Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,607
- 51,519
Mwalimu alishalionya Taifa, kuwa ukiona kuna watu wanapita na kupiga kampeni za kumtaka raisi aongezewe muda, kimsingi wanakuwa wanapigania matumbo yao maana hawana uhakika kama raisi ajaye atawapa nafasi walizonazo sasa.
Kwa muda mrefu sasa Spika Ndugai amekuwa akibehave kama kikaragosi fulani kisichojielewa kwa kuwa bussy kulinda positions za serikali hata kwenye mambo ya hovyo badala ya kusimama kidete kuisimamia serikali ifanye mambo sawasawa.
Alianza mambo yake ya hovyo wakati wa sakata la Tundu Lissu kwa kudai hajui alipo wakati anajua alipo na barua kati ya ofisi na familia za Lissu zipo, Akaja kwenye suala la CAG wakati ule akiwa ni profesa Assad, anekuwa akioneanea wabunge wa upinzani ndani ya bunge, Baadae akamtwaa mtu aliyehamia CCM na kumfanya kuendelea kuwa mbunge kwa tiketi ya Chadema wakati mbunge huyo amekaribishwa CCM na viongozi wa chama cha mapinduzi na kauli ya kuhamia chama hicho kaitoa mbele ya media, Sasa Funga kazi ni hii, ya KUTAKA MIHULA YA URAISI IBADIRISHWE RAISI AENDELEE KUKAA MADARAKANI.
Huyu naye eti ni Spika, Spika wa ajabu kabisa ambaye badala ya kuangalia future ya nchi yeye anaangalia maslahi ya muda mfupi ya kisiasa
Kwanza, ajue, au afundishwe na aelimishwe, kuwa, Vipindi katika katiba viliwekwa miaka ya 1980's baada ya Taifa kutambua kuwa sababu mojawapo ya mataifa mengi ndani ya Afrika kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, Mapinduzi ya mara kwa mara ilikuwa ni kukosekana kwa succession plan, yaani utaratibu mmoja wa kupasiana kijiti cha madaraka kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, hali hiyo ilitengeneza sintofahamu iliyopelekea mambo ya mapinduzi. Je Ndugai anataka kutengenezea nchi yetu Utaratibu wa watu kuingia Msituni au Maasi ya Kijeshi kumuondoa mtawala wasiyemtaka?
Je Ndugai anataka nchi yetu ianze kutawaliwa kama nchi za Kifalme?, Maana ukiondoa term limit huwezi kuandika kuwa hiyo ni kwa ajili ya Magufuli tu, maana Magufuli ni binadamu siku akifa maana yake atakeyakaa kwenye hicho kiti atakuta akina Ndugai wameshamuandalia mazingira na yeye kuwa mfalme. Nchi gani ya ajabuajabu akina Ndugai wanataka kuirithisha vizazi vyetu?
Lakini Kauli ya Ndugai pia ni matusi kwa maraisi wetu mzee Mwinyi, Mkapa na Kikwete, maana hata hao pia wangewasikiliza watu wanaotaka tubadili katiba ili waendekee kutawala huenda hadi leo hii Mzee Ruksa au Mkapa au Kikwete ndiye angekuwa bado raisi, Je ina maana hawa wazee wetu walioheshimu vipindi vyao vya utawala na ambao waliignore kauli za wachunia tumbo walikuwa wajinga?
Ni aibu kubwa, tena ni aibu kubwa mno Taifa kuwa na Spika, mtu wa aina ya Ndugai. Yeye anaangalia nafasi yake ya uspika badala ya kuangalia faida pana za nchi ya kwa nini waasisi na viongozi waliofuata waliamua uamuzi wa busara kabisa wa kuweka vipindi vya uongozi. Waliweka hivyo ili iwe kama njia ya kufungua madirisha kila baada ya miaka kumi Taifa lipumue!
Yaani Ndugai anataka kuiambia nchi na CCM kuwa Taifa Zima halina mtu kama Magufuli?, Nyerere alikuwepo na kwa vigezo vyote alikuwa bora mara 90 kuliko Magufuli lakini busara zilimuongoza na kusema kuwa kwa kweli ili nchi yetu iwe na amani lazima tuwe na vipindi vya uongozi.
Na Ndugai aelewe, hii nchi haihitaji mtu mmoja kuiongoza ifanikiwe, hii nchi inahitaji mifumo mizuri na thabiti, badala ya kudhani ili Tuendelee tunamhitaji Magufuli, aanze kufikiri kuwa ili tuendelee tunahitaji mifumo iliyoimara, inayoweza kujiadjust kipindi tukipata kiongozi mwendawazimu na ambayo. itatoa ushirikiano mzuri pindi tukipata kiongozi mwenye hekima.
Ndugai na genge lake waache maslahi binafisi ajue tu kuwa Magufuli ni binadamu, ipo siku atazeeka, ipo siku atakufa Sasa asiliweke Taifa zima katika mikono ya mtu mmoja as if huyo mtu ataishi milele!. Leo unataka kubadili katiba Magufuli aendelee kutawala, kesho akiwa hayupo kwa sababu ambazo. nimezitaja kisha akaja mtawala kama Bokassa, Ndugai anataka Taifa tuendelee kutawaliwa naye kwa miaka lukuki isiyo na kikomo?
Ndugai na genge lake wasiijengee nchi mazingira ya kushawishi mapinduzi ya kijeshi na maasi katika nchi kwa kuondoa vipindi vya uongozi ambavyo hekima ya kuviweka ni kudiscourage vitu kama hivyo!
Ndugai umetukosea heshima sana Watanzania, Jiangalie!!