Ndugu wa mume ndiyo hawa au kuna kitu nakosea?

Pole sana mamii90 samahani kama nitakurudisha nyuma kwa maswali yangu ila majibu yanaweza kutoa picha ya wewe ni nani ndani ya hiyo nyumba maana kwa maelezo uliyotoa siioni nafasi yako kama mke
Mumeo ana umri gani? Ndoa yenu ilianzia kwenye misingi ya upendo au mlioana kwa sababu zingine tuu? Utaratibu wenu wa mipango ya maisha ukoje, mnashirikishana kwenye maamuzi? Je wewe na mumeo mnafanya kazi? na utaratibu wa matumizi ya mapato yenu upoje?
Kuna mambo siwezi saana kuyaongelea kwa maandishi ni mengi
Ila tulipendana na huyu jamaa mwanzo kiasi kwamba tulikua tunakesha kuchati na kuzungumza kwenda sehemu mbalimbali na mambo kama hayo
Ugomvi mkubwa kuwahi kuyokea baina yangu na yeye ni ndugu
Na kucheat nishawahi komfem kafanya hivyo ila hakukua na ugomvi wowote nilosamehe baada ya yeye kunidangamya danganya juu ya hiyo scenario.
Baadhi ya maamuzi ndio ila sio yote haswa yakiwa yanalink na familia yake
Wote tunafanya kazi ila sijui mshahara wake shingapi
 
Umasikini ni tatizo kubwa sana. Namshukuru Mungu nilipotokea wanajiweza hivyo hawawezi niomba msaada wowote ule. Na twaishi mkoa mmoja hivyo hawawezi kuja lala kwangu
 
Pole sana mamii90 samahani kama nitakurudisha nyuma kwa maswali yangu ila majibu yanaweza kutoa picha ya wewe ni nani ndani ya hiyo nyumba maana kwa maelezo uliyotoa siioni nafasi yako kama mke
Mumeo ana umri gani? Ndoa yenu ilianzia kwenye misingi ya upendo au mlioana kwa sababu zingine tuu? Utaratibu wenu wa mipango ya maisha ukoje, mnashirikishana kwenye maamuzi? Je wewe na mumeo mnafanya kazi? na utaratibu wa matumizi ya mapato yenu upoje?
Umri kanizidi 10yrs
Ndoa inaenda mwaka wa 3 bila break ya amani
 
Acha kushauri na kutetea ujinga. Hao unawaita mawifi wakatafute miji yao.
Mi sitaendekeza huo ujinga na uzuri wote wanajua misimamo yetu hakuna mtu anayejiita wifi anayeingilia miji yetu
Anaongea maana hajawahi jikuta katika hiyo hali.
 
Nilishawahi kumwambia kwamba namna ambavyo achukui hatua yoyote kwa ndugu zake ndo anawaongezea mabawa ya kufanya kila wajisikialo
Akasema maneno yatakua mengi ukweni na yeye akiongea.

Nikisema nimwambie mama mkwe.
Nakumbuka kuna kipindi mr kasafiri alivyorudi niligundua hali flani ya usali(sitaelezea ilikuaje) ila nilidhibitisha ananicheat so nikaongea na mama ake. MAMA AKE AKASEMA AKIWA ANASAFIRI MFUNGASHIE CONDOM
duhhh huyo mama alisema hivi kwa mdomo?
 
Tatizo mkishaahidiwa ndoa basi akili mnaweka rehani hamna muda wa kuchunguza background ya familia unayoenda kuungana nayo,kuna familia zina malezi ya kipumbavu sana hata mtoto wao wa kiume asipojitambua hatakaa ajenge familia,mumeo kinachomsumbua ni aina ya malezi ya familia yake na bado hajitambui,angekuwa anajitambua angesimama kama mwanaume kutetea familia yake,mke na watoto wangu ni sehemu ya maisha yangu lazima nivitetee kwa nguvu zote hasa ninapohisi kuna uonevu.Tumia watu wenye busara waongee na mumeo.
 
pole sana dada bt tambua hakuna maisha bila changamoto...
situation unayopitia huwatesa sana wadada wengi hasa ukikuta mume hayupo upande wao....
ichukulie situation hiyo kua sehem ya maisha yako then jifanye mjinga na uzuie hasira ili utengeneze urafiki na mumeo mpaka atakapokua upande wako, pia fanya maombi ili mume awe upande wako nadhan ukifanya hivo mwez1 tu utaona mabadiliko
Nashukuru dear
 
Pole sana Dada, lakin inaonyesha ni kama vile wewe ndo uliforce au uliweka nguvu nyingi sana ili akuoe, piga picha kuanzia pale kwenye harakati za ndoa visa vya ajabu ajabu tu walikufanyia ndugu zake.

Nahis familia nzima hawakupenda ndugu yao akuoe ndo maana. Ila vumilia tu jipe moyo siku moja wataondoka hawataishi kwako milele,
Upo sahihi.
Ila huyu binti ndo chanzo maana yeye ndo alinijua kabla ya mtu yoyote.ikawa kama naishi na mama mkwe kila linalofanyika linaripotiwa yaani
 
Ndugu pole.. wewe unafanana na mm kidogo. Mm Kuna mtoto wa shemeji yangu naakaa nae sawa ananisaidia kazi zote. Swala linakuja mume wangu anamjali kuliko hata mm. Kidogo tu atamuulizia amekula Mara mumeenda wote kanisan Mara amelala. Kila siku anampa ela. Khaa nilibidi nikwambie tu. Naona anapunguza kidogo
 
Pole mnooo, tukiwa tunaamini kwamba mke ndie msaidizi wa mume basi mume anatakiwa kumpa ulinzi mkewe.
Hapawezi kuwa na familia yenye baba na mama halafu watoto na ndugu wanakua na maamuzi yao jinsi ya kuendesha maisha ndani ya hiyo nyumba lakini nje ya mfumo uliopangwa na wenye yaani mume na mke
Hata kama mwanamke anakosea mahali ni kazi ya mume kuongea na private na kuweka mambo sawa na sio kuonyesha kwamba anaungana na wanaomchukia mke
Utanisamehe ila ninachoona hapa huyu mwanaume ambae tunasema nyie ni mwili mmoja hakupendi, hakuhitaji wala huna thamani kwake. Kama familia haiwezi kusimamia hili rudi kule mlikofungia ndoa kwa ushauri
Sijawahi kwenda poppte zaidi ya kumueleza mama yake ila natamani sana kuongea na mchungaji ila naogopa kumkera
 
Tatizo mkishaahidiwa ndoa basi akili mnaweka rehani hamna muda wa kuchunguza background ya familia unayoenda kuungana nayo,kuna familia zina malezi ya kipumbavu sana hata mtoto wao wa kiume asipojitambua hatakaa ajenge familia,mumeo kinachomsumbua ni aina ya malezi ya familia yake na bado hajitambui,angekuwa anajitambua angesimama kama mwanaume kutetea familia yake,mke na watoto wangu ni sehemu ya maisha yangu lazima nivitetee kwa nguvu zote hasa ninapohisi kuna uonevu.Tumia watu wenye busara waongee na mumeo.
Nishafikiri kufanya hivyo sasa hivi nahisi kufanya hivyo
 
Pole sana! Ukipata nafasi mtafute mtu anaitwa Irene Mbowe nimeona akisaidia wengi sana na wengine wana case ngumu zaidi ya hiyo! na uzuri ushauri wake uko kiimani pia!
 
Ndugu pole.. wewe unafanana na mm kidogo. Mm Kuna mtoto wa shemeji yangu naakaa nae sawa ananisaidia kazi zote. Swala linakuja mume wangu anamjali kuliko hata mm. Kidogo tu atamuulizia amekula Mara mumeenda wote kanisan Mara amelala. Kila siku anampa ela. Khaa nilibidi nikwambie tu. Naona anapunguza kidogo
Bora huyo anakusaidia hata mimi ningempa mapenzi yoote
 
Wanawake wengi huwa ni wagumu kutoka kwenye ndoa jamani, yani kuna kaka mmoja anaitwa iddmakengo huko instagram ni mshauri wa mambo ya ndoa na mahusiano, huwa nasoma visa vinavyoletwa mule mpaka nabaki kujiuliza hivi haya ninayoyasoma kwa wenzangu tupo dunia moja au dunia tofauti, vingine ni scary movie kabisa, lakini still mtu hayuko tayari kutoka, anaomba ashauriwe jinsi ya kuendelea kuvumilia akitegemea kuna muujiza wa kumbadilisha huyo mwanaume. Anyway back to you my dear, looh natamani kujua huyo baby mama wa kwanza aliachwa vipi, nini kilitokea, ulikutana vp na huyo mwanaume na alikuaje kipindi cha mahusiano mpaka mnaingia kwenye ndoa, mana nahisi red flag zilikuwepo toka zamani ila ulizii ignore tena sio za mumeo tu hata za ndugu. Ila kiufupi mumeo ndo tatizo kwenye ndoa yenu, hao ndugu wasingekuwa na ubavu wa kufanya hayo wanayokufanyia kama mumeo angekuheshimisha. Trust me heshima ya mke kwa ndugu wa mume inategemea mumeo anaku treat vp. Mumeo anakudharau, hakuheshim, na hata kukupenda i dnt think kama anakupenda may be but not that much, mana upendo ndo huzaa mazuri yote kwenye ndoa. Hao ndugu wako hivyo kwasababu wanajua kwamba wewe hata kwa ndugu yao huna thamani mana si mara moja umeshawashtakia lakini anakuwa upande wao, its like amewapa go ahead kufanya watakavyo, and he doenst care means uwepo wako kwake hauna uzito wowote, so anachomaanisha ni kwamba ukitaka kaa ukitaka ondoka. Kazi unayo. Pole. Kuna mtu amekushauri huko juu uanze kujiengenezea maisha fanya hivyo haraka, mana unaweza kuzani kifo ndo kitakutenganisha nae unyang'anywe hadi vijiko but TRUST me kifo kinaweza kisije kuwa sababu ya wewe kutolewa humo ndani.
Mama alinishauri sana kabla sijafunga ndo niwe makini na mtu ambae atanioa ila pamoja ns kuona viashiria vingiii tu ila nilisema labda uenda huko mbele mambo yatabadilika
 
Pole sana jamani!

Wewe na dada mnatosha kabisaa kufanya majukumu yenu mkamaliza na mkalala mchana bila hata kugombana na hao ndugu!!

Wajifulie wenyewe, hayo mengine fanyeni!! Chakula ukipika pika cha familia nzima dear! Usikose amani kwenye ndoa yako sababu ya wapita njia!!

Ukiona unakereka mchukue mwanao na dada nendeni mahali kaeni kunywa juice, mtoto abembee jioni mrudi!! Hayo makwazo ni kupotezea tuu dear!! Ongea na mwenza wako vizuri, usiwape nafasi ya kukugombamisha naye dear!!!

Siku zote furaha yako iko mikononi mwako mamii, wewe ni mama mwenye nyumba simamia vyema amani ya familia yako!!
Sakayo kuna kipengengele sijakifanya muda saaana.
Asante yaani kila weekend nitakua natoka na dada na mwanangu maana ndo furaha yangu pekee.
Alafu mimi msichana wa kazi nikimuondoaga huwa anangangania hataki kuondoka maana ki ukweli hao viumbe nawaheshimu maana anaweza hata akakuokoa maana kwa situation yangu ya hawa ndugu hawashindwi nifanya lolote akaniokoa dada
 
Mpendwa
Pole kwa unayopitia,
Naomba kujua maswala mawili ambayo hujayaweka wazi sana
Je huyo mwana mke aliezaa na mumeo mahusiano yao yalidumu kwa muda gani na ilikua ni baada ya ndoa yenu au labla?
Na sababu ya kuachana nae ilikua nini?

Pili, wewe na mumeo mlikutana mkapendana wenyewe au mlilazimishwa na wazazi?

Cha kukushauri, kweli huwa tunaolewa kwenye familia za watu na tunakutana na ndugu wenyw tabia tofauti, cha msingi ni kutumia busara kuliko kutumia nguvu au hasira

Jaribu kutafuta better moment, ongea na mumeo, ikiwezekana hao ndugu muwatafutie shughuli ya kufanya ili waweze kujitegemea badala ya kuwategemea nyinyi

Msipofanya hivyo, hamuwezi kutatua mgogoro uliopo kati yenu na ndoa yenu haitapata amani

Usichukue hasira, enedelea na majukumu yako kama mke, wapikie wakaribishe chakula, ondoa vyombo, maana hapo ni kwako.

Jaribu kuepuka mambo ambayo yataleta ugomvi kati ya mumeo na nduguze

Ila tafuta muda uongee na mumeo hao ndugu wapate cha kufanya ila na nyinyi mpate nafasi ya kufanya maisha yenu

Mumeo ana makosa makubwa na inawezekana kuna mengi nyuma ya pazia yanaendelea kati ya mumeo na nduguze, pengine mumeo bado ana mahusianonna huyo mwanamke alise zaa nae na ndugu wapo upande wake, jaribu kuchunguza na uwe makini katika kila step

All in all mahusiano yakisha fika stage hiyo, mkiona mmeshindwa kuzungumza mkaelewana, watafute watu wa karibu yenu, ikiwezekana hata marafiki ambao wana hekima, wajaribu kuzungumza na mumeo kujua shida ipi wapi
Asante...nitajaribu kufikiria swala la kutafuta watu wa kuzungumza nae
 
Back
Top Bottom