Nothing4good
Senior Member
- Feb 19, 2011
- 180
- 55
Kuna ndugu yangu kaniomba ushauri naomba munisaidie. Huyu ni msichana mwenye miaka 22 sasa ameolewa miaka 4 iliyopita tatizo lake nikwamba mumewe kamwambia akakae kwao mpaka atakapomuhitaji ataenda kumchukua. Ni hivi huyu dada alifahamiana na huyu kaka akiwa 4m two na waliendelea na mahusiano yao mpaka alipomaliza 4m 4 ndipo wakaoana. Walifanya bonge la harusi ya kikatoliki halafu huyu kaka anafanya kazi nje ya nchi. Kila baada ya miezi mita2 huwa anarudi kumjulia hali mkewe anakaa siku mbili ta2 then anarudi kazini. Akamfungulia mkewe stationary awe anaiendesha. Cha kushangaza baada ya mwaka akamwambie mkewe asiende kuwatembelea ndugu zake (mwanaume) mkewe akauliza kwanini? Akajibiwa nimekuambia usiende full stop. Sasa bahati mbaya kukatokea msiba akaamua kwenda halafu atamuelewesha mumewe. Akiwa huko mumewe akampigia simu akamwambia ukitoka huko nenda kwenu lakini alipotoka huko akarudi kwake basi hayo yakaisha. Baada ya kama mwaka akapata mimba kwa bahati mbaya mimba ikatoka. Kumwambia mumewe kuwa mimba imetoka mume wake akawa anamwita muhuni sana wewe mwanamke umetoa mimba yangu baada ya ya hapo mumewe akamwambia kuanzia leo sitak uende stationary tena nimeshatafuta m2 wa kusimamia na hiyo kadi yako ya bank mpelekee mama yangu maskini dada wawa2 akafanya kama alivyoambiwa baada ya muda mume wake akamwambia nenda kwenu nikirud nitakuja kukuchukua bint akaenda. mumewe aliporud hakwenda kumchukua alienda mpaka kijijini kwao na kurudi na m2 anayedai ni mamdogo wake akamwambia huyo mamdogo asafishe chumba baada ya hapo akampigia simu mkewe na kumwambia wewe ni mshirikina imekutwa hilizi ufunguni mwakitanda. Sasa huyu dada anaomba ushaur afanye nini na alikuwa na wadogo zake wawili aliokua akiwasomesha kupitia biashara yake ya stationary? Wazazi wake hawana uwezo na yeye ndo mtoto wakwanza. Msaidien tafadhali