Kaka, unajitahidi kuchanganya habari hapa! Mara unasema alipewa kama hisani mara zikaja share za 75-25%!Ile nyumba...ni...jasho la...marehemu Ikaeli Mbowe na alipewa tu kama heshima...na wala.sio fidia ya mchango wa yule.mzee kwa chama...cha TANU wakati wa kugombea...uhuru
Pia urafiki wake na mwalimu...ulitokana na mchango...kisiasa yule mzee hakua mwanasiasa lakini kutokana na uwezo kifedha alikuwa na ushawishi kilimanjaro na alimsaidia mwalimu kumkutanisha na.vijana ..waliomsaidia kueneza TANU...kanda yaa Kaskazini kama...mzee Kisumo, nsilo swai ,kaaya na eliufooo
Baada ya uhuru Mwalimu alimpa...mzee pale akafungua hoteli iliyokua na.vyumba na club ambayo...pia ilikua sehemu maarufu kwa..mawaziri kubarizi
Mzee yule hakua na wazo la.kuomba hati....hakua na wazo tofauti kwani yeye ,rupia ,sykes,aziz etc waliheshimika sana kama...Godfathers wa Tanu ...na wakridhika hawakuhitaji zaidi
Baada ya mzee...kufariki ndio...watoto walianza kuulizia hati na kwakua Mwalimu aliwapa kwa....mdomo ...alichoweza kufanya mzee Mwinyi ni kuwapatia kina freeman na wenzake( mbowe hotels ) 75% na NHC 25% ,which was good deal...pia kwakua tayari kulikua na..sheria ya kuruhusu ubia na NHC.
Kilichotokea ni kama...miaka ijayo watoto wa.JpM waje kunyanganywa nyumba mfano ya ada esate ya jpm aliyoipata akiwa waziri labda...kwa chuki za kisiasa kwa kuwa wataamua kufanya siasa za upinzani.....hivyo ndio watakavyojisikia
Kwa taarifa yako kuna orodha ndefu ya watu waliopewa nyumba kwa hiyo hiyo hisani toka awamu ya kwanza na ya pili kwa mfano Bibi Titi na wengine kibao, hadi leo hawana hiyo share ya 75-25% wala kulipa kodi NHC! Nyumba zao hazina chembe ya mgogoro hadi leo, chukua muda kidogo ufuatilie na utajua ukweli wa Bilicanas!
Mbowe amekuwa akilipa kodi miaka yote kwa 100% hadi pale alipoingia mkataba wa kuendeleza jengo kwa kuongeza ghorofa kadhaa ktk jengo hilo na makubaliano ilikuwa baada ya kujenga atakuwa na share ya 75% Mbowe hotels na 25% kwa NHC. Hakutekeleza makubaliano huku akisimama kulipa kodi na kudai ana share ya 75% na hicho ndiyo chanzo cha limbikizo la kodi yake hadi kufikia Tshs. 1.2 bilion.
Lakini nikukumbushe tu kwamba hapa DSM na mikoani kote kwa ujumla kuna nyumba nyingi sana zimebomolewa kupisha uendelezaji zikiwa na wakazi wengi na walipa kodi wazuri na zilibomolewa kabla na hata baada ya hiyo Billicanas, iweje tupoteze muda kujadili hili ambalo lilipelekwa mahakamani na likatolewa uamuzi akashindwa!