Neema zinazidi kunikimbilia, leo nimepata zaidi ya Tsh. 15m baada ya kuuza mpunga wangu

Bilionaire kekeman

Senior Member
Nov 26, 2022
142
823
Hakika riziki haupigi hodi kabisa, inakuja mbio mbio kabisa ila hii inakuja ukiwa na jitihada haiji tu eti upo zenu maskani kwenye kijiwe cha bangi unategemea utapa riziki? Hilo sahau kabisa aisee,nyie endeleeni tu kuvuta bangi na kupiga majungu, chuki na kuwasema vibaya waliofanikiwa

Nikuambie kitu pesa ipo kwenye kilimo naendelea kuwasanua ila kama kawaida mkiendelea na majungu mtajua wenyewe baada ya kupambana kununua mazao na kulima zao la mpunga nikaenda kupeleka sokoni kwa maana Kahama nikiwa na gunia zangu 167 za mpunga, basi bwana nikapeleka kahama na kila gunia nikauza 90,000 sikutaka kuuza kwa kilo niliona nitachelewa kwa sababu shambani nimeacha mahindi yangu, choroko, kunde na mengineyo.

Nikafika zangu pale Kagongwa Kahama kwenye maghala ya mpunga ile kufika tu nikakuta na tajiri mmoja mnyarwanda tukahesabu magunia na akaangalia sample na akaridhika nazo akanikatia cash zaidi ya milioni 15 zangu nikachomoka, hapa nilipo nipo miguu juu bijampora nakula bia.

Wenyeji wa Kahama karibu hapa bar ya Bijampora naangalia mechi huku nashushia bia na mtoto wa kinyarwanda karibuni.

Kilimo kinalipa vijana, acheni majungu tokeni maskani huko mkapambane! 😀😀😀😀
 
Hawana umakini pia wana wasiwasi
sana,Watasema chai wapuuze.

Nakazia, wafitini sana, wivu ulioboreshwa, wanachuki na uchoyo, watakutafutia hila wakisema hii ni chai.

Pia mioyo yao imedhaika, wanamakasiriko yasiyo na sababu,watakukasirika huku wakisema hii chai

Kwa vyovyote wana umri usiopungua miaka 48
 
Wamepote
Hawana umakini pia wana wasiwasi
sana,Watasema chai wapuuze.

Nakazia, wafitini sana, wivu ulioboreshwa, wanachuki na uchoyo, watakutafutia hila wakisema hii ni chai.

Pia mioyo yao imedhaika, wanamakasiriko yasiyo na sababu,watakukasirika huku wakisema hii chai

Kwa vyovyote wana umri usiopungua miaka 48
Za dira hao za maisha kwahiyo wivu unawasumbua
 
Back
Top Bottom