NEC CCM: Sitta In Lowassa and Rostam Out

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
NYOTA ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, imeendelea kung’ara baada ya wabunge wa CCM kumchagua kwa kura 104 awawakilishe kwenye Halmashauri Kuu ya chama hicho (Nec).

Katiba ya CCM inaruhusu wabunge wa chama hicho kuwachagua wajumbe 10 kuingia Nec kutoka miongoni mwao.

Walioingia:
Livingstone Lusinde(Mtera), Nimrod Mkono (Musoma Vijijini), Abbas Mtemvu (Temeke) , Hawa Ghasia. Wabunge wa Viti Maalumu, Angela Kairuki, Munde Tambwe na Faida Mohamed Bakari, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba.

Wabunge walioanguka
Brigedia Jenerali Mstaafu, Hassan Ngwilizi (Mlalo), Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Dk Athman Mfutakamba, , Dk Charles Tizeba (Buchosa), Christopher Ole Sendeka (Simanjiro).

Wengine ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, , Dk Faustine Ndungulile (Kigamboni), , Ahmed Salum Ali (Solwa), , Yahya Kassim Issa (Chwaka), Mwanahamisi Kassim Saidi (Viti Maalumu), Martha Mlata (Viti Maalumu) na Saidi Mussa Zubeir (Fuoni).

Waliojitoa kabla ya kura kupigwa
Dk Harrison Mwakyembe(kyela), Dk Hamis Kigwangallah (Nzega), Lediana Mg’ong’o (Viti Maalumu), Naibu Spika, Job Ndugai na Mbunge wa Uzini, Muhammed Seif Khatib.

Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM ni Jenister Mhagama
Mwenyekiti wa kamati hiyo ya wabunge wa CCM ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
 
Wewe Quinine mbona hao kina EL na RA mbona wanaonekana kwenye kichwa cha habari tu? kwanini kama wameanguka majina yao hayaonekani katika orodha ya walioanguka au waliojitoa?
 
Wewe Quinine mbona hao kina EL na RA mbona wanaonekana kwenye kichwa cha habari tu? kwanini kama wameanguka majina yao hayaonekani katika orodha ya walioanguka au waliojitoa?
Ulitaka nisiwataje, nimewataja makusudi kwa sababu ni mahasimu wakubwa wa Six walitaka Six anyang'anywe kadi asiwemo Nec sasa imekuwa kinyume chake.
 
lowassa na rostam ni wajumbe wa nec ulitaka wachaguliwe mara ya pili. inatkiwa wafukuzwe huko wapewe wengine.

wengine wamepata kura ngapi.
 
heading mbona hakina maana...EL na Rostam hawakugombea sasa unasemaje out...ushabiki mwingine bana
 
Walioingia:
Livingstone Lusinde(Mtera), Nimrod Mkono (Musoma Vijijini), Abbas Mtemvu (Temeke) , Hawa Ghasia. Wabunge wa Viti Maalumu, Angela Kairuki, Munde Tambwe na Faida Mohamed Bakari, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba.
.

Gamba namba Sita(NM), Huyu ni defending midfielder, kwenye ile first eleven ya CCM.
Bila yeye attacking midfielder gamba namba nane (RA) halishwi, na playmaker (EL)gamba namba 9 hatoi pasi.
Kuna winga wa kulia hatari sana, anapanda na kushuka na krosi zake goli, gamba namba saba (NK).

Hii ndo timu nzima: Orodha ya Mafisadi (List of Shame)
 
Yaaani mnaaamini kabisa kwamba EL na RA hawamo?
Tena kuto onekana kwao kwenye list ndo kuna wapa nguvu zaidi,.....
Wana kiburi cha pesa hao,which will make them drive/take control of nec and ccm at large
 
Back
Top Bottom