Ndugai: Wananchi na Wanasiasa tutekeleze wajibu wetu kwanza kabla ya kuhoji wajibu wa Serikali

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Habari!

Spika wa Bunge aliyejiuzulu Kwa kusema Nchi itapigwa mnada Kwa sababu ya Madeni,amewataka Wananchi na Wanasiasa na jamii kiujumla kutumiza Wajibu wao Kila mtu Kwa nafasi yake ndio Wahoji Wajibu wa Serikali kwao.

Ndugai ametoa angalizo Hilo huku Vyama vya upinzani vikijiandaa Kwa Mikutani ya Hadhara Wikendi hii na vinatarajia Kuhoji mambo mbalimbali ya utendaji wa Serikali..

Swali,Je Ndugai kaona nini? Kwa nini atoe angalizo Hilo Sasa?

-----

Spika wa Bunge Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai ametoa wito kwa kila mwananchi kutekeleza wajibu wake katika kukuza maendeleo ya nchi badala ya kuiachia Serikali pekee yake.

Ndugai ameyasema hayo wakati akishirki mkutano wa kuutangazia umma mafanikio ya miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Sita katika mkoa wa Dodoma.

“Yako majukumu ya mtu binafsi, ya familia, ya jamii iliyoko pale ambayo hayo nayo yakifanyika, sasa yakiungana na yale ya Serikali ndio kinachoitwa maendeleo,” amesema.

Aidha, Ndugai ameeleza kuwa kila mmoja ana haki kikatiba na sababu ya kuhoji kinachofanywa na Serikali lakini pia wananchi wana wajibu wa kutekeleza majukumu yao kwa kufanya shughuli za kiuchumi ili kuisaidia Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Twendeni tukafanye shughuli za kiuchumi ni jukumu letu tukafuge kwa kadri tunavyoweza, Serikali kwa sababu ni baba na mama atatusaida majosho, kwa sababu siyo kila mtu ataweza kujenga josho lake, atatusaidia baadhi ya madawa na huduma nyingine za ugani,” ameeleza.
 
Habari!

Spika wa Bunge aliyejiuzulu Kwa kusema Nchi itapigwa mnada Kwa sababu ya Madeni,amewataka Wananchi na Wanasiasa na jamii kiujumla kutumiza Wajibu wao Kila mtu Kwa nafasi yake ndio Wahoji Wajibu wa Serikali kwao.

Ndugai ametoa angalizo Hilo huku Vyama vya upinzani vikijiandaa Kwa Mikutani ya Hadhara Wikendi hii na vinatarajia Kuhoji mambo mbalimbali ya utendaji wa Serikali..

Swali,Je Ndugai kaona nini? Kwa nini atoe angalizo Hilo Sasa?

Yaani Ndungai hataki tukaihoji Serikali hata katika kukopakopa kila mara ?!! Mbona anatuchanganya ?! Yeye mbona aliihoji wakati ule ?!! Kwahiyo kumbe anakiri alikosea sana !!!
 
Back
Top Bottom