Ndugai alijianda kuwatoa kina lisu bungeni

mbasajohn

JF-Expert Member
Mar 14, 2009
247
39
ukifuatilia kwa makin utaona toka bunge linaanza leo tareh 28 july 2011 utagundua kuwa Mh. Ndugai (naibu speaker) alikuwa amejpanga kuwatoa wabunge wa CDM kwan toka anaanza alikuwa akcctza kanun inayohusu kuwatoa wabunge bungen hasa kwa kuongea bila kufata kanun. Kwa nn nasema hv baada ya kufungua tu bunge mweshmiwa ndugai alisoma kanun hi.
Pili baada ya matangazo mh ndugai alisoma na kufafanua kanun h.
Kwann nasema alpanga kuwatoa wabnge wa cdm na sio wengne, kwanza hotuba ya Lema alikuwa nayo tayar na pengne hata mwongozo wa Lukuvi alikuwa nao na aljua Lukv k2mia mda mrefu kchambua hotuba ya Lema na aljua kabsa makamanda wa CDM wasingekubal upuuz huo.
Naomba kuwasilisha.
 
Kuna kwa kaukweli kwenye madai yako. Mh Lukuvi wakati anaomba mwongozo (anahutubia) alisema maneno haya, "tulitaka bejeti yote isomwe kama ilivyo ili watanzania waisikie". Je, nani hao anaowasemelea 'tulitaka'?

Nadhani kupitia bunge ccm wanataka kujenga picha kuwa CHADEMA ni watu wa vurugu au wachochezi wa vurugu. Lakini ningefurahi kama angetokeza mmoja wa wabunge wa ccm (mmoja tu) aseme kuwa hakuna rushwa polisi, hakuna tatizo la kesi za kubambikiwa? au polisi hawajauwa raia wasio na hatia. Atokeze mtu ccm akanushe hayo.
 
Ndugai namuheshimu sana kama mtu ambaye nilisoma naye enzi zetu. Lakini kwa alichokifanya jana naanza kuwa na wasi wasi na umakini wake. Sitaki kuamini kwamba kanuni hazijui, la khasha.

Haiwezekani msemaji wa kambi Rasmi ya upinzani anawasilisha hoja halafu wewe Naibu spika unamwambia ruka hiyo paragrafu, eti soma inayofuata. Maana yake nini, na kanuni ipi ya bunge inaruhusu spika kufanya hivyo.

Akina Lissu wakataka kujua kulikoni, hawakupewa muda ila Lukuvi yeye aendelee kuhubiri kwa muda anaotaka. Lukuvi kakuwa msemaji, alisimama kuomba mwongozo, kwa nini aliachwa aanze kujibu hotuba ya Lema wakati waziri mhusika ndiye angekuja kujibu?? Wapi bwana hapa inaonekana wazi alikuwa amepanga kuwatoa.

Haiwezekani kusema eti: Nimewaona watu wa3 wamekiuka kanuni kwa kuongea bila ruhusa. Bunge zima lilikuwa linapiga kelele wakati huo, lakini akasema amewaona wabunge watatu tu, tena wote wa CDM. Huu ni uonevu wa hali ya juu, na hakuna anayeweza kuvumilia.

Mimi nasema nchi hii ikiingia kwenye machafuko, ni ccm na serikali yake ndo wakulaumiwa. Full stop...
 
nakubaliana nawe kuwa walipanga kuwatoa nje wahusika kutokana na mlolongo wa matukio ulioutaja. kinachonishangaza mimi ni watu kuangalia tukio la pili la wahusika kuongea kwenye vipaza bila ruhusa ya spika na kuliacha kosa la kwanza la LUKUVI kutumia muda mwingi kujibu hoja wakati wabunge wengine hawaruhusiwi. kumbukeni kosa la pili lisingekuwepo bila la kwanza kuruhusiwa na wahusika hii ni sawa na mtu kukupiga ngumi halafu unaambiwa huruhusiwi kurudishia kwani ukirudisha unakuwa umevunja sheria. this is insane.
 
Every man gotta right to decide his own destiny,
And in this judgement there is no partiality.
So arm in arms, with arms, we'll fight this little struggle,
'Cause that's the only way we can overcome our little trouble.

Brother, you're right, you're right,
You're right, you're right, you're so right!
We gon' fight (we gon' fight), we'll have to fight (we gon' fight),
We gonna fight (we gon' fight), fight for our rights!

No more internal power struggle;
We come together to overcome the little trouble.
Soon we'll find out who is the real revolutionary,
'Cause I don't want my people to be contrary.
 
Sielewi,,,,,mi sielewi,,,yani sielewi kabisa,,,,,,na naomba mnieleweshe hawa wabunge na hasa wale waongoz bunge wanafanya vile kwa utashi waooooo auuuuuuuu???????
 
Kama tutashikilia kulaumu bila ya kujitazama wenyewe kwanza, naamini hata nafasi yetu itakapofika itatukuta hatupo tayari
 
Ni kweli ilipangwa kwani Ndugai alifanya maamuzi hayo fastafasta bila kuonyesha kuwa alitafakari jambo hilo kwanza, halafu kama ni kelele mbona zilikuwa nyingi tu zaidi ni zile zile kutoka upande wa ...Ndiyooooooo au kutoka wale jamaa wa...Naunga mkono bajeti mia kwa mia halafu wanaanza kutaja mlolongo wa matatizo ya watu wao.
 
Ukijaribu kufuatilia mwenendo mzima wa vikao bungeni hasa nyakati hizi, hukawii kuelewa kuwa wabunge karibu wote wa ccm ajenda yao kuu ni kupinga kila kinachoibuliwa na wapinzani..
Bunge zima linatakribani ya wabunge 360 (nisahihishwe kama nimekosea) wale wa upinzani nao wanafika arobaini na kitu..kufanya idadi niliyoitaja hapo awali. Mara zote wabunge wa ccm wamekuwa wa kwanza kupinga hoja zote za upinzani kana kwamba yanayosema na upinzani ni uwongo. Mfano ripoti ya kituo cha sheria na haki za binadam inasema watu52 wamekufa mikononi mwa polisi, hili ni jambo lililowazi kabisa.. Mbunge wa upinzani anapotaka kuonesha ukiukwaji wa haki ulofanywa na polisi Mjinga Flani Lukuvi anaibuka kuomba mwongozo akiwa na jazba kupinga hayo yalosemwa.. Huu ni ujuha kabisa
Mbona mara zote hatujawahi kusikia wapinzani wamempinga paragraphy flani isisomwe? Iweje leo hii wazuiwe kutujuza madhila ya serikali ambayo tunapaswa kuyafahamu?
Ndugai, Makinda, Lukivi na wote mliokaa kishabiki bila kuweka mbele maslahi ya waliowapa dhamana ya kuwaongoza siku inakuja mtakaposema kuwa..mlipitiwa na pepo mbaya ndio mkapinga yote ya wapinzani.. Na msipotubu Mungu atawahukumu... kwa sababu mmepofushawa na kuamini kuwa mpo juu ya sheria.. Hivo mnaweza kufanya lolote lile.
NAUMIA SANA.
 
mishale ya Mh G. Lema ilikuwa ya moto, ni lazima wapagawe. Huo ni mwanzo kila kituko cha CCM ni njia ya ukombozi wa watanzania. Viongozi wa Bunge hawana busara na wanauwezo mdogo sana kufikiri. Ila Lema aliwaambia ni nchi isiyolinda haki za raia wake, ikumbukwe na wabunge ni raia. Kwa hiyo ukiwa CCM kwa sasa wewe huna kosa. Ila wananchi wanaona.
 
ukifuatilia kwa makin utaona toka bunge linaanza leo tareh 28 july 2011 utagundua kuwa Mh. Ndugai (naibu speaker) alikuwa amejpanga kuwatoa wabunge wa CDM kwan toka anaanza alikuwa akcctza kanun inayohusu kuwatoa wabunge bungen hasa kwa kuongea bila kufata kanun. Kwa nn nasema hv baada ya kufungua tu bunge mweshmiwa ndugai alisoma kanun hi.
Pili baada ya matangazo mh ndugai alisoma na kufafanua kanun h.
Kwann nasema alpanga kuwatoa wabnge wa cdm na sio wengne, kwanza hotuba ya Lema alikuwa nayo tayar na pengne hata mwongozo wa Lukuvi alikuwa nao na aljua Lukv k2mia mda mrefu kchambua hotuba ya Lema na aljua kabsa makamanda wa CDM wasingekubal upuuz huo.
Naomba kuwasilisha.

Kwa kitendo cha kudhalilishwa wakina Lissu, Msigwa na Lema, inabidi wajiuzulu, kwani hawana heshima tena mbele ya jamii, napenda kuwasilisha !
 
Ukweli siku zote unauma. Hayo yanayoelezwa kuwa ni uchochezi katika hotuba ya Lema mbona hawayakanushi?? Walitakiwa wayakanushe halafu ndiyo lifuate la uchochezi lakini kama hawayakanushi maana yake yana ukweli na kama yana ukweli basi hayawezi kuwa uchochezi. Serikali ya magamba ijifunze kukubali kukosolewa kwa kuambiwa ukweli. Kama ni rushwa ipo kila mahali tena siku hizi sio kwa kificho, kama ni watu kubambikiwa kesi na polisi sio siri, kama ni polisi kuua raia kiholela tunayashuhudia, kama ni madini yetu yanachukuliwa na wanaoitwa wawekezaji kwa faida yao na wale wateule wa magamba, kama ni wanyama wetu kwenye mbuga wanachukuliwa wazima wazima na kupelekwa arabuni, sasa hivi nchi inauzwa kwa wamarekani kwa kupewa maelfu ya ekari za ardhi, kama ni mikataba mibovu imeshatuangamiza tumekwisha, kama ni elimu imeshaporomoka kiasi kwamba inaonekana ni elimu ya msingi mpaka chuo kikuu, kama ni mipaka ya nchi yetu iko wazi masaa 24 watu wanaingia na kutoka na kuchukua wanachotaka wapendavyo serikali inakoroma, wanajeshi nao manameremeta tu, umeme ndiyo huo unatuaga na kuishia, uchumi umeporomoka, jamaa anaendelea ku-fly kama mwewe, watu wanaitafuta shilingi haipatikani, semina elekezi ndiyo hiyo walifundishana kuhongana ili waongee kwa kauli moja walipoona limevuja haraka haraka wakajilipua wenyewe sasa wanatafuta namna ya kuweka mambo sawa kwa ile imani waliojijengea "Wanaongoza mataahira". Kubwa zaidi wametuletea misamaki yenye sumu sasa ili tule tuishie. SERIKALI LEGELEGE itatumaliza
 
huu ujinga ukiendelezwa cdm watoke wote bungeni hizo hoja ziletwe kwa wananchi ccm hawataki zisemwe bungeni ccm hawalari usingizi poropaganda zote wamechemusha siraha yao iliyo baki nikuwatimuwa wabunge mbowe mtoke wote tuingie barabarani
 
IPO SIKU! IPO SIKU! IPO SIKU INAKUJA!
INANIUMA SANA,INANIUMA SANA INANIUMA SANA................IPO SIKU INAKUA......
WAZALENDO WATASHINDA NAKUAMBIA....IPO SIKU NASEMA
HAKIYANANI TUTASHINDA .....TUTASHINDA NASEMA TUTASHINA...
NAWAAMBIA WABUNGE WOTE WAliokaa kishabiki bila kuweka mbele maslahi ya waliowapa dhamana ya kuwaongoza siku inakuja watakapotamani walau wakakae kwenye viti vya wageni pale bungeni lakini hawataipata!. Nawambia wasipobadilika Mungu atawahukumu.kwa sababu wanaamini kuwa wapo juu ya sheria na kuamua kufanya lolote lile.
INANIUMA SANA. IPO SIKU NASEMA >.....IPO KARIBU SANA!
 
Back
Top Bottom