Ndoto ya ajabu inayojirudia rudia na mikasa niliyopata inanifanya nichanganyikiwe

angwisa1

New Member
Oct 13, 2016
3
2
Habari za mapambano wana Jf?

Mimi ni kijana wa miaka 27 ni muhitimu wa chuo kikuuu x na nipo nasubili ajira. Na saivi najishughurisha na bodaboda pia nalima. Kuna ndoto inanijia mara kwa mara yaaani " naota nipo shule nafanya mitihani ambayo ni migumu ambayo simalizi, nyingine nipo kwenye maandalizi ya mtihani yaaan najisomea nakua na hofu ya mtihani kuwa mgumu hofu inapitiliza " pia kuna siku za hivi karibuni nimeota nimefanya mtihani nimefaulu.

Sasa kutokana na tafsiri ya ndoto hizo ambazo nimeziona sehemu mbalimbali kwenye tv na social media inaonesha kama kuna nguvu za giza zinanirudisha nyuma.

Mimi kwa kiwango changu napambana sana yaaani sijabweteka toka nimalize chuo pia nimebahatika kushika hela ad kufikia million 10 maaana nalima pia nafanya biashara mbali mbali changamoto nimeshanunua vitu vingi kama kiwanja mashamba ila nimeuza pia nikitaka kununua kitu kuna roho inakuja ya kunikatisha tamaa.

Yaaani nimesha kubaliana na wateja mbalimbali wa mashamba na viwanja ila sijafanikisha kununua bila sababu ya msingi na mda huo ila inakuwepo.

Pia kunakipindi wakati naendesha boda boda nikiota tuuu ndoto hizo nipo shule yaaan lazima nipate msala barabarani kama sio kukamatwa na polis basi ajari au kukosana na abiria. Nateseka sana na hiii hali najaribu kuomba mungu na kushirikisha watumishi tofauti wananipa moyo.

Kama umewai kukutana na tatizo hili au ata kulisikia naomba msaada wako.

Ninabahati ya kushika hela pia kukubarika na watu ila sina ata maendeleo ata kidogo.
 
Asikudanganye mtu , ndoto hiyo ni ya kawaida sana hasa kwa watu waliokuwa wanasoma sana wakiwa shuleni ! Kuota upo shule unafanya mtihani au unajiandaa na mitihani ni jambo la kawaida na watu wengi sana wanaota ndoto hizo.

Hii ni kwa sababu mda mwingi wa maisha yako umeutumia kwenye kusoma!

Suala la ndoto hiyo kutafsiriwa kuwa mambo yako yanarudi nyuma ni UONGO MTUPU! Watu wengi wana maisha mazuri na mambo yanaenda fresh tu ila daily wanaota ndoto hizo.

Ushauri wangu: Achana na kuamini mambo ya ndoto! Mimi nilishajitoaga kwenye kuamini ndoto na hazitokei kamwe!

Nikiota ndoto huwa naipuuza na kuksemea kwamba ndoto zangu huwa haziwi kweli, na matokeo yake haziwi kweli
 
Endelea kuomba utafanikiwa zaidi,

Kuota umefaulu mtihani, ni Ishara kuwa Kuna kihunzi umekiruka salama. Na matokeo yake utayaona soon.

Ukiomba zaidi zitakujia ndoto ukivuka stage, ikiwa uliota uko shule ya msingi, utaota uko secondary, baadae chuo na kuhitimu, baadae kazini na kuendelea.

Si Rahisi ufanikiwe wakati hujahitimu mitihani, mtu halisi Yuko katika ndoto anazoota Ulimwengu wa Roho, huku mwilini ni matokeo.

Ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom