Ndugu Shemsa Mohammed Aongoza Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM Wilaya ya Meatu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943

NDUGU SHEMSA MOHAMMED AONGOZA KAMATI YA SIASA MKOA WA SIMIYU KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM WILAYA YA MEATU

Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Simiyu chini ya Mwenyekiti wake ndugu Shemsa Seif Mohammed tarehe 22/11/2023 imeendelea na ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2020/2025 ndani ya Mkoa wa Simiyu, Wilaya ya Meatu, Jimbo la Meatu

Katika Jimbo la Meatu jumla ya Miradi 6 yenye thamani ya bilion 10.829 iliyotolewa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mwenyekiti wa CCM ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imekaguliwa.

Miradi hiyo ni pamoja na;
1. Utafiti wa Maji, Uchimbaji wa kisima na Bwawa kata ya Bukundi, Kijiji Cha Lukale iliyogharimu Tsh. 60,000,000/=

2. Ujenzi wa Matundu 10 ya Vyoo Shule ya Msingi Kasala iliyogharimu Tsh.11,000,000/=

3. Mradi wa kupeleka Umeme Vijijini (REA) III R2, Kijiji Cha Lukale iliyogharimu Tsh. 1,167,703,951/=

4. Ujenzi wa Daraja la Itembe iliyogharimu Tsh. 8,400,000,000/=

5. Ujenzi wa Lami Mwanhuzi Km 1.25 na Taa zinazotumia Nishati ya Jua yenye thamani ya *Tsh 999,303,450/= na

6. Matengenezo ya Barabara ya Rest House - Mwanzagamba iliyogharimu Tsh. 190,451,580/=

Hata hivyo, Kamati ya Siasa ya Mkoa Simiyu imeridhishwa kwa kiasi kikubwa na Utekelezaji wa Miradi hiyo

WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.53.15(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.53.14.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.53.15.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.53.15.jpeg
    178.7 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.53.15(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.53.15(2).jpeg
    179.9 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.53.15(3).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.53.15(3).jpeg
    192.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.53.17.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.53.17.jpeg
    254.1 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.53.16(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.53.16(1).jpeg
    198.8 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.53.16.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-23 at 15.53.16.jpeg
    217.8 KB · Views: 5
Back
Top Bottom