Melki the Storyteller
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 5,701
- 9,779
Habari wana JF, ni mimi hapa nguli wa mapenzi, a.k.a mzee wa ovyo, hapa kitaani ukiulizia nyumbani kwa mzee wa matikiti kudondokeana unaletwa hapa mlangoni kwangu
Basi bhana, miezi miwili iliyopita nalisikia sauti kali mithili ya malaika wa peponi ikichomoza kutoka bustanini mida ya alfajiri. Hakuwa mwingine, bali mwanangu wa kiume ambaye ni mhitimu kidato cha nne. Japo nilivutiwa na kipaji chake, nilimkaripia vikali huku nikimtaka aandae akili yake akasome Pre Form Five
Mwanangu hana imani kabisa na elimu ya Tanzania. Ni vile tu baba yake sina pesa ya kumpeleka nchi ya nje. Hivyo anaamini katika kile kitu alichonacho kumkichwa. Ili kuthibisha hilo, nalisikia wimbo wake kwenye bars za sebureni kwangu ambazo huwa nazitumia kupigia nyimbo za urabu
Vipi wana JF, nimuendeleze kipaji chake ama niachane nacho? Kisije kuwa hakina manufaa kama elimu ya vyuo vikuu nikajutia!