Ndolanga achezea kichapo msikitini

Status
Not open for further replies.

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,558
25,323
Habari nimezisikia ya kuwa Muhidini Ndolanga kachezea kichapo cha maana msikitini magomeni ambapo yeye ni mjumbe wa bodi ya wadhamini wa msikiti huo wa mchangani.

Imeelezwa kulikuwa na sintofahamu kuhusu maswala ya msikiti huo iliyopelekea kudundwa, kuchaniwa kanzu, kupotezewa kobazi hadi kufadhiliwa kanzu ya mtumba nje ya msikiti.

Hali ilikuwa mbaya kwani walimtoa ngeu waumini waliochachamaa, singlendi yake ilikuwa na mabaka/madoa ya damu, alionekana akitolewa nje baada ya kuokolewa na baadhi ya waumini.
 
Hapo tu ndiyo nawapendea ndugu zangu waislamu. Wao hawajui kukopesha, unafanya mzaaa unapewa hapohapo. Hakuna cha kusubiri.

Nasubiri Jesuit, Malaria Sugu, Faizafox n.k. waje tuone mambo!
 
Kama ni kweli, wala sishangai. Njia nzima aliyopita ameacha finger print zake,kuanzia Loliondo miaka ile ya Mwinyi, akaja FAT na mwenzake Rage. Ni mazoea ambayo hujenga tabia ya kufikiri unbaongoza watu katika jamii, kama unavyoongoza watoto wako nyumbani
 
Yule si alikuwa na a.k.a ya Tyson! Huwezi jua anaweza akawa yeye ndo kawadunda wenzie, maana amewahi kumchapa Matep Quaresi enzi za kuuza vitalu vya uwindaji
 
Ndolanga ana Hati Chafu... na Yule ni Zaidi ya Mswahilina Nakumbuka Office Yake pale Raha Tower nilishaenda kutoa Photocopy alikuwa anafukizia Udi time zote za kazi ukiingia kama huna ustahimilivu uvae mask otherways lazima uchezee kikohozi Office hadi inakuwa Giza kwa Moshi ya Udi na Ubani...

Nilikuwa najua Jamaa ni Mwanga kwa Mambo niliyoyaona pale kwa Office yake na Ujeuri aliokuwa nao kwa Taifa alipolitunishia kifua kwa Fifa Tufungiwe tusicheze hadi yeye arejeshwe Madarakani wakati ni Kiongozi Mbovu na Si muaminifu...

Nakumbuka kauli yake aliyomuambia Abdallah Majura kuwa yeye ni Kiongozi wa FAT na Mpira Sijui...
 
Ilikuwa ni jana baada ya swala,Ndolanga akachukua mike nakuanza kuwatangazia waumini kuwa kuna mabadilliko ya uwongozi,na kusema kuwa ma imam wasaidizi wawili mikataba yao imekwisha watachaguliwa wangine,ndipo hapo watu wakaanza kuhoji yeye kama nani na katokea wapi wakati wanajua yeye hupenda kuswali msikiti wa manyema......wanajua kilichompekapale ni pesa,ule msikiti na miradi mingi sana na mfadhili mwenye mshiko....ndipo zongo lilipo anza japokuwa Ndolanga alikuwa amekuja na mabaunsa wa nne lakini walishindwa kumsaidia,asichezee makofi,yule mzee alichezea makofi mengi sana kutoka kwa vijana pale,baadaye walipiga tanganyika jeki akiwa pekupeku wakampeleka kituo cha polisi usalama magomeni.......
 
hah hah kumbe dini siku hizi nazo ni dili eeeh? Mola uwasamehe wote hawajui walitendalo.
 
Ilikuwa ni jana baada ya swala,Ndolanga akachukua mike nakuanza kuwatangazia waumini kuwa kuna mabadilliko ya uwongozi,na kusema kuwa ma imam wasaidizi wawili mikataba yao imekwisha watachaguliwa wangine,ndipo hapo watu wakaanza kuhoji yeye kama nani na katokea wapi wakati wanajua yeye hupenda kuswali msikiti wa manyema......wanajua kilichompekapale ni pesa,ule msikiti na miradi mingi sana na mfadhili mwenye mshiko....ndipo zongo lilipo anza japokuwa Ndolanga alikuwa amekuja na mabaunsa wa nne lakini walishindwa kumsaidia,asichezee makofi,yule mzee alichezea makofi mengi sana kutoka kwa vijana pale,baadaye walipiga tanganyika jeki akiwa pekupeku wakampeleka kituo cha polisi usalama magomeni.......

Panga la shaba nakushukuru kwa kutoa ufafanuzi.
 
Hii mpya, ina maana ndugu zetu waislamu hatuna moyo wa kuvumiliana na kuchukuliana?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom