais anaweza kuitwa ' Rais wa Barabara, au Rais wa Maji' kama katika muda wake wa uongozi ameweza kuwasaidia watu wake katika kujenga barabara na kuwaletea maji. Wapiga kura Afrika wana shukrani, tatizo ni baadhi ya viongozi Afrika kukosa shukrani.

Ndio, nchi zetu kimsingi bado changa, na demokrasia zetu pia.

Maana, nchi nyingi katika bara letu hili la Afrika mwaka huu na mwakani zitatimiza miaka hamsini tangu kupata uhuru wake kutoka kwa wakoloni. Ni nusu karne. Ni muda mrefu. Yamkini shingo zetu wanadamu ni ndefu, lakini maisha yetu ni mafupi sana. Ndio, muda wetu wa kuishi humu duniani ni mfupi sana. Na historia itabaki kuwa hakimu kwa tunayoyafanya sasa.
Maana, wengi wetu tunaishi na kuziacha nchi zetu tulizozaliwa hata kabla hatujatimiza miaka 70 humu duniani. Lakini, nchi tulizozaliwa tunaziacha zikiwa na wanadamu wenzetu. Ni watoto wetu, ni wajukuu zetu. Na sisi Waafrika tumekuwa ni watu wabinafsi sana. Ni watu tunaoishi bila kufikiria sana ya kesho na kesho kutwa. Tunajiangalia sisi tu.
Sehemu kubwa ya matatizo ya nchi zetu hizi yanatokana na ubinafsi huo. Na bahati mbaya kabisa, baadhi ya viongozi tuliowapa dhamana za uongozi ndio wenye kuongoza kwa matendo yenye kutanguliza maslahi yao binafsi. Katiba za nchi zetu ni kielelezo halisi cha ubinafsi huo. Maana, wakoloni walitengeneza katiba ili ziwasaidie katika kututawala. Katiba ya mkoloni ilikuwa na maana moja kubwa; kuonyesha namna ya kuwatawala watu wa nchi iliyo mikononi mwa wakoloni. Na nchi zetu nyingi zimerithi misingi ya katiba hizo za kikoloni. Katiba nyingi za nchi za Kiafrika zinaonyesha namna ambavyo Waafrika wachache walio katika mamlaka ya Kiserikali watakavyowatawala “ Waafrika” wenzao! Na hilo ndilo ‘Neno La Leo’. Fikiri kwa bidii.
Maggid,
Kinondoni Biafra.
 
Maggid,

Article yako ina udhaifu mkubwa sana unapoanza kwa kichwa kuwa viongozi wa Afrika hawana shukurani halafu sehemu kubwa article inajumuisha kuwa waafrika wote ni wabinafsi na hivyo kuhalalisha ubinafsi wa viongozi wa Afrika. Usije kujinyonga kwa kuonyeshwa udhaifu huo. Tambua kuwa ubinfasi ni tabia ya binadamu wote, ila viongozi thabiti huweka sheria za kubana ubinafsi huo. Nyerere aliweka miiko ya uongozi kupitia Azimio lake la Arusha kuwabana viongozi wasiwe wabinafsi lakini Azimio hilo likabomolewa ili kuhalalisha ubinafsi wa viongozi; kwani Nyerere alikuwa mzungu? Marekani wana sheria thabiti sana za kuwabana viongozi wasijinufaishe kwa nafasi zao za uongozi lakini bado kuna wanaoshikwa kwa kukiuka sheria hizo na hivyo kufungwa miaka mingi jela.
 
Viongozi Afrika hawana shukrani

Na Maggid Mjengwa,

HISTORIA ni mwalimu mzuri. Nimekumbushia hilo mara kwa mara. Kabla ya kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Winston Churchill alipata kuwa waziri wa masuala ya majini ( Marine Minister). Ilikuwa ni wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Winston Churchill ambaye pia alikuwa askari mwanamaji, aliacha ofisi yake na kuongoza vikosi vya wanamaji katika vita hivyo. Na hata baada ya vita kwisha, Churchill akafanywa kuwa ' Waziri wa Vita' ( Defence Minister). Baadae, Winston Churchill akaja kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza.
Pamoja na ukweli, kuwa Winston Churchill aliiongoza vema Uingereza na hata kuweza kufanikisha ushindi katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia, bado, Waingereza hawakumchagua Winston Churchill katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1945. Inaweza kusemwa, kuwa wapiga kura wa Uingereza hawakuwa na shukrani. Kwamba wapiga kura wa Uingereza hawakumpima Churchill kwa historia bali kwa yatakayokuja. Kuna cha kujifunza, maana, Afrika kiongozi ukihangaika ukawajengengea watu wako barabara na madaraja, kuna shukrani watakazokupa. Afrika Rais anaweza kuitwa ' Rais wa Barabara, au Rais wa Maji' kama katika muda wake wa uongozi ameweza kuwasaidia watu wake katika kujenga barabara na kuwaletea maji. Wapiga kura Afrika wana shukrani, tatizo ni baadhi ya viongozi Afrika kukosa shukrani.

Ndio, nchi zetu kimsingi bado changa, na demokrasia zetu pia.

Maana, nchi nyingi katika bara letu hili la Afrika mwaka huu na mwakani zitatimiza miaka hamsini tangu kupata uhuru wake kutoka kwa wakoloni. Ni nusu karne. Ni muda mrefu. Yamkini shingo zetu wanadamu ni ndefu, lakini maisha yetu ni mafupi sana. Ndio, muda wetu wa kuishi humu duniani ni mfupi sana. Na historia itabaki kuwa hakimu kwa tunayoyafanya sasa.
Maana, wengi wetu tunaishi na kuziacha nchi zetu tulizozaliwa hata kabla hatujatimiza miaka 70 humu duniani. Lakini, nchi tulizozaliwa tunaziacha zikiwa na wanadamu wenzetu. Ni watoto wetu, ni wajukuu zetu. Na sisi Waafrika tumekuwa ni watu wabinafsi sana. Ni watu tunaoishi bila kufikiria sana ya kesho na kesho kutwa. Tunajiangalia sisi tu.
Sehemu kubwa ya matatizo ya nchi zetu hizi yanatokana na ubinafsi huo. Na bahati mbaya kabisa, baadhi ya viongozi tuliowapa dhamana za uongozi ndio wenye kuongoza kwa matendo yenye kutanguliza maslahi yao binafsi. Katiba za nchi zetu ni kielelezo halisi cha ubinafsi huo. Maana, wakoloni walitengeneza katiba ili ziwasaidie katika kututawala. Katiba ya mkoloni ilikuwa na maana moja kubwa; kuonyesha namna ya kuwatawala watu wa nchi iliyo mikononi mwa wakoloni. Na nchi zetu nyingi zimerithi misingi ya katiba hizo za kikoloni. Katiba nyingi za nchi za Kiafrika zinaonyesha namna ambavyo Waafrika wachache walio katika mamlaka ya Kiserikali watakavyowatawala " Waafrika" wenzao! Na hilo ndilo ‘Neno La Leo'. Fikiri kwa bidii.
Maggid,
Kinondoni Biafra.

HEADING yako inazungumzia viongozi lakini ndani ya habari yako unazungumzia waafrika kwa ujumla, na mimi nitawaongelea Binadamu kwa ujumla wao
ubinafsi ni Hulka ya Binadamu haijalishi rangi wala kabila
wazungu wa Zimbabwe walikuwa wabinafsi kwa kuchukua Ardhi kubwa yenye rutuba na kuwapa Waafrica ardhi ya mawe, Makaburu Africa kusini Waliwabagua waafrica kwa ubinafsi wao na kujifanya kuwa wao ni bora kuliko wengine, Zanzibar hapo Waarabu walikuwa wanawabagua Waafrika kwa ubinafsi wao wa kijiona wao ni bora kuliko Waafrica
ubinafsi ni hulka ya binadamu na hata maandiko matakatifu yanazungumzia hilo la "kumpenda jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe", hapa ina maana ya kutoa ubinafsi na umimi, SIAMINI KWAMBA NA WEWE (MAGGID) UMEKUWA BRAIN WASHED KIASI CHA KUJIDHARAU MWAFRIKA KWA KIASI HICHO
 
Ndugu zangu,
Kichuguu na Kituko ( Na majina yenu nayo ni ya vituko!)

Neno huzaa neno, yakawa maneno, na ndio maana ya ' Neno la Leo'. Msihangaike na heading, ni kichwa tu, yasemeni yaliyo mioyoni mwenu!
 
HEADING uliYoandika, haiendani na ulichoandika, UBINAFSI NI HULKA YA BINADAMU WOTE period
 
Maggid,
Ni kweli sio rahisi mtu kuelewa nini hasa ni mada katika tahariri yako. Para ya kwanza unazungumzia shukrani za wapiga kura hata hivyo humo umechanganya mambo nadriki kuita ovyo ovyo. Na nikupinge tu kuwa sijawahi kusikia rais anayeitwa rais wa barabara, au madaraja. Nitajie mmoja kama mfano. Hizo ni ideas zako tu na una sababu. Lakini pia si kweli kwamba mtu akifanya mema watu hawana shukrani. Huo ni uongo na narudia ni uongo.

Sasa ngoja tugeukie upande wa pili. Ubinafsi ni kitendo kinachotokana na ukosefu wa upendo tu.

Mtu asiye na upendo kwa wengine siku zote lazima ataishia kuwa mbinafsi. Lakini si kwamba waafrika wote hatuna upendo kwa wengine. Hapana. Tuna viongozi wetu waliozungukwa na watu wasio na upendo na hivyo kuwaambukiza hali hiyo ambayo si njema.

Mwenye upendo hujali wenzie. Uumia pamoja nao. Upata uchungu pamoja nao. Ulia nao. Uwapa kipaumbele wengine. Hana visasi kwa mahasimu wake. Huyo ndiye mwenye upendo. Na kwa kuwa ni kitu cha tunu wasicho nacho baadhi ya viongozi wetu wa kiafrika ndio sbabu tumefikia hapa tulipo.

Waafrika wengi tumejawa na upendo na ndio sababu tunaonewa vya kutosha na watawala na tumewavumilia tu.
 
Back
Top Bottom