NECTA rudisheni utaratibu wa kutoa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na cha sita kwa majina kilichotokea si kigeni mitaani huku

Huu mfumo ni mzuri lazima privacy za watu zilindwe kwa gharama kubwa Sana .

Huu mchezo wa kusomea jina ulianza zamani na Muda huu umekomeshwa kwa kias Fulani.
Hakuna privacy kwenye kusoma privacy ya nini mmeona sitofahamu iliyojitokeza kwa privacy ambazo hazina msingi siri za kishamba mkeka utoke jina liwepo jamii ijue uzembe unaofanyika mbona zamani ilikuwa hivyo
 
Hakuna privacy kwenye kusoma privacy ya nini mmeona sitofahamu iliyojitokeza kwa privacy ambazo hazina msingi siri za kishamba mkeka utoke jina liwepo jamii ijue uzembe unaofanyika mbona zamani ilikuwa hivyo
We unaishi Zama za mawe
 
Lakini Mkuu! Selection ya kwenda A level au vyuo uwa inatoka kwa majina. Hivyo hii ya kwenda kuripoti kwa jina la mtu mwingine halitamalizwa kwa NECTA kutoa matokeo yanayoonesha majina. Labda ungeshauri hao wanaosahau majina yao kama huyo binti wawe wanagongwa muhuli wa jina lake kwenye paji la uso wake!
Boss shukuru mungu kama upo kwenye jamii inayojua kutafuta tarifa, kuna wazazi wapo mjini kabisa hawalewi lolote zaidi ya kutafuta pesa ya kukidhi mahitaji ya familia

Pili watoto wanao danganya wazazi wengi hawasemi wamepata ufauru wa selection kwenda kidato cha tano au kwenda vyuo vya kati wao wanadanganya ufauru kuanzia ufauru wa D nne na wengine wanase,a wamesahau kabisa number kwakua mzazi alimpeleka mtoto shule kutimiza wajibu wa sheria asiitwe ofisi za kata nk anapotezea yani ni majanga
 
Kuna kijana wa jamaa yangu wa karibu kafanya kama unavyosema lakini yeye alipata matokeo mazuri ya kwenda CO lakini alipo kwenda chuo alisoma mwaka mmoja tu baada ya hapo akaachilia mbali chuo lakini akawa anaendelea kupewa ada na huduma zote zinazohusu chuo na wazazi wake mwisho wa siku miaka mitatu ilipoisha wazazi wanamwambia wamwombee ajira kwenye private sector alete vyeti anakodoa macho. Mzazi akaamua afuatilie kule chuoni alipo fika alichoambiwa alimpigia cm mkewe akiwa huko huko chuo na kumueleza akifika pale nyumbani asimkute yule mtoto wasije wakagawana majengo ya serikali. Kijana kakimbilia kwa wajomba xake
Kiongozi hilo ni janga kuna wazazi wengi sana wanajua watoto wao wamehitimu vyuo ila kiukweli hakuna kitu na wapo na vyeti majumbani na kwa vile sasa ajira zimekuwa ngumu ndio njia hiyo wapo kusumbua wazazi wapewe mitaji
 
🤣🤣🤣🤣 tatizo lilianzia pale mtoto wa KIKWETE alipofeli alipata div 4 ,FFFFFFFFF
Kikwete ishi maisha marefu sana baba, kuna maskini huku kama hawakukusema wewe hawapati usingizi kabisa kabisa. Wakishakusema tu basi wenyewe wanajisikia amaaaani na husahau njaa zao kwa muda🤣🤣🤣🤣
 
Usiri wa nini? Mambo ya Elimu hayapaswi kuwa siri. Mtu kama kafaulu vizuri ajulikane na kama amefeli watu wajue mnaweka siri kwa watoto ili iweje?
Ila hata kwa nchi zilizoendelea matokeo huwa ni siri...

Ndiyo maana mpaka leo Hata marekani Hakuna anayejua matokeo ya Trump Shuleni mpaka anamaliza University..

Hata ya Obama hajayaweka wazi...
 
Ila hata kwa nchi zilizoendelea matokeo huwa ni siri...

Ndiyo maana mpaka leo Hata marekani Hakuna anayejua matokeo ya Trump Shuleni mpaka anamaliza University..

Hata ya Obama hajayaweka wazi...
Wao acha waweke siri kwani ndio utaratibu wao tangu awali.

Mimi nimeuliza kwanini iwe siri nipe sababu za kuficha matokeo hao US achana nao hatuwezi kuiga kila kitu.
 
Ila hata kwa nchi zilizoendelea matokeo huwa ni siri...

Ndiyo maana mpaka leo Hata marekani Hakuna anayejua matokeo ya Trump Shuleni mpaka anamaliza University..

Hata ya Obama hajayaweka wazi...
mambo yaende kiafrika zaidi hatujakua na wakina trump hawa watoto wanakua wapumbavu siku hizi mashuleni kidogo kuweka majina kutawachangamsha
 
Mfumo uko sawa na serikal haiwez badili mfumo kisa watoto wajinga wachache na wazazi wasio makin na elimu za watoto wai
Km mzazi yuko makini na elimu ya mwanae kamwe hawezi danganywa kirahis ivyo tena kwa mda mrefu km unavyeleza apo
 
Kisheria na kiutaratibu matokeo ni Kwa ajili ya aliyefanya mtihani sio Public.

Siungi mkono matokeo kutolewa Kwa majina, Hata Kama zamani walitoa Kwa majina Hilo halihalalishi kuwa ni sahihi.

Jukumu la kuona matokeo ni Kwa aliyefanya mtihani pekee. Awadanganye wazazi wake au laah!! Hiyo ni kesi nyingine.
 
Yawekwe majina ili iweje izo ni siri za watu ndo maana wanapewa kila mtu code number yake ndo maana majibu ya form 4 na 6 wanaweka code ila form2 sio dili saana maana ni mitihani rahisi sana ndo maana kuna majina
 
Suala ambalo limejitokeza wiki hii mwanafunzi kungangania namba ya mtihani ambayo si yake na kusema ni yake si geni kwenye jamii zetu, wazazi ambao si waelewa sana wanadanganywa sana na watoto zao pale matokeo yanapotoka hasa mwanafunzi akiferi wengi huchukua namba za wenzao na kusema ni namba zao wanafunzi wengine hudanganya wazazi wamesahau namba wengine huenda mbali na kusema wamefauru kwa kupata arama zinazomuwezesha kwenda chuo cha kati.

Hivyo wazazi wanaingia gharama kutoa pesa mtoto aende chuo kijana anapanda gari anafika chuo husika anapanga gheto anakuwa asomi anaishi kubet, kunywa pombe, na kuomba pesa kwa wazazi za matumizi yani kijana anadanganya miaka hata sita kuwa yupo chuo wazazi wanatuma pesa nk mwisho wa siku wazazi wanagundua ni uongo wanaishia kulalamika tu ila chanzo nini hawakujua matokeo ya mtoto wao kidato cha nne kwani yalitoka kwa namba nao uelewa mdogo.

Kwahiyo toeni kwa majina ili iwe vyepesi hata majirani kujua mtoto wa bwana kipara matata kafauru au kaferi, leo hii kuna wazazi wengi wanamini vijana wao wapo vyuo wanasoma au wamehitimu astashahada furani kumbe ni invalid wana vyeti vya stationary wana matokeo ya stationary wanakuja umbuka hawataki kazi wanasumbua wazazi wawape mitaji wajiajiri lengo wasijulikane kama waliferi na wana vyeti feki.

Wito wangu NECTA rudisheni utaratibu wa zamani matokeo ya kidato cha nene na kidato cha sita toeni kwa majina kama aibu iwe sawa tusiogope kwanza hii inaweza saidia wanafunzi jituma maana akiferi atanikwa hii kuficha ficha ni tatizo kwanza kuferi si ugonjwa weekeni mambo hadharani.

Mbona matokeo ya upimaji kidato cha pili, darasa la nne na matokeo ya mtihani wa darasa la saba mnatoa matokeo kwa jina la mtahiniwa kwanini kidato cha nne na kidato cha sita mnatoa kwa number pekee wekeni mambo hadharani wajomba wanatudanganya sana anapata zero anakwambia amepata division four ya 28 anakusumbua umpe mtaji ataki shule, ukimwambia nenda VETA ataki at the end anataka umnunulie bodaboda yani ni shida juu ya shida NECTA tueleweni.
NECTA ni majitu ya ajabu sana. Kwanini wanafichaficha matokeo kama vile matokeo ni bangi au dawa nyingingine za kulevya? Haya matatizo yote yanayopelekea wazazi kudanganywa na wanafunzi kuteseka yanasababishwa na umbumbumbu wa NECTA kuficha matokeo kwenye namba za mtihani badala ya kutoa jina la mtahiniwa. Ni aibu kubwa sana kwa taifa.
 
Bado nchi ina wazazi wapumbavu sana. Mzazi hufuatilii mtoto wako unataka nani afuatilie? Acheni ujinga aisee. Mzazi makini anatakiwa afanye ziara za kushtukiza anakosoma mwanae. Namshukuru baba yangu kunikalia kooni nisifanye biashara wakati niko chuo. Alihakikisha namaliza chuo kwanza ndo nifanye biashara. Huenda nisingemaliza chuo. Kuna mzee jirani yetu alikuwa kila siku asubuhi lazima aende na mwanae mguu kwa mguu hadi shuleni wakati mwanae akiwa kidato cha nne. Yule dogo alikuwa anaishia mitaani kwa wavuta bangi shule haendi. Mzee aliingilia kati na kujitoa mhanga hadi mwanae alimaliza form four na kupata Div IV.
 
Back
Top Bottom